Thursday, April 26, 2012

TUKUMBUKE METHALI ZETU!!!

1. Shida ingekuwa sumu tungekufa wengi.
2. Mwisho wa biashara yoyote ni faida au hasara.
3. Mpe akupaye, ukimpa asiyekupa ni sawa na kutupa.
4. Nyumba ya udongo haipingwi deki.
5. Hata mbuyu ulianza kama mchicha.
6. Kucheke sio dalili ya wema kwa mwenzio.
7. Usilie kwa kupigwa lia kwanini umepigwa
8. Akupendaye katika shida ndiye rafiki wa kweli.
9. Raha ya pilau ni kula kwa mkono
10. Usimchokoze kichaa ukiwa unakaa kwenye nyumba yenye vioo.
KILA LA KHERI.

4 comments:

  1. Yasinta...Hizi ni methali kweli au misemo, mbona kama naanza kusahau tena...

    Ubarikiwe sana dadangu.

    ReplyDelete
  2. Hata mimi nime kwama kidogo.mfano mtakacha uvunguni jibu lake ,ni lazima ainame.sasa hii nimethali au kitendawili.? maana nakumbuka kuna-methali,kitendawili na Nahau. hebu anaye kumbuka atu pe kidogo,samahani dada Yasinta naomaba msaada hapo.kaka s.

    ReplyDelete
  3. Nipe kitabu nichome,niwafundiche wajinga,hai chindimba!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Jamani, jamani basi itabidi tuanze darasa la Methali, misemo, nahau na vitendawili hapa, nafurahi kwa wazo lenu...na hapo ndipo tutakapojua nini ni nini.
    Ray umenikumbusha huo wimbo:- hai sindimba kwechu kwechu sindimba ngoma ya wamakonde....

    ReplyDelete