Sunday, March 11, 2012

SALAMU ZA JUMAPILI YA LEO : MASIKINI NA PESA YA KUOKOTA!!!

MASIKINI MMOJA ALIKWENDA MAPORINI KUTAFUTA RIZIKI YA KAWAIDA KAMA UJUAVYO KULE VIJIJINI KWETU RUWILA. BASI ALIPOFIKA KATIKA KICHAKA KIMOJAWAPO ALIKUTA KITU KIMEFUKIWA CHINI KATKA KUFUKUA BASI ALIKUTA SANDUKU LA CHUMA LIMEJAA PESA YAANI KAMA NI DOLA BASI NI ZILE DOLA MIA MIA TUPU ,KAMA NI ZILE ZA KWAETU BASI NI WALE WEKUNDU WA MSIMBAZI WATUPU,
BASI YULE MTU ALIKUWA NA IMANI SANA YA KUMWAMINI MUNGU. HIVYO ALIPOZIONA ZILE PESA AKAMWAMBIA MUNGU ,,, HIVI WEWE BWANA MUNGU KWANINI UNANIPIMA MIMI IMANI YANGU KIASI HIKI ? SASA NAKUAMBIA MIMI SICHUKUWI PESA HII HATA CENTI. KAMA NI SHIDA WEWE UNAJUWA NIIPATAVYO. BASI KAMA UMEPANGA KUNIPATIA PESA HII MIMI. UTANILETEA PESA HII NYUMBANI KWANGU. BASI YULE BWANA ALIONDOKA MPAKA KWAKE ,,NA AKAMWELEZEA MKE WAKE YALIYOMKUTA KULE MAPORINI. DUH! MKE WAKE AKAMWAMBIA WEWE MUME WANGU NDIO MJINGA KABISA. SASA KAMA ULIONA NI MZIGO MKUBWA KWANINI HUKUCHUKUA JAPO KIDOGO? YEYE ALIMJIBU KUWA ZILE NI PESA ZANGU KAMA MUNGU ALIIPANGA ZIWE ZANGU, BASI ATAZILETA HAPA NYUMBANI KWANGU.BASA WAKATI WANA BISHANA NA MKEWE AKASIKIA SEBULENI KITU KIMEANGUKA KWA KISHINDO KIKUBWA ,AKAMWAMBIA HAYA PESA IMEKUJA MKEWE AKACHEKA KWA KEBEHI .. YAANI UMEZIACHA PESA HUKO NANI AKULETEE? AKASEMA, MUNGU NIMEMWAMBIA ATAZILETA TUU ,KWELI BWANA KUMBE WATU WAWILI WALIPITA PALE WAKAZIONA WAKAWA WAMECHUKUZANA ,WAKAWA WANA PITA NYUMBANI KWA YULE BWANA KATIKA KICHOCHORO BASI WALIPOFIKA KATIKATI TA NYUMBA ILE KUANGALIA MBELE WAKAONA POLISI WAKATAKA KUGEUKA WALIKOTOKA WAKAONA POLISI DUH! WAKASEMEZANA BWANA HII PESA YA SERIKALI ,,, SASA ,,TUFANYEJE? WAKASEMA HII PESA TURUSHIE KWENYE NYUMBA YA HUYU MASIKINI KAMA KUKAMATWA AKAMATWE YEYE ,, BASI NDIPO WAKAIRUSHIA MLE NDANI NA NDIPO MASIKINI ALIPOSEMA PESA AMELETEWA KUMBE BWANA WALE WALIKUWA MALAIKA SI POLISI MASIKINI AKAWA TAJIRI KWA IMANI YAKE KWA MWENYEZI MUNGU ,,,,,,, TUNAJIFUNDISHA NINI???
Hii nimetumiwa na ndugu yangu kaka CHE JIAH. NA SIKUTAKA KUWA MCHOYO.
Labda dada Rose Muhando amalizie na wimbo huu IMANI.............


JUMAPILI NJEMA KWA WOTE !!!!!!!!!!!!!

9 comments:

  1. Tunajifunza imani.kaka s

    ReplyDelete
  2. Ama kweli haya yanatokea basi Imani inaweza kuwafanya masikini wengi wakawa matajiri.Lakini mbona wanasema na asiyefanya kazi na asile? iweje Huyo masikini alivyokuwa akishindwa kabisa kuchota hatapesa hizo kwa awamu hadi azimalize kwa kuwa zilikuwa nyingi ?
    Na kushukuru kwa michapo kama hiyo ya Jumapili Njema ambapo sasa Manispaa ya Songea ina amani ya kutosha kutokana na ulinzi shirikishi wa polisi kata na sungusungu kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.Juma pili njema na Dominika ya tatu ya kwa Resma.

    ReplyDelete
  3. Amakweli imani inaweza kuhamisha Milima. Nakutakia Jumapili Njema sana Dada yangu.

    ReplyDelete
  4. stori nzuri lakini imani inajenga na hasa kutokufanya jambo ambalo hulijui mwanzo na mwisho wake

    ReplyDelete
  5. Imani...Kaka Sam Ni kweli kabisa hapa tunajifunza kuwa na imani/Uaminifu /kuaminiana.

    ndugu yangu Christian Sikapandwa..maskini kuwa tajiri ni imani pia na ni kweli asiyefanya kazi na asili...Lakini hii pia ni imani. Nafurahi kuona upo nasi..pia ni furaha kuwa kuna AMANI Songea...

    kaka Festo...Kama una amini imani inaweza kufanya hivyo basi itakuwa hivyo..Jumapili njema nawe pia:-)

    Hahahahah Kadala..nimelipenda jina hili ..kwa hiyo na wewe KADODA?..jumapili njema Kadoda:-)

    Usiye na jina ahsante kwa kuona story tamu....

    B! Umenena ndugu yangu ..Jumapili njema ...

    ReplyDelete
  6. J'2 njema dada na wote hapo nyumbani na wapitao hapa!

    ReplyDelete
  7. Habari zenu nyote nimefurahi kuona kuwa wengi tumelipa tendo la Imani kama ndo msingi wa histori hii hata mimi pia nilijengeka kuwa imani hata wale mitume wake kristu/kristo waliishi kwa imani pia baadae walimtumainia mungu na imani ile ndiyo hii tuliyonayo mpaka leo kuwa kristu alikufa kwaajili yetu na kufa kwake leo nasi tumepona ila kwa kuwa hata kabla ya hapo wapo mitume walipita kwa imani kama vile yule aliyepona kwenye tundu la simba Paula na Sila tumesikia habari zao kwa hiyo tuendane na imani na leo hii ni Krersma tuweni na imani na Amani pia Namalizia mjadala kwa hilo AMANI YA BWANA IWE NASI
    CHE JIAH

    ReplyDelete