Monday, January 9, 2012

HABARI ILIYONISIKITISHA...MICHEZO NI YA WATOTO AU WAZAZI?

Jana jini nikiwa nasikiliza taarifa ya habari. Kukawa na habari ya michezo ya watoto. Ni mchezo wa innebandy/floorball, mtoto huyo mwenye miaka 10 jina halikutajwa baada ya mchezo timu yake ilishindwa. Na hapo baba yake mzazi alikasirika, na kumwacha mtoto huyo nje akiwa na jezi tu na wakati nje kulikuwa na baridi. Baada ya muda mzazi mwingine alikuwa akipita akamwona yule mtoto akamchukua na kumpeleka kwao. Usiku wote nikawa nafikiria na kujiuliza hivi hii michezo ni kwa ajili ya watoto au wazazi?

2 comments:

  1. Edna yaani nimepatwa na uchungu si mchezo fikiria na baridi hii kuwacha mtoto na vinguo hivyo..wazazi wengine wanataka watoto wafanya kitu kwa niaba yao kwa vile wao hawakufanikisha basi ndo wanafanya hivyo..unyanyasaji tu.

    ReplyDelete