Na hapa inakuja baadhi ya misemo ambayo nimeipata kwenye kanga ambazo ninazo:-
1. Yote fanyeni maskini mkumbukeni.
2. Ahsante mama Mungu akupe kheri Daima.
3. Usigeuze sikio kusikiliza ya wenzio.
4. Upendo na Amani ametujalia Mungu.
5. Nakuridhiya kwa kila hali ujuwe nakupenda kweli.
6. Ya mitaani uyajue wewe yako ayajue nani?
7. Furaha yako ni faida kwangu.
8. Nilijua kiroho kitawauma.
9. Ukinienzi ni wako ukinidharau kazi kwako.
10. Tuishi milele tusifanye kelele.
Hivi kwanini kunakluwa na misemo kama hii kwenye kanga? Haiwezi kuwa kanga tu bila maneno/misemo au methali?
Nyingi huwa zimejaa vijembe.
ReplyDeleteNakubaliana na wewe kaka Chib. Lakini kwanini iwe hivyo??
ReplyDeleteUnajua Yasinta khanga ni maalum kwa kupeleka ujumbe kwa jamii ila sasa inategemea ni ujumbe gani maana kuna ile kumtakia mtu baraka njema, pole, furaha ama pia ujumbe wa mahaba, vijembe nk. Kama si mpenzi wa maneno basi kuna vitenge hivi havina maneno na bado utavaa nakupendeza kwa muonekano kama wa khanga.
ReplyDeleteRafiki Kay! umesema kweli lakini huu ujumbe kwa nini usiuwakilishe moja kwa moja kwa muhusika? Kuhusu vitenge siku hizi naona hata hivyo navyo vimeanza kuandikwa.... Ahsante kwa ushauri rafiki....
ReplyDeletenadhani hapa wakina mama mtatusaidia zaidi
ReplyDeleteHii ni inapekeleka ujumbe kwa mlengwa sasa hayo ya vijembe inategemea na mtu mwenyewe,kama hutaki kuna za maneno mazuri nyingi tuu,kwanini usimwambie mojakwamoja mtu?Nikama unavyomtumia kadi ya pole,asante,nakupenda .......sasa kuna kanga za maneno ya kufariji na shukrani pia zamani zilikuwepo ambazo hazina majina mama yangu alikuwa nazo,kwa sasa sinauhakika.
ReplyDeleteNimejaribu kuwaza dada.
Da Yasinta: na wewe unampiga nani vijembe huko?...lol!
ReplyDeleteIngawaje misemo mingine huwa ni kupigana vijembe hasa kwa watu wenye chuki, lakini misemo mingine huwa inaliwaza
ReplyDeletei mean unapoivaa wewe mvaaji unajikuta lile neno linakufariji. na una pendelea khanga fulani sio kwa uzuri wa rangi lakini ni kwa ule msemo ulioandikwa
eg: "MPAJI NI MUNGU". "TUNDA LA ROHO NI UPENDO" etc.
Uzuri wa khanga maneno yake somo kasema mzaramo si mimi mtoto wa kichagga kutoka Mamba Mkolowony kule Moshi vijijini
ReplyDeleteUzuri wa khanga maneno yake somo kasema mzaramo si mimi mtoto wa kichagga kutoka Mamba Mkolowony kule Moshi vijijini
ReplyDeletevimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg
ReplyDelete