Saturday, March 10, 2012

UJUMBE WA LEO:- NI VYEMA KUIJUA SIRI HII!

Huu ndio ukweli, ukitaka kupata furaha ya maisha





1.Sema kweli

2.Furahia maisha na furahisha wengine, Penda kwa dhati bila unafiki na bila masharti

3.Jiamini

4.Chukia kusema uongo

5.Tetea unachokipenda na kukiamini

6.Ukiwa dhaifu wa kukumbwa na mawazo potofu usichukie kumbuka mawazo potofu yameumbiwa na Binadamu

7.Jitahidi kufikiri na kuwaza vyema ili uzidi kujiamini, kujipenda na na kuwapenda wengine. Yote yanawezekana.

Kumbuka usemi huu “ukivuliwa nguo chutama. Ukikosea tubu haraka.Wastara huwa haumbuki……………

JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE....NA MNAPENDWA SANA!!

14 comments:

  1. Hapa leo mwalimu hataki kelele......
    Kaamua kutoa semina elekezi.
    Asante sana mwalimu Yasinta Ngonyani.

    ReplyDelete
  2. Nanukuu ''Ukivuliwa nguo Chutama'' kweli kaka Ray Leo mwalimu Ngonyani,mamake Erik kamaliza!!Ahsante kwa kutupa shule dada wa mimi,Uwe na j'mosi njema pamoja na baba na wanangu.

    ReplyDelete
  3. Replies
    1. Dah Kaka Wambura nahuku pia umo! Haya jioni njema ucsahau kesho Kanisani.

      Delete
  4. Asante kwa maneno mazuri mdada.

    ReplyDelete
  5. Asante kwa SHULE!
    Ila katika namba moja MY 2 cents: Katika enzi hizi za mitandao na simu-SEMA KWELI na Fanya kweli na sio Yasemekayo kiukweli MITANDAONI na USO kwa USO ni vitu viwili tofauti! Jumamosi njema!

    ReplyDelete
  6. Asante Dada kwa kutupatia Darasa nakutakia Uck Mwema wewe pamoja na Wadau wote.

    ReplyDelete
  7. hapo umenena mdada lakini huwa nawashangaa watu wengi hawapendi ukweli

    ReplyDelete
  8. Ray..ukiwa darasani hutakiwi kupiga kelele..Ahsante nawe kwa kuona hii ni shule/simina.
    Mija, unaweza kusema kwanini hukubaliani na namba sita?
    Rachel...Unajua unapopata kitu ni vizuri kugawa na wengine na hapo ndo utaona nawe unafaidika..Jumamosi yangu iliishia kubeba mabox..salamu zimefika .

    Kaka Chacha, shukrani!
    Edna, Ahsante nawe kwa kuona ni ujumbe mzuri.

    Mtakatifu Simon!Inawezekana mtandaoni na simu..ndiyo inawezekana ikawa tofauti na utakavyoonana na mtu huyo huyo uso kwa uso au labda yule mtu akawa mwoga kuonana uso kwa uso na mtu ambaye hajaonana naye. Si unajua kushikwa na woga, wasiwasi, na mwisho kushindwa kusema alichotakiwa kusema.

    Festo!Ahsante nawe kwa mchango wako...
    batamwa ..ni kwamba inasemekana ukweli unauma...

    ReplyDelete
  9. Asante Dada Yasinta Endelea kutubariki ilinawe Ubarikiwe zaidi.

    ReplyDelete
  10. Asante Dada Yasinta Endelea kutubariki ilinawe Ubarikiwe zaidi.

    ReplyDelete