Friday, September 2, 2011

CHAKULA NILICHOANDAA na KULA JIONI LEO/IJUMAA HII KARIBUNI TUJUMUIKE!!

Kwenye sahani hii ni :- Wali (mchele wa kutoka nyumbani tena kule kunakosemekana ni mchele bora kuliko yote hasa Tanzania sio kwingine tena ni KYELA).... mshikaki wa kuku na kachumbali ..kitelemshio ni maji lakini usiogope kuna vinyaji vingine kwa anayependelea. KARIBUNI TUJUMUIKE ..JIONI NJEMA...

12 comments:

  1. TUNA SHUKURU KUJUMUIKA KATIKA MLO HUO ULIYO ANDAA,

    ReplyDelete
  2. Naona hakuna pilipili katika kachumbali,vipi ni wali nazi ama?Napenda sana mlo huo ulioandaa, asante, ubarikiwe

    ReplyDelete
  3. ASANTE DADA YASTANTA LAKINI MIMI NAONA INGEKUWA BORA KAMA NI UGALI MAANA KAMA NI WALI UTAKULA NA KIJIKO AU MKONO RAHA YA UGALI NA MSHIKAKI ULE NA MKONO AU VIPI BWANAE

    ReplyDelete
  4. ASANTE DADA YASTANTA LAKINI MIMI NAONA INGEKUWA BORA KAMA NI UGALI MAANA KAMA NI WALI UTAKULA NA KIJIKO AU MKONO RAHA YA UGALI NA MSHIKAKI ULE NA MKONO AU VIPI BWANAE

    ReplyDelete
  5. Kaka Chib! kwanini iwe visa?

    Christian! kwanza nasema karibu tena maana ulipotea kidogo. Karibu sana.

    Usiye na jina wa 2/9 10:40 PM ! usiwe na wasiwasi pilipili ipo tena pilipili mbuzi.

    usiye na jina wa 12:39 AM! Wala usipate taabu ugali utakuwepo kwa ajili yako...Ni kweli ugali ni bora kwa mshikaki:-)

    Kamala! mbona mh? vipi?

    ReplyDelete
  6. KUENDAKO HISANI HAKURUDI NUKSANI BALI SHUKRANI.UKARIMU WAKO WA KINGONI
    UNATHAMINIWA SANA.ASANTE SANA!

    ReplyDelete
  7. Mmmmh! Wali na KACHUMBARI mpaka MSHIKAKI havitoshi kwetu kijiweni ! Huo si matonge mawili rijali akifinyanga mlo?:-(

    Asante lakini!
    Ila funga jiko kwa kuwa tunaweza kwenda huko ukilala.... kwa kuwa lazima ukoko na makombo yapo huko!:-(

    ReplyDelete
  8. hahahaha! Simon huo wali ni mwingi sana... halafu umenifanya mpaka nicheke kidogo eti nifunge mlango...Haya Mtakatifu!!!!

    ReplyDelete
  9. mie hivyo vinywaji vingine tu, ndio nataka!

    ReplyDelete
  10. Ha ha hahaaa! watu weweeee, kaka John wala usipate tanu kuna kila kinywaji hadi ULANZI:-)

    ReplyDelete