Friday, December 2, 2011

TUWE PAMOJA NA KAKA Addson Noel Omari ( Mfalme Mrope ) KWA MAOMBI YA MSIBA WA MAMA MZAZI HUKO NYUMBANI TANZANIA!!

Kaka Mrope pole sana kwa msiba wa mama yetu mzazi kwani naamini mama yako ni mama yetu.Katika pita pita zangu nimekutana na habari hii ya kusikitisha.
-----------------------------------------------------------------------------------------------
TAARIFA YA MZIBA
Napenda kuwataarifu ndugu zangu na marafiki popote mlipo kuwa nimepatwa na msiba wa mama yangu mzazi Shamsa binti Hassan aliyefariki huko nyumbani Tanzania leo tarehe 2/12/2012. Habari za kisomo na dua zitawajia baadae. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA...Kwa pole napatikana 301 222 7739.... nahitaji maombi yenu.Wenu, Addson Noel Omari ( Mfalme Mrope ) http://tustaarabike.blogspot.com/

7 comments:

  1. Pamoja kaka Mrope Mungu awatie nguvu katika wakati huu Mgumu.

    ReplyDelete
  2. Pole sana, Bw. Omari!

    Mama yako mzazi ni mtu mwema sana...hata huko aliko anaendelea na uwema wake... kwani ametukumbusha leo sisi sote ni wasafiri tu katika dunia hii!

    Mungu amlaze pema peponi!

    ReplyDelete
  3. Pole sana Ndugu Mrope. Tuko pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu. Naelewa uzito wake, kwani nami nilishafiwa na baba zamani kidogo, na halafu mama miaka michache iliyopita. Pole pole utazoea hali hii, ingawa kusahau haitawezekana. Mungu akupe wewe, ndugu, jamaa, na marafiki nguvu ya kuhimili shida hii, na amweke mama yetu mahala pema Peponi. Amina.

    ReplyDelete
  4. Pole che kaka, innah illah wa innah lillah rajuun.

    ReplyDelete
  5. RIP mama yetu.

    pole mfalme. uwe na uvumilivu

    ReplyDelete
  6. Nami naungana nanyi kutoa pole kwa kaka Addeson kwa kupata msiba wa
    kufiwa na mama mzazi nampa pole hayo yote mipango wa mungu pia napenda
    kutoa pole kwa watanzania wote kwa msiba waliopata kwa kufiwa na mwana
    mziki Mr Ebbo nawapa pole yote tumuachie mungu jmosi njema

    ReplyDelete
  7. Ahsanteni wote kwa kuwa pamoaja na kaka Mrope. Kwa kweli kufiwa na mama ni pigo kubwa sana. Pole kaka.Pamoja daima.

    ReplyDelete