Monday, March 12, 2012

JUMATATU HII TUANZA HIVI:- MATUNDA NA VIUNGO!!


Nadhani wote mnajua hapa ni mti wa malimao angalia jinsi yalivyo yaani nashindwa hata kuelezea hapa ni mwaka jana wakati nilipokuwa nyumbani na ni Matema beach kwa rafiki yetu....

....na hapa bila kiungo hiki kachumbali hainogi ni pilipili kichaa ...swali la kizushi hivi ukila hizi unakuwa kichaa kweli? na kwanini zinaitwa pilipili kicha?..


Bado tupo Matema Beach bonge la mkungu wa ndizi mpaka nikatamani nipata na unajua nini? niliupata:-)
..Hapa ni Mdunduwalo mti wa machungwa ...naipenda Afrika yangu kwa kweli matunda na chakula ni kutoka tu nje na kuchukua....JUMATATU NJEMA JAMANI ILA MWENZENU LEO NIMETAMANI kwelikweli nyumbani...




3 comments:

  1. Na kweli hapa Dar sa hizi machungwa kwakwenda mbele,sio lazimakusubiri kulazwa hosptalini, ....ndio hali ngumu, lakini afya ni muhimu sana

    ReplyDelete
  2. Na machungwa ni mazuri kwa vitamini na matamu pia...Ngoja kidogo nimekumbuka kitu hapa nilipokuwa mdogo yaani wakati nasoma darasa la kwanza mpaka la tatu kule Lundo kulikuwa na miti mingi sana ya matunda mablimbali pale shuleni. Na mimi nilikuwa "mwizi" wa malimao nilikuwa nakula kwa siku kumi. Duh enzi zile nakumbuka sana:-)

    ReplyDelete
  3. Pole da'Yasinta!Ooohh narudi Nyumbani eeeee,Ooooohh narudi SONGEA eee!!!Umenikumbusha nami Nyumbani dada yangu, Mmmmhh kwetu ni kuzuri.@hahahaaha Ndugu wa mimi bei sikuhizi inakwendaje? duuhh manafauduuuuu,basi ukute inapita mpaka wiki watu hawali hilo Chungwa,kweli kitu kikiwepo huoni samani yake.

    ReplyDelete