Kwanza tunapenda kuwasalimu sana Ndugu walimu na wanafunzi na wadau wote mliopo popote nchini Tanzania na Duniani kwa ujumla, Kwa heshima na Taadhima tunapenda kuwatambukisha kwenu Blog mpya kabisa inayo kwenda kwa jina la MATUKIO NA WANAVYUO ambapo lengo kubwa ni kuwakutanisha wanavyuo wote Nchi nzima na kubadilishana mawazo pia kujua nini kinaendelea kila wakati kupitia mtandao huu, Hatuna mengi sana ya kuandika hapa kwa maana mtandao wenu unajieleza vizuri kabisa, pia mtandao huu ni wanavyuo wote waliopo vyuoni sasa na wale walio maliza pia ni wa watanzania wote kwa ujumla kwa maana kuna mambo yanayo wahusu na muhimu. Tunawaomba mpitie kila kona ya mtandao huu na kutoa maoni kama yapo nini kiongezwe ama kuboreshwa zaidi, Tunawakumbusha tena mtandao huu ni wako. sisi tunaongoza tuu kwa mawasiliano zaidi tutumie Barua pepe kupitia
( twanavyuo@live.com)tunatanguliza shukrani zetu pia atakae pata taarifa hii ampe na mwenzake
Asanteni sana.
Matukio na wanavyuo Crew
KUTEMBELEA MTANDAO HUU BOFYA HAPA http://tzwanavyuo.blogspot.com/
Sijui kama ni matatizo ya kampyuta yangu, Kapulya, lakini sikuweza hata baada ya majaribio mawili kufika katika mtandao huo ulietangaza hapo juu. Nakuomba nawe uchunguze kidogo; maana yake mtandao wa aina hiyo ni mzuri sana. Lakini ni uzuru wa hewa tu kama utakufa kabla ya kuzaliwa... pole lakini, na pia samahani kama nakosea!!!!
ReplyDeleteVilevile nitumie upya hiyo link kama blog hiyo iko hai: manyanyaphiri@gmail.com