Hapa ni marafiki wawaili waliokuja kutufariji siku ya ijumaa wote manjua mimi ni hapo katikati na kulia kwangu ni Dada mkubwa Mariana Kutoka nchini Angalo na kuchoto kwangu ni Dada Asta kutoka Ivory Coast. Hapo walinilazimisha kunywa chai na unywaji wangu wote wa chai hapo nilikuwa hoi kabisa. Wote tunawashukuru kwa kutufariji maana wanaonywsha ushirikiana mzuri. Na jana Jumapili alikuaja Dada mmoja yeye anatokea Njombe ila samahani nilitingwa kuchukua picha yake. Na picha hii hapo juu mpigaji si mwingine tena ni Erik..... nitarudi mtandaoni hivi karibuni nitengamae kwanza. MNAPENDWA WOTE...
Mungu azidi kuwafariji.
ReplyDeletePamoja sana Da Yasinta!
ReplyDeleteMungu akupe uvumilivu!
Huyo katikati ndo,watu walikuta manyoya tu kukumwenyewe kishaliwa! doh(cheka kiduchi bas!) .pole sana,mshukuru mungu unawatu hata wakuku ambia kunywa chai.mungu mkubwa.
ReplyDeletekaka s.
@Kaka S, msanii ni msanii tu huachi visa? ninaamini hata da Yasinta pamoja na majonzi amecheka kidogo..
ReplyDeleteYasinta mungu azidi kuwa nanyi, na hao kina dada wabarikiwe sana.
Pamoja daima.
Tunawashukuru sana kwa kuja kukufariji katika wakati huu mgumu, hata sisi ingelikuwa karibu tungekuja kwa wingi sana, ila kama unavyojua umbali pia majukumu ya watu, huku Ulaya hawakupi ruhusa kama unavyojua.
ReplyDeletePole zangu sana tena kwako Dada Yasinta.
Mungu azidi kukupa nguvu!wabarikiwe wageni wetu pia nasi tupo pamoja nawe!
ReplyDeleteDa mija,una juwa kwenye misiba huwa kunautani wa kimakabila/kikabila.sasa kwa yeye mpendwa mtukufu ,ndugu, kingunge Yasinta inakuwa ngumu kuwapata watu kama sisi watanizake.inasaidia sana kupunguza machungu,natamani ningekuwapo nyumbani kwake ningefanya shughuli zote kama mtani ,ila ungo wangu na kikombe kutoka kwa babu wa loliondo vina matatizo kidogo hivyo siwezi kuruka mpaka huko uliko Yasinta,na nguvu ya kikombe nayo muhimu niko kwenye foleni nikinywa tu nakamata ungo,utaniona sebuleni.kaka s.
ReplyDeleteInapendeza marafiki kufarijiana.Tunawashukuru kwa kutuwakilisha physically...siku zote tupo nanyi mentally!
ReplyDeletePole sana Dada Yasinta kwa msiba mkubwa.
ReplyDeleteNaungana nawe katika majonzi na kukuombea kwa rehma za mwenyezi Mungu akupe nguvu na kuweza kushinda vita hii ya masikitiko.
pole sana dada yasinta may the comfort of god be with you.
ReplyDeleteMungu akujaze ujasiri wa subira, kwani yote ni mapenzi ya muumba
ReplyDeleteOk! most welcome.there's time of sorrowful and time of joyful", we welcome them once more the time of joyful!but their presence is a challenge to us. Africa is One.
ReplyDeleteKind regards Yasinta( Mtani)
pole dada! msiba ukikukuta mbali huwa unauma sana. pole mungu akutie nguvu.
ReplyDeleteMungu awabariki hao wadada kwa moyo wa upendo na umoja.
ReplyDeleteKuwa ugenini; inapokuja dhida kama hii hapo ndipo utapaotamani uwe na mabawa na uruke. Lakini dada zangu hao Mariana na Asta ni kweli akina dada wa kweli tunashirikiana sana kwa raha na shida. Nawashukuru nao pia wanawashukuruni ninyi wote kwa kuwa nasi. Mbaribiwe sana.
ReplyDeleteBlog yako dada nzuri hongera sana.
ReplyDeleteNami pia ni mwanablog kama wewe,ombi langu kwako naomba link hapo globuni kwako blog yangu hii: http://allyshams.blogspot.com/
Natumaini utafanya hivyo.Nakutakia kila la heri.Mungu akubariki,
asante.
Ally
Tunawapa pole wafiwa, na tunamuombe mwenyezimungu aiweke mahali pema peponi roho ya mpendwa wetu huyo. Na Pole sana ndugu wangu,...yote ni mapenzi ya Mungu!
ReplyDelete