Kaka Sam upo? au bado unataka nivae LOL.......hapo kwenye deshi jaza wewe LOL... mdada huyu ni mpezi sana wa sketi ndefu. Sketi ya kitenge hii imeshonwa Songea, top nyeusi imenunuliwa Vila, blauzi kijana /maji ya bahari imenunuliwa H&M. Na nyuma yake nadhani mnaona baiskeli nyekundu hiyo ndiyo inayomfikisha kila aendako...ni usafiri wa haraka sana...
Hapa pia yupo kakaa chini na sketi yake imetanda kama gauni la bibi harusi... LOL.
Swali je? unafikiri ni mpiga picha ni mmoja au ni tofauti? kama ni tofauti hiyo picha ya kwanza nani kapiga na hii ya pili nani kapiga?
JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE NA KUMBUKENI MNAPENDWA SANA!!!
Ndiyo, nipo nipo nipo kabisa jeuri ya chama!!? hapana jeuri ya picha. kwanza kabisa umependeza sana.hapo ulivyo vaa umenikumbusha,jinsi waalimu walivyokuwa wana vaa zamani kwa nidhamu ya hali ya juu na heshima juu.yaani hapo Da yasinta nikupatie na kakiboko/fimbo pembeni mknoni,nimekupata yani bonge ya mwlimu,sijuwi kwa nini nimepata picha mwalimu wa shule ya msingi. ambaye yuko makini na anafuatilia kilakitu hasa usafi wa nguo kwa watoto wa shule,kamahujanyoosha shati/sketi hapo lazima upate bakora.nguo hizi zimekupa husika ,yamdada makini,mwalimu,anae jiheshimu,ila upepo ukipeperusha sketi yako kwa bahati mbaya na ikaonekana sehemu kidogo ya mguu lazima samaahani ikutoke. haya jumamosi njema na wewe,lakini huyo mpiga picha yawezekana si mmoja ila ngoja nitangalia tena. kaka S.
ReplyDeleteUmependeza sana,kweli mwanamitindo kutoka SONGEA namfahamu anaitwa Yasinta Ngonyani.....lol!
ReplyDeletePicha ya kwanza kapiga Erick na picha ya pili kapinga Camila.xx
Picha ya kwanza kapiga Shemeji na ya2 kapiga Erik.
ReplyDeleteYaani da'Yasinta hata ukivaa gunia utatoka tuu dada yangu, kupendeza si kuvaa vichupi tuu,@ kaka Sammmmmmm hahahaha yaani mguu ukionekana ataomba msamaha, kaka s unavituko sana ngoja kaka Mmoja akija hapa, Sijui kalala au anakunya hiyo supu yenu, mwamfudenge Furani, nani anamjua?.
Wapendwa kama umeguswa na swala la emu-3 tuwasiliane hata kwa email.@ Da'Yasinta kaka Manyanya na mimi tumejaribu kuzungumzia na kuona itakuwaje, unaweza kuona na kuongezea mchango wako .Kwani mpaka sasa tupo 3, ni da'Rachel,da'Yasinta na kaka Manyanya.
Yaliyosemwa yamesikika,yaliyosikika yameeleweka na yaliyoeleweka yamehifadhiwa.
ReplyDeleteKaka S kanisikitisha sana kwa kukubaliana na vazi hili!
ReplyDeleteMie bado nasubiri PENSI a.ka. Bukta hapa!:-(
Kaka S kwani hujui wengine tunataka kuona paja?:-)
umependeza sana mdada,kama kasichana kamiaka 15 vile...nimependa mpangilio wa rangi pia.
ReplyDeleteSimon,wala usiwe na wasiwasi, nilikuwa naitikia wito wa dada Yasinta na vazi lake la leo. sasa mwana mitindo mimi,kwa nguo hiyo hiyo ningefanya yafuatayo.1 ninge mrudishia Yasinta helayake.2 sketi nige iwekea mipasuo miwili ya pembeni, mpasuo unge kuwa kupita mgoti kufika kwenye mapja(samhani lakini) 3 isingekuwa pana ,ningeibana, kiasi ili iweze kuonyesha umbo lako la asili.4 hipsi lazima zionekane. upande wa blauzi 1. ninge ichoma moto kbisa.2 ningekutengenezea blauzi mikono mifupi,ambayo kwa mbali imekaa kama kijsti. sasa hebu pata picha utakuwa mchicha kinoma.ila ombi la pensi a.k.a bukta liko pale pale. kaka s
ReplyDeleteKaka S sasa unaongea!
ReplyDeleteha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Mwehhh sasa mbona siri umetoka? unafikiri kabisa hizo ni nguo za kuvaa mwana wa Ngonyani kaka Sam au ni ndoto yako tu:-)
ReplyDelete@Kapulya:Unambishia Kaka S?
ReplyDeleteIla mtoto mzuri weye asante kwa kutovaa miwani jamani!
Naanza kuaminia kuwa,....MWANAMKE JICHO mwenzio kwa kukodolea picha zako.
Geuka basi tuone ramani za kwa upande wa nyuma basi DADA!
.....ila mwanamke weye kunasiri watu hawastukii iliyo kwenye jicho! Umejistuki eeh baada ya mimi kusema eeeh!?
Hapana Simon simbishii kaka S. Najua singevaa hilo vazi alilolisimulia hapo.
ReplyDeleteKugeuka siwezi nimeganda...
nanukuu ".....ila mwanamke weye kunasiri watu hawastukii iliyo kwenye jicho! Umejistuki eeh baada ya mimi kusema eeeh!?" mwisho wa kunukuu...HAPANA SIJASTUKIA je unaweza kusema au kuninongóneza?
@Yasinta: una bonge la jicho malaika wee!Kimahaba kumbuka kulitumia kwa kuwa linaweza kuamsha jambo au tu kusisimua mshawasha!:-(
ReplyDeleteHahahahahaaaa! Simon unavijimambo weye?....nimecheka sana!
ReplyDeleteAhsanteni sana wote kwa kuwa nami jumamosi hii yaani ni raha sana kuwa na marafiki kama ninyi...Picha ya kwanza imepigwa na mume wangu na ya pili na binti yangu.
ReplyDeleteMPIGAPICHA ni MWENYE CHEO KIMOJA....Cha MPIGA PICHA
ReplyDeleteHahahahahaaaa. Mzima wewe?
Mzee wa Changamoto karibu sana maana umekuwa kama mwana mpotevu...Mie mzima kakangu..."MPIGAPICHA ni MWENYE CHEO KIMOJA....Cha MPIGA PICHA" nimependa msemo huu
ReplyDeleteKwikwikwikwikwikwikwikwi...jamani mbavu zangu miye..." ..eti kaka S kanisikitisha sana kukubaliana na vazi hili..
ReplyDeleteJamani watu mna mambo!! Ila da Yasinta umependeza sana na pia usisahau kulitumia hilo jicho kama ulivyoshauriwa...
Baraka kwenu..
mhhhh nimeliangalia hilo jicho mhhhh............napita tu jamani
ReplyDelete