Tuesday, April 26, 2011

KWA NINI IWE NI WANAUME TU WANAONUNUA MKUYATI?

Jamaa akinunua Mkuyati

Kuna wakati wanaume wanaweza kuwa na ugumu wa kujua kwamba wake au wapenzi wao hawaridhiki kimapenzi. Hiyo inatokana na uwelewa mdogo waliokuwa nao wanaume juu ya tofauti kubwa iliyopo kati ya wanawake na wanaume kuhusiana swala zima la hisia za kimapenzi.
Wanawake wana matarajio makubwa sana katika kila eneo linalohusu maisha yao, lakini linapokuja swala la tendo la ndoa mambo ni tofauti sana. Kwa kawaida wanawake wengi ambao hawaridhishwi na tendo la ndoa kwenye uhusiano wao huwa wanafanya siri.

Bila kujali kama tatizo liko kwao au kwa waume zao, wanawake hufanya siri kutoridhika kwao kimapenzi, na huweka siri kwa waume zao na hata kwa madaktari. Na ndio maana sishangai kuona kwamba wateja wa wauza dawa zinazohusiana na kuongeza hamu ya tendo la ndoa yaani Mkuyati ni wanaume.

Nilipokuwa nyumbani Tanzania, jijini Dar Es Salaamu nilishangaa sana kuona katika magazeti maarufu ya Udaku, {Tabloids} matangazo mengi ya biashara yanayotawala katika magazeti hayo ni ya kuuza dawa za kuongeza nguvu za kiume au hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume na nyingine zilikuwa ni za kuongeza ukubwa wa maumbile ya kiume, dawa kama Mkuyati, Mzakaru, Super Shaft, Kifaru, Sekwa na nyingine chungu nzima ni maarufu sana jijini Dar Es Salaam.

Sio kwamba wanawake hawana matatizo ya tendo la ndoa, la hasha. Wanawake wanayo matatizo hayo ya tendo la ndoa lakini kwao hiyo siyo agenda, yaani si kitu cha kuwaumiza sana kichwa. Lakini kwa wanaume ni tofauti sana, wanapokuwa na tatizo la kukosa ufanisi katika tendo la ndoa huo utakuwa ni mgogoro mkubwa sana, kwani kwao hili ni jambo linalopewa kipaumbele kuliko mambo yote.

Kwa wanaume kukimbilia hospitalini au kwa mganga wa jadi na kusema “nina tatizo kubwa” ni jambo la kawaida kabisa…. Lakini wanawake hawafanyi hivyo, Badala ya kulifanya tatizo hili ni mgogoro halisi, huwekwa chini kabisa kwenye orodha ya matatizo yao, huwekwa kiporo na litashughulikiwa kwa wakati atakapojisikia kufanya hivyo kwa wakati wake.

Wanawake wanaweza kwenda kuomba ushauri au kuwasimulia mashoga zao, kuhusu matatizo ya ndoa. Lakini ni hadi wachokozwe ndipo wanapoweza kusema kwamba maisha yao ya tendo la ndoa na waume zao hayako sawasawa. Hilo halipewi uzito wa juu au naweza pia kusema hufanywa siri.

Wanawake hawaridhishwi na tendo la ndoa kwa sababu mbali mbali. Lakini bila kujali sababu hizo, kwao ni vigumu sana kusema kuhusu kutoridhishwa kwao. Ukiona mwanamke anatangaza sana kuhusu kutoridhishwa kwake na tendo la ndoa, basi ujue huyo na mumewe wako kwenye uhusiano mbaya sana. Kwani atakuwa anatumia maelezo ya kutoridhika kwake kama adhabu ya kumkomoa mumewe kwa kumuaibisha.

