Picha hii imenikumbusha enzi zile miaka arobaini na saba familia nzima inajumuika pamoja na kushika chakula kiwe cha asubuhi, mchana au jioni. Hakika hii ilikuwa safi sana...kukaa hivi na familia yote kwenye mkeka/mpasa na kula chakula. Raha sana, halafu sasa muwe wengi hapo ndiyo chakula kita/kinanoga zaidi... Ila kuna baadhi ya watu wakiona watu wamekaa hivyo na kula chakula kwa mikono basi wanafikiri kuwa wana hali mbaya ..hapana hii ni moja ya tabia zetu yaani mila na desturi ambazo ni nzuri tu... ...je wewe nawe umekumbuka nini katika hili?
JUMATANO NJEMA NA UKIPATA NAFASI KULA NA JIRANI YAKO AU RAFIKI.
dada Yasinta ndio ninachokupendea hicho hapo yaani umenikumbusha mbali sana hapo hata chakula kinaingia tumboni vizuri sana,vilevile kula na mikono ni faradhi kwani ndio asilia hiyo maana ndivyotulivyozaliwa,ila huyo mwenye shati ya buluu sijui ndiye mkuu wa familia maana sisi kwetu huko Bukoba ukiwa mtoto na kukaa hivyo hapo lazima utakula viboko yaani(kulya otandamile)lakini kama yeye ndiye mkuu wa familia hapo ni ruksa maana ndiye kijogoo wa familia asante sana kwa kumbukumbu murua
ReplyDeletebatamwa! Ahsante nawe wapendwa...Yaani wakati mwingi ilikuwa ukishakula hakuna haja ya kutafuta kitanda ni kupumzika hapohapo...Batamwa ni kweli hata kwetu mtoto kukaa hivyo mmmhh haingewezekana..nashani ni kweli huyu atakuwa baba wa nyumba. Kwetu baba alikuwa akikaa kwenye kigoda/au kitu kidogo cha mkalio wa nyani....nawe asante kwa kunikumbusha hili.
ReplyDeleteZoea la Kula Pamoja Linatoweka
ReplyDeleteKutoweka kwa zoea hili la kula mlo wa pamoja katika kipindi ni uthibitisho ulio wazi wa kubadilika kwa mazoea ya familia ya kuwasiliana,Ni mambo gani yanayochangia kubadilika kwa tabia za watu?
Kwanza, gharama ya juu ya maisha imewalazimu waume kwa wake wafanye kazi kwa saa nyingi.
Wazazi wasio na wenzi, ambao mara nyingi hali yao ya kiuchumi huwa ngumu hata zaidi, huwa na wakati mchache zaidi wa kuwa pamoja na familia zao.
Pili, pilkapilka za maisha ya sasa huwafanya watu wakimbilie vyakula vyepesi na vinavyotengenezwa haraka-haraka.
Si watu wazima peke yao walio na majukumu mengi, hata watoto huwa na mambo mengi ya kufanya kama vile michezo na shughuli nyingine za baada ya shule.
Kwa kuongezea, akina baba wengine hupenda kufika nyumbani baada ya watoto wao kulala ili kuepuka kelele za watoto.
Wazazi wengine wanaofika nyumbani mapema huamua kuwapa watoto wao chakula kwanza, ili watoto walale mapema na kuwapa mume na mke nafasi ya kula pamoja kwa utulivu.
Hali kama hizo hufanya familia isile pamoja. Badala ya mazungumzo wakati wa mlo, washiriki wa familia huwasiliana kwa kubandika vikaratasi vyenye ujumbe kwenye friji.
Kila mshiriki wa familia anapofika nyumbani, hupasha moto chakula ambacho tayari kimepikwa na kuanza kutazama televisheni, kutumia kompyuta, au kucheza michezo ya video.
Huenda tabia hizo katika kijamii zikaonekana kuwa haziwezi kubadilishwa.
Hivyo, je, inafaa kufikiria kwa uzito jinsi ya kuacha tabia hizo?
Kaka Ray! Ulichosema ni kweli kabisa na naweza kusema inasikitisha kwasababu huo ndio muda mzuri sana wa kuwasiliana, kuwauliza wtoto,mke, na mume siku yake ilikuwaj?..Hili jambo inabidi kulifanyia kazi kwani kama sisi tulikua na kuwa hivi tulivyo balia hiyo michezo watashindwa wao kwa nusu saaa mpaka saa moja kwa kukaa pamoja na kula mlo?
ReplyDeleteNdiyo! sitaki au sisemi kuwa najidai HAPANA ila mimi huwa najitahidi sana kila jioni tuwe pamoja mizani na kula na pia kuna wakati huwa komputa, televisheni,hata redio havifunguliwi ni kuongea tu na kucheza michezo mingine kama karata nk. Nadhani hii inategemea vipi wenyewe mnbapanga.
Hii ni changamoto yetu sote!!
ReplyDeleteFAMILIA ILIUMBWA AU ILIKUSUDIWA IWE NI UJAMAA FULANI HIVI!Picha hii inafurahisha bila kujali mazingira,Umoja na ushirikiano!
ReplyDeletehapo Yasinta ndio kama ulivyosema wafanyakazi wenzio walivyokuuliza ndio upendo unaanzia hapo kama ulizoea kula chakula pamoja ukila peke yako inakuwa tabu kama unakula kama vile unafukuzwa au kamavile umekikwapua mahali furani
ReplyDelete