Wednesday, March 23, 2011

MSIBA RUHUWIKO:-FAMILIA YA MZEE NGONYANI INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BINTI, DADA,MDOGO,SHANGAZI, MAMA MDOGO PIA SHEMEJI ASIFIWE NGONYANI!!


Asifiwe Ngonyani 26/11/1989-23/3/2011
Jioni hii muda si mrefu nimepigiwa simu kuwa sina mdogo tena. Mdogo wangu mpendwa na wa pekee ametuacha amekata roho jioni hii kama saa tatu kasorobo ya TZ. Mwenyezi Mungu na aipokee roho yake mahali pema peponi AMINA. HAKIKA NI PIGO KUBWA SANA KWA FAMILIA YETU..Habari zaidi nitawaelezeni.....

59 comments:

  1. Pole! Lakini kumbuka wote sisi duniani hapa wasafiri tu.

    Na huyo mdogo wetu alietuwacha hapa duniani leo... itakuwa vigumu kwako kuelewa kwa sasa naamini... LAKINI HUYO KAPANDISHWA CHEO TU... roho zetu lazima kukutana na roho yake siku moja huko tunakokwenda wote bila mmoja wetu kunusurika.

    Poleni!

    ReplyDelete
  2. Poleni sana kwa msiba,mola awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwenu ndugu jamaa na marafiki. Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi.

    ReplyDelete
  3. Ple sana! Mungu awape nguvu ya kukikabili kipindi hiki kigumu. Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina

    ReplyDelete
  4. POLENI SANA DA YASINTA,MAY GOD REST HER IN PEACE.AMEN

    ReplyDelete
  5. Poleni sana. Mwenyezi Mungu awape faraja ana ampe raha ya milele marehemu.

    ReplyDelete
  6. pole sana da Yasinta kwa pigo hili kubwa kwako. Kuna wakati kuna mambo huwa vigumu sana kwa moyo kuyakubali hususani kwa tukio kama hili.

    Ninakuombeeni faraja kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

    Mwenyezi Mungu ametuahidi mitihani, mmoja ya mitihani hiyo ni kufiwa na wapendwa wetu. Mwenye kufaulu ni yule mwenye kusema, hakika sisi sote ni wake na kwake tutarejea. Inna lillah waina lillah rajuun.

    Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake libarikiwe!

    ReplyDelete
  7. Poleni sana wapendwa,kweli ni pigo,mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu,bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.

    ReplyDelete
  8. Pole mno da' Yasinta na familia yote!Hakika ni pigo lakini tunapaswa kukabiliana nalo kwa kufarijiana na kujipa moyo. Bwana ametoa na ametwaa jina lake libarikiwe

    ReplyDelete
  9. Pole sana,Yasinta.nikumshukuru mungu kwani kazi yake haina makosa,wote njia yetu moja,ila muda nasaa ndo mimi nawewe hatujuwi.
    pole sana.
    kaka s

    ReplyDelete
  10. Pole sana Dada Yasinta. Mungu awapeni nguvu ya kuvuka kipindi hiki kigumu, na amweke dada yetu huyu mahala pema Peponi. Amina.

    ReplyDelete
  11. Poleni sana katika wakati huu mgumu, cha muhimu ni kumuombea. Mungu amuweke katika amani, na nuru ya daima imuangaze. Amin.

    ReplyDelete
  12. Poleni sana . huyo ni shetani ndiye anayetuletea kifo.Bwana ndio atawapatia faraja kutoka juu.
    Mungu awenanyi wakati huu Mgumu.

    ReplyDelete
  13. Ni hivi majuzi Jumamosi ya terehe 18/03/2011 nilimtembele4a binti huyu pale maeneo ya Kinondoni Mkwajuni alipokuja na baba yake Mzee Ngionyani walipokuja Clinic kuchunguzwa afya yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa Moyo mwaka jana mwezi wa Februari, niliongea mengi na Mzee Ngonyani pamoja na Asifiwe ambaye leo hii nambiwa hatunaye tena. Mzee Ngonyani alinihakikishia kuwa Asifiwe anaendelea vizuri na ile hali ya kuumwa umwa kama zamani haipo tena.