Lakini wale walioko kwenye ndoa imara ni vigumu kuwasikia wakilalamika kwamba hawaridhiki na tendo la ndoa. Inawezekana kutoridhika kwake kunatokana na yeye mwenyewe, yaani labda hana hamu au hafiki kileleni kutokana na matatizo mbali mbali yakiwemo ya kisaikolojia au matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango, lakini bado sehemu kubwa wanaume huchangia. Hata hivyo pamoja na sababu hizo, mwanamke hayuko tayari kusema kuhusu kutoridhika kwake.

Kushindwa huko kunatokana na jinsi jamii ilivyomfunga mwanamke, kutoonesha kuhitaji tendo la ndoa. Akionesha kutoridhika na tendo la ndoa huonekana ni Malaya, kwa hiyo hukaa kimya na kuonesha kutojali.

Lakini bila shaka nadhani umefika muda wa wanawake kuwa huru kuhusu tendo la ndoa na kusema hisia zao wazi wazi bila kuogopa jamii itawaonaje, kwani jamii imekandamiza haki yao ya kuzungumzia tendo la ndoa kwa muda mrefu sasa.

Wanaume nao wanapaswa kujua kwamba wanawake hawapendi au hawawezi kuzungumzia kutoridhishwa kwao na tendo la ndoa, hivyo kutosema kwao kusitafsiriwe kuwa ndio wanawaridhisha, ni vyema kutoa ushirikiano kwa wake au wapenzi wao na kutafuta kujua kama wanawaridhisha. Ni jambo la busara kama mwanaume atadadisi kwa upendo na lugha ya upendo na kuonesha kama yuko tayari kutoa ushirikiano pale ambapo mke au mpenzi ataonesha kutoridhishwa na tendo la ndoa.

Mada hii nilikwisha wahi kuiweka hapa kibaraza , nimevutiwa nayo tena nikaona sio vibaya kuirejea ili kujikumbusha. Kama nisemavyo kila wakati kurudia kusoma kitu ndio kujifunza mengi.

18 comments:

  1. Replies
    1. Mtaalamu wa tiba asil na mitishamba toka tanga anatibu ugumba.. Uzazi.. Nguvu za kiume.. Kukuza UUME na kunenepesha uume.. UTI SUGU...KUKUZA hips shape na makalio...anatumia dawa za mitishamba na za KISUNA... Wasiliana nae 0764839091

      Delete
  2. Hahahaha da Yasinta nitarudi ngoja nikalale kidigo!!!!!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kutana na Dr Kalyundu anatibu NGUVU za kiume..ugumba ..uzazi..UTI SUGU..KISUKARI..UKE KUJAA MAJI NA KUWA NA HARUFU CHAFU ...MAPENZ ZINDIKO NA UCHAW ..MPIGIE 0764839091

      Delete
    2. Kutana na Dr Kalyundu anatibu NGUVU za kiume..ugumba ..uzazi..UTI SUGU..KISUKARI..UKE KUJAA MAJI NA KUWA NA HARUFU CHAFU ...MAPENZ ZINDIKO NA UCHAW ..MPIGIE 0764839091

      Delete
  3. Nikichangia hapa najua nitazua mgogoro..........
    Naomba niseme tu kuwa ni kumbukumbu nzuri kuirudia mara kwa mara maana sio wote waliowahi kuisoma mada hii hususana kaka Mkandawile........

    ReplyDelete
  4. Duh, oh, heri mimi sijasema kitu...!

    ReplyDelete
  5. mmmh,kuna ukweli hapa.ila kweli wanawake nao wapige mkuyati tena si tutadandiana huko mitaani??maana kwa hali ilivyo sasa tu inatisha sasa mkiongeza na mkuyati sipati picha.haya sie yetu macho tunangoja.

    ReplyDelete
  6. Si kama nyie Wanamama, ni vigumu sana kwasisi Wanaume kudanganya na 'KUFEIKI' tunaposhindwa katika tendo, wewe Dada Yasinta!


