Mbunge wa jimbo la Kilolo Iringa Prof.Peter Msolla akitazama nyama ya kitimoto
iliyokuwa ikiuzwa mnadani eneo la Nyanzwa mapema mwaka jana
SERIKALI Iringa yapiga uchinjaji na uraji wa
nyama ya nguruwe (kitimoto) baada ya kuibuka upya kwa ugonjwa wa homa ya Nguruwe
uliopelekea nguruwe zaidi ya 100 katika Manispaa ya Iringa na Iringa vijijini
kufa kwa ugonjwa huo.
Ugonjwa huo unatishia maisha ya Nguruwe
36,179 wenye thamani ya shilingi bilioni 5, 426,850,000 kwa upande wa wilaya ya
Iringa vijijini pekee huku katika Manispaa ya Iringa nguruwe 2812 zenye thamani
ya shilingi milioni 421,800,000 wapo hatarini kukumbwa na ugonjwa huo.
Kaimu afisa mifugo wa wilaya ya Iringa
vijijini Said Kolwa aliueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com leo
kuwa kutokana na kuwepo kwa ugonjwa huo katika wilaya hiyo ya Iringa tayari
serikali imechukua hatua mbali mbali za kunusuru maambukizi zaidi ya ugonjwa huo
ikiwa ni pamoja na kuzuia uchinjaji wa nguruwe katika wilaya nzima ya
Iringa.
Alisema kuwa Halmashauri ya Iringa ilipokea
tarifa ya kuwepo kwa vifo vya nguruwe katika kata ya Lyamungungwe juni 28 mwaka
huu ambapo ufuatiliaji ulifanyika kuanzia Juni 30 hadi Julai 2 na kubaini kuwepo
kwa ugonjwa huo katika vijiji vya Kikombwe ,Igunda hivyo kuchukuliwa Sampuli
ambazo baada ya kupimwa ilibainika ugonjwa huo.
Kwani alisema katika kijiji cha Kikombwe
jumla ya mazizi 5 yenye nguruwe 14 yalikuwa yameambukizwa na kati ya nguruwe 7
walikufa na kijiji cha Igunda jumla ya mazizi 10 yenye nguruwe 14 yalikuwa
yameambukizwa na kati yao nguruwe 28 walikufa kwa ugonjwa huo.
Kolwa alisema kuwa ugonjwa huo unadaiwa
kuingizwa na mmoja kati ya wafanyabiashara wa nyama ya nguruwe ambaye aliingiza
kwa siri nguruwe katika kijiji cha Igunda akitokea kata ya ukumbi wilaya ya
Kilolo ambayo imekubwa na ugonjwa huo.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na ugonjwa
huo tayari ofisi ya mganga mkuu wa wilaya hiyo Dr .Mathias Matandala imetoa
tangazo la tarantini juu ya ugonjwa huo wa homa ya nguruwe (African Swine
Ferver) ikiwa ni pamoja na kuzuia biashara zote za nguruwe na nyama ya nguruwe
katika wilaya hiyo pia kuingiza wala kutoa nguruwe katika wilaya hiyo.
Wakati kwa upande wake afisa mifugo katika
Manispaa ya Iringa Dr .Augustino Nyeza alisema kuwa katika Manispaa ya Iringa
ugonjwa huo ulibainika Juni 24 katika kata ya Mkwawa ambapo wafugaji wa nguruwe
katika eneo la Don Bosco na Makanyagio ndio nguruwe zao zilianza kukumbwa
ugonjwa huo na kusababisha vifo vya nguruwe 80.
Hata hivyo alisema hatua zilizochukuliwa hadi
sasa ni kufunga machinjio mawili yalipo katika Manispaa ya Iringa katika eneo la
Ipogolo na mjini pia kufunga vibanda vyote vya kitimoto na maeneo yote ya uuzaji
wa kitimoto mjini Iringa .
Alisema kuwa mizoga yote ya nguruwe waliokufa kwa
ugonjwa huo ilifukiwa chini ya ulinzi makali na mabanda 118 ya nguruwe
yalipulizwa dawa .HABARI NA PICHA KUTOKA http://francisgodwin.blogspot.se.
Duh! bila kitimoto mbona kazi sana pole sana ndugu zangu/watani wangu..
ReplyDelete@Yasinta;
ReplyDeleteKuadimika kwa kitimoto hazuii kasi ya gurudumu la maisha na mafanikio kwa kuwa kitimoto ni hamu tu lakini mboga ni dagaa na matembele.
สล็อตออนไลน์ที่ได้เงินเยอะ
ReplyDeleteได้เงินจริง epicwin ฟรีเครดิต
https://www.slotxd.com/epicwin