Asifiwe Ngonyani
Kuzaliwa 26/11/1989
Kuiacha dunia 23/3/2011
Kuzikwa 26/3/2011
Asifiwe Ustarehe kwa amani peponi Amina
Habari nilizozipata leo kutoka nyumbani Ruhuwiko ni kwamba watu wengi SANA wamemiminika na wanazidi kumiminika.TWAMSHUKURU MUNGU KWA HILI.Leo tarehe 26/3/2011 siku ya jumamosi saa tatu tukwenda kuchukua mwili wa Asifiwe katika sehemu ya kuhifadhi miili katika Hospitali ya mkoa Songea. Baada ya hapo mwili wa Asifiwe unapelekwa nyumbani Ruhuwiko kwa buruani ambayo itakuwa saa tano. Saa sita mchana maandamano kwenda kanisani Ruhuwiko. Saa saba nusu mchana misa inaanza katika Kanisa la Ruhuwiko. Na baada ya hapo wote tunaandamana ili kumsindikiza mpendwa wetu ASIFIWE NGONYANI KWA SAFARI YAKE YA MWISHO. MWENYEZI MUNGU TWAKUOMBA UIPOKEE ROHO YAKE PEPONI AMINA.
FAMILIA YA MZEE NGONYANI NA FAMILIA YA NGONYANI/KLESSON ITATOA SHUKURANI ZA DHATI KWA USHIRIKIANO WENU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU!!!!
Asante kwa taarifa hii Yasinta. Ni wakati mgumu sana kwa familia yenu, lakini kumbuka Mungu yuko nanyi na wala hatawaacha hasa katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteMungu azidi kuwatia nguvu.
Amen.
Poleni sana!
ReplyDeletepole sana ,kufiwa na ndugu yako ukiwa mbali na kwenu-tanzania ningumu sana jikaze,na mungu atakusimamia. kaka s
ReplyDeletePole sana Yasinta, yaani sikumjua huyu dada lakini nimestukia nalia kama nilikuwa mtu wa wa karibu na huyu dada. Mungu akutie nguvu mpenzi.
ReplyDeletepole sana.
ReplyDeleteTunamtakia Asifiwe kupumzika kwa amani.
Amina.
Soo sad,Mungu awafariji.
ReplyDeletePole sana Dada yasinta, kwa pigo hili kubwa. Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele na lenye raha tele mpendwa Asifiwe. Pia ninyi familia kwa ujumla ili mpate nguvu zaidi katika kipindi hiki kigumu cha msiba huu mzito. Poleni sana!
ReplyDeletePole sana dada Yasinta na ndugu na jamaa wote walioguswa na msiba huu, Mungu awape nguvu na Imani katika kipindi hiki kigumu.Mungu akaweke roho yake mahala pema peponi na Mwanga wa milele akamuangazie Asifiwe Ngonyani.
ReplyDeleteAmina!
"Waache watoto waje kwangu maana ufalme ni wao" Courage,prayer,hope and blessings.
ReplyDeleteI remain.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi..
ReplyDeleteUSIJALI DADA YASINYA. YOTE HAYO YALISHAPANGWA, HIVYO HAYANA BUDI KUTOKEA KAMA TUJUAVYO HISTORIA YA MWANADAMU NA KISA CHA SHIDA ZOTE HIZI, ILA IPO SIKU YATAKOMA.
ReplyDeletehttp://mtayarishaji.blogspot.com/2011/03/je-unajua-yanayotokea.html
HATA HIVYO NIMEFANYA MUENDELEZO WA FARAJA KWA KUZUNGUMZIA JAMBO HILI KWA NAMNA INAYOTIA MOYO KWA JINSI NILIVYOGUSWA.
TUPO PAMOJA WOTE...PEACE.
Sina cha kuongea wala kuongeza katika machungu. Inasikitisha sana lakini ndio kipindi cha kuenzi na kuendeleza yale mazuri aliyoyaacha. Nafsi na mwili wake vitamezwa ardhini lakini hakika roho yake itaendelea kuishi. RIP ASIFIWE.
ReplyDeleteRIP Asifiwe!
ReplyDeletePoleni sana Ngonyani/Klaesson family
natoa pole kwa familia yake yote Bwana awafunike na kuwaondolea majonzi.
ReplyDeleteJamani was too young!!!!!!!!!!!!!.
ReplyDeleteMwili wake na ulale salama.
Hakika ni kipindi kigumu sana tena mno lakini namshukru Mungu ninyi ndugu zangu hampo nyuma, hamuachi kunitia/kututia moyo bila hivi nawaambieni leo hii ilibidi nilazwe kabisa. Lakini Sala zenu na zangu/zetu hakika zinasaidia. Ahsanteni kwa kushirikiana nasi katika safari ya kumsindikiaz ndugu yetu Asifiwe. Amina.
ReplyDeleteAma kweli nimekuwa mbali sana na blog kutokana na matatizo ya mitandao.Dada yasinta Pole sana kwa Msiba wa ndugu yetu mpendwa Asifiwe Ngonyani.Pole sana kwa ndugu na jamaa iliyo kutwa na msiba huo,Ni imani yetu Mungu amesha mpokea dada Asifiwe mahala pema peponi. Yasinta msiba huwa hauishi upesi utazidi kupokea pole nyingi sana kwa wanablogia wote wenye upendo.Kwa kawaida kazi ya Mungu haina makosa.
ReplyDeletePole sana uwe mpole sana katika kipindi hiki cha majonzi kwako.
Dada