Wednesday, April 4, 2012

Je, ni muhimu wanandoa kusalimiana mnapoamka asubuhi?

Sio vinginene tena bali ni kile kipengele chetu cha JUMATANO YA MARUDIO..LEO nimetembelea Njombe kwa kutaka kusoma kazi zake zaizi unaeweza kutembelea Mbilinyi


Kwanza fahamu kwamba wanandoa wanapokaa muda mrefu baadhi ya vitu huanza kuchakaa kimapenzi. Hata hivyo upendo na wema husaidia kurudisha moto wa mapenzi na wanandoa kujiona wapya kila umri unavyozidi kuongezeka.
Matendo yanayoonesha wema kwa wanandoa ni gundi inayoshikisha wawili kujiona wapo karibu na moja ya tendo la wema ni kumsalimia mwenzako wakati mnaamka hata kama mmelala kitandani kimoja na hata mlikumbatiana usiku mzima au ulimuweka mwenzi wako kifuani usiku mzima.
Anayesalimiwa hujiona anapendwa, ana thamani na pia appreciated

+++++++++++++++++++++++++++++++++

Tupo kwenye new millennium kiasi ambacho watu tupo busy hata kuamka tunahitaji kuweka alarm ituamshe hata hivyo badala ya kukimbia bathroom kuoga ni muhimu kumpa kwanza salamu mwenzi wako ndipo uendelee na kazi zingine au na ratiba yako.
Tafiti zinaonesha wanandoa ambao husalimiana asubuhi wanajiona ndoa yao ni nzuri sana na wana mahusiano yanayoridhisha.
++++++++++++++++++++++++++++++++
Je, nini kinafanya maneno ya salaamu ya asubuhi kuwa muujiza katika ndoa na mahusiano?
Unapomsalimia mwenzi wako maana yake unamwambia na kumpa ujumbe kwamba ni asubuhi njema tumeamka pamoja katika upendo na furaha na kwamba unajisikia vizuri kuanza siku mpya na mtu wako na pia unaweza msingi mzuri wa mawasiliana kwa hiyo siku mpya.

-----------------------------------------------------------------------------------------------

Ahsanteni tukutane tena panapo majaliwa..nwatakieni maandalizi mema ya PASAKA!!

4 comments:

  1. `Salaamu' kwa wale waumini wa dini wanajua ina maana gani, hili no moja kati a mjina 99 ya Muumba, kwahiyo utaona kwanini salamu inamiujiza ndani yake.
    Ujumbe murua dada yangu. Tupo pamoja

    ReplyDelete
  2. DAIMA TUDUMISHE ,SALAMU,SAMAHANI,SHUKRANI NA SUBIRA.

    ReplyDelete