Monday, January 9, 2012
HUU NI MLO WANGU WA MCHANA WA LEO KARIBUNI NI SUPU YA KAROTI!!
HAPA NI KAROTI AMBAZO TAYARI ZIMEMENYWA KWA AJILI YA SUPU
Karoti 6-8 kubwa,
Vitunguu 2
Vitunguu swaumu/saumu vipande 3,
Kijiko 1 cha siagi,
Vijiko 2 vya tangawizi iliyokunwa.
Lita 1 ya maji.
Vikombe 2 vya cream,
Vikombe 2 vya maziwa,
Kijiko1 chumvi
Pilipili kidogo/kadili upendavyo.
Jinsi ya kufanya:-
Menya karoti, vitunguu na vitunguu saumu/swaumu. Kisha kata vipande vipande. Yeyusha siagi na kaanga kwa dakika 3-5 kwenye sufuria kubwa. Weka tangawizi , kisha tia maji. Pika supu kwa joto la chini huku umefunika hadi karoti ziwe laini. Weka cream, maziwa na pilipili. Kisha unamixa na blender ya mkono mpaka kuwa laini. unawezawa kuongeza maji au maziwa kama unaona supu ni nzito. KILA LA KHERI NA UPISHI HUU:-)
Asante sana, mi nitakuja kweli...shauri yako, halafu utaanza
ReplyDeletekusema ooh ni kidogo, ha ha ha haaaa!!!!
niko njiani!
ReplyDeletenaweka mafuta ungo wangu, ili niruke salama,usimalize supu. naomba nikute na kamkate kidogo.
ReplyDeletekaka s.
Mmmh recipes poa hizi dada... ngoja nami nitajaribu. Ahsante kwa maarifa na mlo mwema
ReplyDeleteUtamu wa supu, uikute mezani!
ReplyDeleteKaka zangu :- Baraka, Chacha, Sam, Mrope na Chib wote mnakaribishwa sana na wala msiwe na shaka kuwa kweli tutashiba supu ipo tena nyingi tu. Karibuni sana tujumuike maana hapo ndo chakula kinanoga muwapo wengi...pia karibuni wengine wote
ReplyDeleteNilikuwa nikonjiani, na ungo wangu,ila nahisi kunambaya wangu mahali,nimeanguka naungo.naona aibu sitafika jinsi nilivyokuwa nimevaa,sasa sijuwi huyu atakuwa ninani....... au mgoni,msambaa, hapana sijuwi!! haya sikunyingine. kaka s
ReplyDeleteHii sasa ndio tiba ya manjano kimlo au? Keroti zimezidi!! (LOL!!!)
ReplyDeleteKaka Sam, labda uliweka mafuta kidogo:-) ila sio mbaya siku nyingine, lakini siku nyingine jaribu kuchukua usafiri mwingine ili kuepuka huyo mshindani wako...
ReplyDeleteKaka mkubwa Phiri! ndio maana inaitwa supu ya karoti. Ungeonja usingeacha kula kila wiki...
Rafiki asante kwa recipe hii nitajaribu week end hii halafu nitakujulisha kama imenoga hahahah!
ReplyDeletemimi jana nilikuwa nipo kwenye miahangiko jumapili nitainywa tuu kwa raha zangu
ReplyDeletetazama naja upesi
ReplyDeleteUkarimu wa kingoni tumeukubali na tunakuja kwenye mlo huo ila msosi wenyewe ni kiduchu na ubahili.
ReplyDeleteRafiki wangu wa hiari! yaani hutajigamba na nasubiri kwa hamu kunijulisha ilikuwaje:-)
ReplyDeletekaka ISSACK CHE JIAH! nafurahi kusikia nijulishe baada ya kuinywa:-)
Kamala! mbona unachelewa upo wapi??? karibu sanaaaaaaaaaaaaa
Kaka Ray! Ahsante sana kwa niaba ya wangoni wote. Na wala usiwe na shaka kuna lisufuria lizima kwa hiyo hakuna ubahili hapa.KARIBUNI WOOOOTE
Maji ya kisima changu hayanyweki
ReplyDelete