Wednesday, March 23, 2011

SUPER MUHOGO: Unga Safi wa Muhogo !!!!

Katika makuzi yangu chakula changu kikuu kilikuwa ni uji na ugali wa muhogo. Si mnajua tena ukiwa mkazi/mzaliwa wa kando ya ziwa Nyasa hiki ndo chakula kikuu. kutoka U-KACHIKI mpaka kufikia U-MBUYAMUNDU wangu hii ndo ilikuwa lishe yangu kuu. Ugali wa muhogo na majani yake KISAMVU na pia bila kusahau SAMAKI. Nilienda kumsalima Prof. Mbele ili nibadili chakula angalao nipate ugali wa MAHINDI na MAHAREGWE (mandondo). Kumbe naye siku hizi anakula ugali wa MUHOGO . Jamani tule ugali wa muhogo. Ahsanteni sana kwa kuendeleza biashara hii ya unga wa muhogo kila la kheri....Zaidi unaweza kumsoma prof. Mbele kwani naye amesema kitu. Prof.Mbele

2 comments:

  1. Hata mimi naupenda sana ugari wake nile na mboga za chukuchuku/zisizo ungwa!!!
    pia uji wake nikitia ndimu na pilipili mtama/manga!!sijui nanyi mnajua kwa jina hilo kwa kithungu ni Black Pepper!.nimesisitiza kidogo dada.

    ReplyDelete