    Nilimsaili Marehemu Asifiwe maswali kadhaa nikitaka kujiridhisha kama kweli amepona na alinihakikishia kuwa amepona kabisa.

    Nilijikuta nikimwambia kuwa sasa anatakiwa kurudi Shule, akiwa na tabasamu pana usoni mwake alinijibu kuwa yuko tayari kurudi shule na ndipo baba yake akaniomba nimsaidie kumtafutia shule nzuri atakayosoma binti huyu.

    Ninayo mengi ya kusimulia kuhusiana na mazungumzo yangu na Asifiwe lakini naona niishie hapa wakati nikitafakari msiba huu mzito.

    ReplyDelete
  14. pole kwa msiba dada,So sad,may her soul rest in peace

    ReplyDelete
  15. Kila kilicho na mwanzo hakikosi mwisho, sidai kulitukuza maana kalitukuza muweza aliyeumba tupate ila hali ya uasi ikasababisha tukose japo tuna rehema.

    Yote hayo ni matokeo ya uasi pale Eden maana yake ndio hiyo kwamba KUFA TUTAKUFA HAKIKA.

    Kutokana na tahadhari iliyotolewa kwa ADAM na HAWA ya kutokula mti wa mema na mabaya hasa matunda yake. Maumivu yote tunayoyapata na huzuni zinazotusonga hata uchungu unaotuandama kila hali ina mwisho wake.

    Ipo siku tutakutana na hauyo mpendwa ama katika ufufuo wa uzima au ufufuo wa mauti, kila mmoja ana zamu yake na kiukweli MUNGU NAYE ANATUPENDA SANA MNO.

    ReplyDelete
  16. Poleni sana Wafiwa,MUNGU awape uvumilivu na kuwajaza nguvu katika hiki kipindi kigumu mtakachokuwa mna'experience gap yake.
    BWANA alitoa na BWANA akatwaa hatuna jinsi zaidi ya kulihimidi jina lake.

    ReplyDelete
  17. Oooh…………Noooo this can not be…….my God……huh!!!!! Why…..why…….why……. Nimeishiwa na maneno wallahi, Pole sana dada Yasinta, poleni sana familia ya Mzee Ngonyani.

    ReplyDelete
  18. 2 Corinthians 1:3-5
    Praise be to the God and Father of our Lord Jesus Christ, the Father of compassion and the God of all comfort, 4who comforts us in all our troubles, so that we can comfort those in any trouble with the comfort we ourselves have received from God. 5For just as the sufferings of Christ flow over into our lives, so also through Christ our comfort overflows.

    REST IN HEAVENLY PEACE ASIFIWE.
    pOle sana Yasinta,Mungu akutie nguvu maana najua uko ktk uchungu na majonzi makubwa,kuondokea na mdogo wa pekee ni kitu chenye kuumiza sana lkn hata kama ulimpenda vipi baba yake wa mbinguni alimpenda zaidi yetu ndio maana amemuita.
    POLE SANA MPENDWA WANGU.

    ReplyDelete
  19. Oh Gosh! Pole sana Da Yasinta.

    Nakumbuka nilipomtembelea hospitali muhimbili mara tu baada ya kufanyiwa upasuaji.

    Sitaki kuamini hili lakini ndo imeshatokea hivo...

    RIP Asifiwe.

    Nawaombea nguvu ndugu na jamaa na marafiki wote walioguswa kwa namna moja ama nyingine na msiba huu.

    ReplyDelete
  20. Mungu wangu!!! Ni juzi tu nimekuuliza Yasinta kuhusu mdogo wetu...Sitaki kuamini dadangu...

    Poleni Sana Yasinta, poleni pia wanablogu wote..

    R.I.P Asifiwe

    ReplyDelete
  21. Sitaki kuamini juu ya Hili, nakumbuka makala yako uliyoiweka mwaka jana mwezi Machi ukitoa shukrani kwa Mwenye enzi Mungu kwa kuitendea familia yenu miujiza kwa kufanikisha upasuaji wa moyo wa mdogo wetu huyu.

