Mimi leo nataka tutumie maazimisho ya miaka 50 ya uhuru wa nchi yetu kujadili swali lifuatalo :-
Baba wa Taifa hayati mwalimu Nyerere, aliamini na kuja na falsafa ya maendeleo iliyokuwa inasema ili tuendelee kama taifa tunahitaji mambo muhimu manne(4) watu, ardhi, siasa safi na Uongozi bora. Lakini pia akasisitiza ili hayo maendeleo yafikiwe tunahitaji kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Kwa zama hii tuliyonayo pamoja na kuwa na hivyo vitu vinne kumeongezeka suala la UFAHAMU NA MAARIFA.
Swali katika ngazi ya familia na koo zetu za Kitanzania tunahitaji mambo gani ya msingi ili kuendelea.
Maana kwa hali ilivyo hasa kwa sisi watanzania tumebobea katika kulaumu, kulalamika na kulaani wakati hata siku moja kulaani na kulalamika hakujawahi kuwa suluhu ya kile unacholalamikia, kulaani na kulaumu.
UJUMBE HUU:- Nimetumiwa na kaka yangu pia msomaji wa MAISHA NA MAFANIKIO SALEHE MSANDA AMBAYE NI MKAZI WA NJOMBE. TUJADALI PAMOJA....
Kweli kabisa lawama zimezidi sana, na kulaani vitu badala ya kutafuta solution ya tatizo, utakuta watu wamekaa kikundi kwa muda mrefu wanaongelea siasa,ubaya wa serikali, maisha yalivyo magumu kila kitu ni kulaaani serikali, wanapoteza muda mwingi sana kuongelea mambo ambayo hayana msingi wala mtatuzi zaidi kuotkana na maisha magumu watu hulaumu na kumaliza stress zao kwa njia ya lawama .Ila kimsingi hata serikali iwe na pesa kiasi gani haiwezi fanya mtu akawa anaishi maisha ya juu muhimu ni sisi wenyewe kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka kwa njia yeyote ile ili kuinua familia zetu, maendeleo huanzia kwenye familia maana familia ni taifa ambalo ni rasilimali ya serikali. lawama na kulaani tuache tufanye kazi serikali haiwezi mpa pesa kila mwananchi ni ngumu sana swala la ajira ni duniani kote shida si marekani wala wapi. TUBADILIKE JAMANI
ReplyDeleteBEN/SOUTH KOREA