Tuesday, October 16, 2012

KWANINI KUNA MAHINDI YA NJANO NA MAUPE?

 MAHINDI YA NJANO....
Na hapa ni mahindi MEUPE ambayo mimi binafsi nimeyazoea tangu nilipokuwa katoto kadogo. Ndiyo, nimewahi kuona mahindi mekundi meusi au mchanganyiko lakini hayo ya njano sijawahi kuona Tanzania yetu. Je? kwanini?

5 comments:

  1. Wakaaji wa Ulaya waligundua mhindi mnamo 1492 baada ya mvumbuzi Christopher Columbus kuwasili katika visiwa vya Karibea. Ferdinand, mwana wa Columbus aliandika kwamba baba yake aliona nafaka “wanayoita mahindi na ina ladha tamu sana ikichemshwa, ikichomwa, au ikisagwa na kuwa unga.” Aliporudi nyumbani, Columbus alibeba mbegu, na “kufikia katikati ya miaka ya 1500,” Kastner anaandika, “[mhindi] ulikua huko Hispania, Bulgaria, na Uturuki. Wafanyabiashara ya watumwa walipeleka mahindi barani Afrika . . . Wafanyakazi wa Magellan [Ferdinand, mvumbuzi Mhispania aliyezaliwa Ureno] waliacha mbegu kutoka Mexico nchini Filipino na Asia.” Mahindi yalikuwa yameanza kutumiwa kwa wingi.
    Siku hizi, mhindi ni nafaka ya pili kutumiwa kwa wingi zaidi baada ya ngano. Mchele ni nafaka ya tatu kutumiwa kwa wingi zaidi. Nafaka hizo tatu zinawalisha wanadamu wengi, na pia mifugo.
    Kuna aina nyingi za mhindi. Kwa kweli, huko Marekani pekee kuna zaidi ya aina 1,000, kutia ndani mbegu zilizochanganywa. Mimea hukua kufikia kimo cha kati ya sentimita 60 hadi mita 6! Pia urefu wa bunzi hutofautiana. Nyingine zina urefu wa sentimita 5; huku nyingine zikifikia urefu unaostaajabisha wa sentimita 60. Kitabu Latin American Cooking kinasema hivi: “Aina fulani za mhindi unaokuzwa leo huko Amerika ya Kusini, hutokeza bunzi kubwa zilizo na umbo la mpira wa miguu, zenye mahindi yenye urefu wa sentimita 2.5 na upana unaokaribia huo.”
    Pia mahindi yanakuwa na rangi tofauti-tofauti. Mbali na manjano, bunzi linaweza kuwa na rangi nyekundu, bluu, pinki, au nyeusi. Nyakati nyingine, mahindi yanaweza kufanya bunzi lionekane kuwa na mistari au madoadoa. Inaeleweka basi kwa nini badala ya kupikwa mara nyingine mahindi yenye rangi tofauti yanatumiwa kutengeneza mapambo.
    Nafaka Yenye Matumizi Mengi
    Kuna aina nyingi za mahindi zinazogawanywa katika vikundi sita vikuu: dent, flint, flour, sweet, waxy, na popcorn. Mahindi aina ya sweet hayakuzwi sana kama aina nyingine. Utamu unaopatikana katika aina hii ya mahindi unatokana na kasoro fulani ambayo huizuia kubadili kiasi cha kutosha cha sukari kuwa wanga. Zaidi ya asilimia 60 ya mihindi inayokuzwa ulimwenguni hutumiwa kulisha mifugo huku asilimia 20 hivi ikilisha wanadamu. Asilimia inayobaki hutumiwa viwandani au kama mbegu. Bila shaka, matumizi hutofautiana katika nchi mbalimbali.

    ReplyDelete
  2. Kaka Ray! Ahsante sana kwa historia hii ya mahindi.

    ReplyDelete
  3. Dada Yasinta wewe kwani hukula ule ugali wa yanga kipindi kile cha njaa? pop corn je? haya mahindi yana ladha tamu sana na pia yana virutibisho zaidi kuliko m eupe

    ReplyDelete
  4. Mie nadhani ni mbegu tu!, hata mekundu yapo na meusi/zambarau sjui ila unakuta yako mchanganyiko changanyiko

    ReplyDelete
  5. Shukrani Kwa historia uliyotupa

    ReplyDelete