    Makala ile niliipenda sana kwa kuwa uliiandika kwa hisia na umahiri mkubwa ukionesha kufurahishwa kwako na kufanikiwa kwa upasuaji ule.

    masikini kumbe ulikuwa ni mpango wa Mungu kuwapa faraja ya muda tu, japo kuwa kwa sasa mmejawa na simanzi kwa kuondokewa na mpendwa wenu, lakini ni vyema mkatambua kuwa hivyo ndivyo iwavyo na wote ni lazima tutapita njia hiyo hiyo....

    Najua kinachotukwaza wengi ni kule kutangulia kwa yule tunayempenda, lakini hivi sisi ni nani hadi tumpangie Muumba?

    Yatupasa tukubali kuwa yote yaani lile linalotufuahisha na lile linalotusononesha yanatoka kwake.....

    Namuomba mwenye enzi Mungu awape ujasiri katika kipindi hiki kigumu na pia tumuombee dada yetu huyu aliyetangulia mbele ya haki apumzike kwa amani

    Amen

    ReplyDelete
  22. Dada Yasinta, ndugu, jamaa na marafiki, poleni sana kwa msiba huu. Tuzidi kufarijiana katika kipindi hiki kigumu. Roho ya Marehemu ipumzike kwa amani. Amen.

    ReplyDelete
  23. Pole sana kwa kufiwa na mdogo wako. Nami natuma rambirambi zangu kwako Dada Yasinta. Na kwa familia yako yote.

    ReplyDelete
  24. Pole sana kwa kufiwa na mdogo wako. Nami natuma rambirambi zangu kwako Dada Yasinta. Na kwa familia yako yote.

    ReplyDelete
  25. Pole sana Yasinta, Mungu akkupe moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. na aiweke Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi AMIN

    ReplyDelete
  26. Poleni sana na msiba. Mungu na awape faraja katika kipindi hiki kigumu. Amen.

    ReplyDelete
  27. Poleni sana, Mungu na awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
    Bwana ametoa bwana ametwaa.

    ReplyDelete
  28. Polenii sana na msiba huu, wote sisi ni wasafairi, ..Mungu ailaze roho ya mpendwa wetu mahala pema peponi. AMIN

    ReplyDelete
  29. Hizi ni habari mbaya sana.

    Mungu Akupumzishe salama Asifiwe kwani umetangulia tu.

    Na poleni sana wafiwa. Mungu Awashike mkono na kuwatia nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  30. poleni sana KWA MSIBA Mungu ailaze mahali pema pepono roho ya marehemu amina. tuko pamoja ndugu yangu

    ReplyDelete
  31. Pole sana da Yasinta na familiya ya mzee Ngonyani!Mungu awatie nguvu na moyo wa uvumilivu kwa wakati huu mgumu.

    Mungu ailaze roho ya Marehemu mdogo wetu mpendwa mahali pema peponi amina!.

    ReplyDelete
  32. Pole sana Yasinta. Mungu azidi kukupa nguvu dada yangu.

    ReplyDelete
  33. Kwa masikitiko makubwa tumepokea Msiba mzito kwa Familia yenu Mungu ailaze pema peponi Roho ya Marehemu...Timu nzima ya Mbeya yetu inawapa pole sana Familia ya Mzee Ngonyani...

    ReplyDelete
  34. Kwa masikitiko makubwa tumepokea Msiba mzito kwa Familia yenu Mungu ailaze pema peponi Roho ya Marehemu...Timu nzima ya Umabe arts inawapa pole sana Familia ya Mzee Ngonyani...

    ReplyDelete
  35. Timu nzima ya Cheka upasuke blog inapenda kutoa pole kwa Familia ya Mzee Ngonyani kwa msiba mzito ulio wapata...Tunaomba Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema Pepon amen

    ReplyDelete
  36. Kwa niaba ya timu nzima ya Amazing Tours Tunasikitika pia tunawapa pole sana ndugu na familia ya Mzee Ngonyani kwa msiba mkubwa ulio wapata Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali Pema peponi

    ReplyDelete
  37. Pole sana Dada kwa msiba mkubwa ulio wapata sisi pia tuko pamoja kimaombi..Mungu awatie nguvu..pia pole kwa Familia ya Mzee Ngonyani

    ReplyDelete
  38. Poleni sana kwa msiba!
    Mungu awape faraja.

