Habari jamani!
Leo nimeona si vibaya kama nikiongelea jambo hili, katika maisha kuna kupenda/kumpenda mtu na kuna kuchukia /kumchukia mtu. Yaani kumtendea mtu mema na kumtendea mabaya. Hii huwa inakuwa ni ngumu sana kwa sisi binadamu kusema /kutamka hili neno SAMAHANI/NISAMEHE. Basi mimi leo nimeona sina budi kuomba msamaha kwa yeyote yule ambaye nimemkosea/nilimkosea, nimemkwanza/nilimkwaza yule ambaye nilimwahidi jambo na sijaweza kulitimiza. Kwani naamini mimi pia ni binadamu na ni rahisi kukosa/kukosea. NISAMEHENI NDUGU ZANGUNI!
Habu TUENDELEE na WIMBO huu WA kaka BONNY mwaitege NISAMEHE....
TUPO PAMOJA DAIMA TUSISAHAU HILI NA WOTE MNAPENDWA!!!!IJUMAA NJEMA:-)
Ijumaa njema kwako pia Yasinta!
ReplyDeleteNa wewe pia, kama tumekukosea twaomba utusamahehe!
ReplyDeleteAhsante Simon!
ReplyDeleteem3! Usiwe na shaka kwani mtu aombapo msamaha basi ni LAZIMA atakuwa amewasamehe walo walomkosea...Ahsante!!
Ni miezi kadhaa na masiku mengi tu sijaonekana katika tasnia hii ya blog.
ReplyDeleteleo nimerejea tena. Nawaahidi mambo mazuri, karibuni kibaraza cha Tegelezeni. Tupo Pamoja.