Kutokana na maoni ya ndugu zangu Mangi na kaka Simon Kitururu ambayo yanatoka katika picha hizi nimeona niweke hii picha labda itasaidia. Maoni yenye yalisema hivi:Ndugu Mangi anasema "Akina msitudanganye kabisa!Tuonyesheni kitu kipya na kamili kwa kuvaa mavazi ya wanawake katika picha kamili kuanzia juu kwenda chini mkionyesha uwakilishi wa kitanzania." Na kaka Simon naye anasema "Ghafla naamia upande wa mtani wangu MANGI ,...... nahisi kuna kitu hamjatuonyesha. Na neno la MANGI liheshimiwe nanyi. Amen.
JUMAMOSI NJEMA WAPENDWA!!!!!
Wadau mpo hapo.Yasinta katoka kivingine kabisa tena na miguu ya bata sijui kasahau ndala/viatu.Lakini raha ya lizombe ucheze peku.Hapo,hapo ni lizombe mpaka bombambili kwenye nyumba yenye madirishi na pale nje utakutana na kajogoo keusi kadogo kanawika kokoliki!Hapo umefiki!
ReplyDeleteNafurahi kuona mwanamke wa kitanzania katika mavazi ya kiheshima ya Kitanzania. Hebu endelea kuwafundisha wadada wa hapa bongo namna ya kuvaa maana hivi sasa inatisha .. kila wanachoona kwenye runinga wamedaka.. hizo model jeans, legging jeans, vipedo .. hadi inatisha! na jamii inakaa kimya kabisa .. hamna anayefungua mdomo .. hivi sasa nguo za kulalia na zile za kuvaa ndani mnaita skin tight zinavaliwa na kutokea... yani mmmh! jasho linanitoka .. kama ni kutegani kumepitiliza! tunashindwa kutegeka tunaishia kupata kichefu chefu .. hata wakati mwingine inafikakia unamchenga mtu unayemfahamu!
ReplyDeletetabasamu lako bibi...kwa raha zako
ReplyDeletehalafu pozi hilo kama la Bikira Maria mkingiwa Dhambia ya asili a.k.a Maria Imakulata...lol!
sifa ya vitenge,uwe na bodi,tako,wowo ,nk maranyingi wamama wenye miili ya wasitani hupendeza sana wakivaa vitenge. haya dada wawa watu umetoka vizuri na vitenge. walio toa ombi watakuwa wameridhika. jumamosi njema.kaka s
ReplyDeleteMambo ndio haya sasa!Ila ngojea nifikirie kidogo,.. isijekuwa ushantia majaribuni kwa dhambi ya kutokwa udenda!:-(
ReplyDeleteJumamosi njema Mdada!
haahaha haya kaka Njau na kaka Simon nami nimeshajibu.
ReplyDelete@Rachel :Nimeona na umependeza kweli!
ReplyDeleteUmependeza kweli kweli mwanakwetu.
ReplyDeleteWape, Dada! Wape, tu! Wasithubutu kusema tena! Safi saba!
ReplyDeleteMlongo upendizi sana, nimelipenda sana hili vazi na Mama Afrika linakubali sana dada yangu.
ReplyDeleteUmependeza mdada, umekumbusha hako kamshono ni ka miaka mingi lkn kama kawaida ya kitenge kila ukivaa mshono hauchushi
ReplyDeleteNachukua nafasi hii na kuwapa Shukrani wote.Pamoja daima:-) Rachel nimekuona pia mdada umependeza nawe mwenzangu.
ReplyDeleteAsanteni wadau na asante Yasinta kwa kukidhi kiu ya wadau wako.Yale yote mema yaandikwe kwenye mawe ili yasifutike na yale mabaya yaandikwe mchangani ili upepo uyachukue.
ReplyDeletehivi dhambi ya asili ni ipi?nijuze walimwengu kwauelewa wangu si alisema nendeni mkaijaze dunia? au...... batamwa
ReplyDelete