Wednesday, January 25, 2012

MTOTO AVUNJA MLANGO NA KUMBAKA MAMA YAKE MZAZI AKIWA AMELALA

NI JUMATANO NA NI SIKU ILE YA KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO NA LEO NIMEFIKA NYUMBANI RUVUMA NA HABARI HII YA KUSIKITISHA... EBU SOMENI..NIMEKUTANA NAYO Na Mwandishi Wetu, Songea
-------------------------------------------------------------------------------------------------
JESHI la polisi Mkoani Ruvuma linamshikilia Frank Jota (26) mkazi wa kijiji cha Litisha Wilayani Songea kwa tuhuma za kumbaka mama yake mzazi mwenye umri miaka 54 ambaye jina lake limehifadhiwa wakati amelala nyumbani kwake majira ya saa za usiku.
Kamanda wa Polisi Koa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea januari mosi mwaka huu huko katika kijiji cha Litisha kilichopo nje ya mji mdogo wa Peramiho.
Amesema kuwa siku hiyo ya tukio majira ya saa za usiku Jota alikwenda nyumbani kwao ambako alimkuta mama yake mzazi akiwa amelala na baadaye alianza kutafuta namna ya kuingia kwenye nyumba hiyo ambayo mlango wake ulifungwa na komeo kwa ndani.
Amefafanua zaidi kuwa Jota baada ya kuona mlango umefungwa kwa komeo kwa ndani aliamua kuuvunja mlango wa nyumba hiyo kisha aliingia ndani na kwenda moja kwa moja kwenye chumba alicholala mama yake mzazi ambaye jina lake limehifadhiwa.
Amesema kuwa Jota akiwa kwenye chumba ambacho mama yake alikuwa amelala alianza kumtishia kwa kisu alichokuwa ameshika mkononi na baadaye alimkaba shingo na kufanikiwa kumvua nguo ya ndani aliyokuwa amevaa kisha alianza kufanya naye mapenzi.
Amebainisha zaidi kuwa wakati Jota akiendelea kufanya mapenzi na mama yake watu waliokuwa jilani na tukio walisikia kelele za mtu akipiga mayowe na walipofika kwenye eneo hilo la tukio waliingia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta Jota akitokea kwenye chumba alicholala mama yake na baadaye alipowaona watu alijalibu kukimbia lakini majirani hao walifanikiwa kumkamata na kumpeleka kituo kidogo cha polisi cha peramiho.
Hata hivyo kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Kamuhanda ameeleza kuwa polisi baada ya kumuhoji mtuhumiwa amekili kutenda kosa hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu upelelezi utakapo kamilika.
Mwisho.
TUKUTANE JUMATANO IJAYO !!!!!!

5 comments:

  1. Mungu wangu, yale yale...ya uso wa binadamu kukosa haya na tunaeuka kuwa kama kuku

    ReplyDelete
  2. Nadhani Frank ni mgonjwa wa kichwa..ni vyema kama atafanyiwa uchunguzi na kupata matibabu badala ya kuwekwa mbaroni.No question about it,he is insane!

    ReplyDelete
  3. Tukio hili ni miongoni mwa matukio yanyothibitisha kuwa katika dunia yetu sasa tunakabiliwa na changamoto ya mshuko wa maadili kwa kiasi ambacho haijawi kutokea toka kuumbwa kwa Ulimwengu.Hapa ni changamoto kwa wazazi,walezi na wanazuoni mahirini makini katika asasi za kidini.

    ReplyDelete
  4. Kama si bangi, basi ni mshirikina. Au ndo yale mambo ya oedipus?
    Ulaaniwe kijana, haijalishi sababu ilokufanya ufanye hivyo.

    ReplyDelete
  5. Ina maana alikosa wanaojiuza hadi kwenda kubaka mama yake?

    ReplyDelete