    ReplyDelete
  39. Pole sana dada mungu alimpenda zaidi kuliko sisi.

    ReplyDelete
  40. Pole sana Yasinta. R.I.P Asifiwe

    ReplyDelete
  41. Poleni sana kwa msiba mkubwa huo. Mungu ailaze roho ya Asifiwe mahali pema peponi, Amen

    ReplyDelete
  42. Pole dada Yasinta kwa kuondokewa na mdogo wako, MUNGU akutie nguvu, roho ya marehemu iwekwe mahala pema peponi amen.

    ReplyDelete
  43. Kwa kweli ni pigo kubwa sana.Ila jipe moyo sisi Wakristu twaamini kuwa amehama makao tu,hivyo tuombe Mungu roho yake ailaze mahali pema peponi. Amen!!

    ReplyDelete
  44. katika kifo cha mtu fulani, mwandishi nguli wa afrika kusini hayati Can Themba alinukuliwa kusema "He had no business to die"

    baada ya kifo cha mtu tegemeo nilimsikia bibi yangu akisema "Po Kyala nkonyofu" (tafsiri ya haraka 'Mungu kakosea')

    panapotokea kifo cha mpendwa, kibinadamu tunahuzunika sana na tunapaswa kuhuzunika kwa kuwa hatuna uhakika (wa kibinadamu) wa kuonana na huyo mtu tena. Wote Can Themba na bibi yangu walifikiri kibinadamu zaidi. Yupo mwenye kujua hatima ya sisi tuliosalia na ndugu aliyetutoka.

    Mungu na aiweke roho ya Asifiwe pahala pema peponi. amen

    ReplyDelete
  45. Pole sana Dada Yasinta na Pole kwa Familia yote.
    Tukumbuke maneno ya Ayubu katika Uchungu mkubwa alisema "Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake na Lihimidiwe..."Job.1,21.
    Naahidi sala zangu ili Roho yake Istarehe kwa Amani.
    Pd. Nova

    ReplyDelete
  46. Pole sana Da Yasinta kwa msiba huo mzito.

    Mungu ailaze roho ya Asifiwe Ngonyani mahali pema peponi, Amina

    MAKULILO
    California, USA

    ReplyDelete
  47. Dada Yasinta na Mtani wangu, pole sana sana. Roho ya marehemu ipokelewe mbinguni. Mwenyezi Mungu akupe nguvu wewe na ndugu wote wa marehemu pamoja na sisi ili tuweze kukipita kipindi hiki kigumu kwetu wote - Amen!

    Blackmannen

    ReplyDelete
  48. Pole sana dada yasinta Mungu awatie nguvu katka kipindi hiki kingumu.Mungu ndo mfariji wetu atawafariji.pia tunatakiwa tushukuru kwa kila jambo.

    ReplyDelete
  49. Poleni sana kwa msiba, may she RIP. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki. Hakika bwana yu pamoja nanyi.

    ReplyDelete
  50. Pooooooooooooooooole sana ma dear.. Najua inauma vp kumpoteza mpendwa katika familia, Ni maombi na sala kwake mnyazi Mungu ili ampuzishe mdg wetu kwa amani.

    ReplyDelete
  51. Mwenyezi Mungu na awe nanyi wote kwa upendo na ushirikiano mloonyesha katika familia hii. Ahsantena sana hii ni kwa niaba ya wanaukoo wote. upendo daima...

    ReplyDelete
  52. Rest in peace asifiwe

    ReplyDelete
  53. Hi, dada Yasinta,
    I have just learnt about the death of your sister, Asifiwe.
    I am deeply sorry. please accept my condolence together with my apology for not contacting you for a long time and not visiting your blog where I would have got the news in time.
    I was so preoccupied with my problems. Sorry a thousand times.
    May Almighty God forgive Asifiwe's and May Almighty God rest her soul in peace.
    njonjo

    ReplyDelete