    Rafiki yangu mmoja tena padre hapa bondeni alimpa talaka mke wake na alipoulizwa na hakimu sababu akajibu: "Yeye 'hana ladha'"


    HAKIMU: "Hana ladha kivipi, Padre, mtu ukiwa umekwishazaa naye watoto hadi wanne tayari? Kotekote ulikuwa huoni ladha?"



    PADRE: "Wewe Mheshimiwa Hakimu, unaniuliza nini sasa? Mimba sikitu weee! Mbona mwanamama hushika mimba hata kwa aliembaka tena kwa uchungu?"


    Nimeyasimulia hayo ya padre na hakimu wake kuonyesha (kama itasaidia) kwamba ndoani uvumilivu ndio mkuyati kiboko. Na mara nyingi wewe Mwanamme ukishawoa nakushauri tafadhali sahau kwa yale uliyewaza awali ndio tendo PERFECT!

    ReplyDelete
  7. Dada Yasinta.usihofu dunia tuliopo sasa niya uwazi kiasi kimapenzi,tofauti na ilivyokuwa zamani,wewe ukiwa shahidi.ulivyo pata ujasiri wa kuandika makala hi ni dalilitosha kwa ukombozi wa mwanamke.sasa hivi dada zangu mmepiga shule, mmetembea shemu mbalimbali za dunia,na wengine mna blog zenu,hivyo taratibu kizazi chako cha sasa lazima kita jidili swala kungonishana,na pindi itokeapo kutorithishana nina uhakika,kutatafutwa tiba.sasa hivi dada zangu wa kibongo wanatongoza, na wana kauli juu ya miili yao.sisi wanaume tunajitutumua sana hasa wakati wa kungonishana,bila kukumbuka kuwa jambo hili ni kuwasiliana,kusikiliziana,na pia hata kuulizana maswali,mfano ukimaliza una muuliza mpenzi wako vipi umefurahiya.kaka s

    ReplyDelete
  8. Yasinta unaakili sana yaani IQ yako iko juu na unafanya mambo mkuu sana kwani wewe kila sehemu unaweza. Unaweza kuandika kuhusu ushauri pia mambo mengine yayohusu jamii.

    Ila kwa leo nimegundua kuwa kumbe wewe ni Mwanasaikoloji mkubwa sana katika dunia hii nakufananisha binbwa wa saikolojia duniani ambaye anafahamika kama "Father of Psychology" Freud. Asante sana kw3a kazi nzuri.

    ReplyDelete
  9. ukisha waza namna hiyo uwaze pia 'kwa nini iwe ni wanawake tu wanaonunua limbwata?' teh teh teh teh teh!

    ReplyDelete
  10. @Chacha

    Mkuu Chacha, unamaana kweli kinyume cha mkuyati ni limbwata?

    Asante sana kwa kunikumbusha PHYSICAL SCIENCE yangu: [FOR EVERY ACTION THERE IS A REACTION OF EQUAL ENERGY ALBEIT IN THE OPPOSITE DIRECTION].

    ReplyDelete
  11. chacha

    chacha! you really made my day.

    Du! katu sikuwahi kufikiri kama wewe. akili yako inafanya kazi haraka sana

    ReplyDelete
  12. Kutana na Dr Kalyundu..kutoka tanga mtaalamu wa tiba asil.. Anatibu ugumba ...uzazi....NGUVU za kiume.. KUKUZA na kurefusha uume..MAPENZ.kubana na kuondoa maji ukeni...UTI..ZINDIKO NA UCHAW.MPIGIE SIMU 0764839091

    ReplyDelete
  13. Kutana na Dr Kalyundu..kutoka tanga mtaalamu wa tiba asil.. Anatibu ugumba ...uzazi....NGUVU za kiume.. KUKUZA na kurefusha uume..MAPENZ.kubana na kuondoa maji ukeni...UTI..ZINDIKO NA UCHAW.MPIGIE SIMU 0764839091

    ReplyDelete