Tuesday, January 10, 2012

LEO TUANGALIE VITENDAWILI VYA KISWAHILI:- KITENDAWILI…..

1. Haukamatika wala haushikiki.........
2. Anataga huku akitambaa...................
3. Ninapompiga mwanangu watu hucheza...................
4. Ubwabwa wa mwana mtamu........................
5. Kuku wangu katagia mayai mibani.................

38 comments:

  1. Vitendawili vigumu kuliko mawe!Hapa nimeshindwa nami nakupa mji nenda Songea.

    ReplyDelete
  2. Nimekipenda kitendawili: "Ninapompiga mwanangu watu hucheza..................."

    Sijui maana ya kitendawili.

    Nafurahia lakini ukweli ndani yake kwamba labda kila unapompiga mwanao maadui zako hufurahia ujinga wako.

    Ukweli ni kwamba ziko namna nyingi za kumlea mwanao kwa nidhamu bila kumpiga.

    ReplyDelete
  3. duh....nimepita kapa maana nikitoa majibu watu wanaweza kuvunjika mbavu...sasa sijui utawalipia gharama za kwenda huko India!!!

    ReplyDelete
  4. Hahhahahahhaa kaka Manyanya umeniacha hoiiiiii,jibu NGOMAAAA, Nipe thawadi dada Yasinta!!!!!Mbarikiwe wooote!

    ReplyDelete
  5. Majibu- 1 jibulake ni mwanga.
    - 2 ushanga
    - 3 ngoma
    -4 matandu/ukoko
    -5 nanasi
    kaka s

    ReplyDelete
  6. Nadhani kuna haja ya kukumbushana zaidi, Yasinta viongeze..

    Kaka Manyanya kula tano kwa tafsiri...

    Kaka Sam duh! Yaani umezipatia zote!!

    ReplyDelete
  7. Wapendwa ndugu zanguni kwa kweli inabidi tukumbushane daima maana naona watu wameanza kusahau ...ila Dada Rachel na kaka Sam mmepata hapo kwenye jawabu la Ngoma na kaka Sam hapo kwenye jawabu la Nanasi ...jaribuni tena mshindi zawadi nono imeandaliwa:-)

    ReplyDelete
  8. Naona ni afadhali nitoe majibu au je kuna mtu anataka kujaribu? Maana naona kama vitendewili vilikuwa vigumu kweli au?

    ReplyDelete
  9. Haya majibu yake ni haya:-
    1. Moshi
    2. Mboga
    3. Ngoma
    4. sungizi
    5. Nanasi.
    Nadhani siku nyingine mtaweza tu labda nifanye hii kila wiki kuchemsha bongo kiduchu:-)

    ReplyDelete
  10. 1. Moshi
    2. Boga
    3. Ngoma
    4. Usingizi
    5. Nanasi

    ReplyDelete
  11. Mwanangu akiwa na wenzake hatambuliki

    ReplyDelete
  12. Naomba mnisaidie hiki kitendawili Maiti anasema lakini walombeba wako kimya

    ReplyDelete
  13. Hii leo imenisaidia mtoto wangu wa primary school kupata majawabu ya vitendawili amepatiwa Kama kazi ya nyumbani....asanteni.

    ReplyDelete
  14. Nina mwanangu ukimpa chakula Amalia ukimnyima halii

    ReplyDelete
  15. kitendawili isemayo ubwabwa wa mwana ni mtamu

    sijui jibu lake

    ReplyDelete
  16. Kitendawili ukiona njigi utathani njege na ukiona njege utathani njigi

    ReplyDelete
  17. Nina mwanangu nikimpa chakula analia nikimnyima chakula halii jibu nini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naomba jibu la kitendawili hiki nina mwanangu nikimpa chakula angalia nikimnyima chakula halii

      Delete
  18. Jibu lake sikujui naomba nipewe jibu

    ReplyDelete
  19. Nisaidie vitendawili hivi1, hesabu yake haina faida
    2, maji ya kisima changu hayanyweki

    ReplyDelete
  20. Nina swali, sijui kitendawili ya kurunzi

    ReplyDelete
  21. Ukimgusa mwanangu mimi hucheka

    ReplyDelete
  22. Nina mtoto wangu nikimpa chakula analia

    ReplyDelete
  23. Nisaidien ich kitendawili maji ya kisima changu hayanyweki jibu lake

    ReplyDelete
  24. Nikimpiga mwanangu nalia mwenyewe jibu lake nn jamani

    ReplyDelete
  25. Nikimpiga mwanangu naliq mwenyewe jibu Lake ni kitunguu

    ReplyDelete