Wednesday, February 9, 2011

BABA NA MAMA, NI NANI AMBAYE HAKUCHEZA MCHEZO HUU?

Katika ukuaji wetu, naamini wengi wetu tumeshiriki michezo mingi ya utotoni.
Mingi ya michezo tulioshiriki ni huu wa baba na mama ambao kule kwetu Songea tumezoea kuuita Madangi.

Mchezo huu wa baba na mama huchezwa na watoto kwa kuwaiga wazazi wafanyavyo kwa kuigiza mambo ya mapishi na mambo ya mapenzi ya kitoto.

Mchezo wa Mapenzi ya kitoto ndio ambao ningependa kuuzungumzia leo. Naamini karibu wote sisi, hakuna ambaye hajapitia mchezo huu. Inasemekana watu saba kati ya kumi miongoni mwetu, hakuna asiyefahamu mchezo huo.

Hata hivyo takwimu zisizo rasmi zinaonyesha kwamba watoto wa kiume ndio wanaoshiriki zaidi mchezo huu wa mapenzi ya utotoni kwa asilimia 85, ukilinganisha na watoto wa kike ambao wao hushiriki kwa kiwango cha asilimia 75.

Mchezo huu kiukweli hauna madhara yoyote kwa kuwa washiriki wote ni watoto, isipokuwa, adhabu na kauli zinazotolewa na wazazi hugeuka sumu.
Hebu fikiria watoto wanafumaniwa na mzazi wakicheza mchezo huu wa mapenzi ya kitoto, mzazi huyo anatoa adhabu ya viboko kwa watoto hao kisha kuwaita watoto hao kuwa ni wajinga na shetani wakubwa kwa kufanya jambo hilo ambalo wakati huo litabatizwa jina la mchezo mchafu na usiofaa kabisa, na mara nyingi kauli hizi kuelekezwa kwa mtoto wa kike, lakini mtoto wa kiume huachwa tu kwani kwa wazazi wengine huonekana ni shujaa.

Mara nyingi kile tulichoambiwa utotoni ndivyo tunavyokichukulia hata ukubwani, kwa hiyo zile adhabu za kuchapwa bakora na kuambiwa kuwa huo ni mchezo mchafu na wa kishetani, hubaki akilini mwetu hata leo na ndio maana tendo la ndoa miongoni mwetu hasa wanawake linabeba taswira ya kitu cha aibu na kisichofaa. Hii inatokana na zile kauli tulizoambiwa utotoni kuwa mchezo huo ni mbaya na wa kishetani.

Wanawake ndio wahanga wa kauli hizi na ndio maana hata wale walioko kwenye ndoa wanakosa uhuru wa kujieleza kwa wenzi wao kutoridhishwa na tendo la ndoa inakuwa ni vigumu. Atawezaje kujieleza wakati alimbiwa kuwa huo ni mchezo mchafu na wa kishetani usiofaa hata chembe kufanywa na mwanaadamu?

Unaweza kukuta mwanamke ameolewa lakini hawezi kuwa huru kumueleza mwenzi wake hisia zake za kimapenzi kwa sababu ya kauli hizi kukaa kichwani na kuhisi aibu.

Kwa hiyo kwa kutumia sauti za wazazi wetu au walezi wetu na sauti ya jamii tunalitazama tendo la ndoa kama uchafu ili hali tunalihitaji na ni muhimu ili tuendelee kuwepo.

5 comments:

  1. hapa patakuwa na michango mingi sana. naisubiri.

    ReplyDelete
  2. Athari za Kisaokolojia kwa Watoto Wanaotunza Wazazi Wenye VVU
    Laure Pichegru

    JOHANNESBURG, Jul 16 (IPS) -

    Nomasonto* mwenye umri wa miaka tisa hana la kuchagua lakini kubadilishana majukumu na mama yake na kumtunza mwanamke mwenye VVU ambaye alimzaa.

    Badala ya kuhofia kuhusu kazi za shuleni alizopatiwa kufanya nyumbani na kwenda kucheza na marafiki zake, wasiwasi mkubwa wa kila siku wa Nomasonto sasa ni suala la kufa na kupona.

    Soma zaidi kisa chote hapa:
    http://www.ipsinternational.org/africa/sw/nota.asp?idnews=3497

    Najiuliza je na huyu alipitia michezo hiyo? fikra na moyo wake wa kujali umetokana na halii halisi ya mambooo/mazingira au malezi aliyoyapata.

    Ni mwanzo tu ila nitarejeaa tena kusema wakishasema waliosoma.

    ReplyDelete
  3. Mimi kwa maoni yangu,nivyema kuwa na michezo au tulicheza michezo hii,pia katika michezo hii kikubwa baba anaenda kazini na akirudi yule mke na watoto wanampokea,mama anapika na kuandaa mambo yote ya nyumbani.Hayo ndiyo tuliyokuwa tukiyaona wazazi wakiyafanya nasi kuyaiga katika mchezo wa baba na mama.
    Sasa wakianza mambo ya ndani sana ya kuchokoana hapa najiuliza wameyaona wapi? Maana zamani mambo ya kujamiiana yalikuwa na siri kubwa. Hata mama akitoka kujifungua na ukiuliza mtoto huyu mama umempata wapi atakwambia nimemnunua.
    sasa wakifanya kinyume sijui tumlaumu nani?
    na kila mchezo unafaida zake na hasara zake pia. Ngoja niishie hapa nisubiri na wengine watoe mawazo yao ili tujifunze zaidi.

    Ahsante da Yasinta!.

    ReplyDelete
  4. Hi dada yangu! umenikumbusha mbali mno maana tulikuwa na marafiki zangu tulikuwa tunaenda kuchukua ndizi mtoni na kwenda mashine na kuokota mahindi yaliyo kobolewa na kupika madangi umenikumbusha mbali sana . asante my sister.

    ReplyDelete
  5. Εvery weekend i used tο viѕit
    this web page, for the reasοn that i want enjoyment, fоr the reаsоn that this this
    ѕite cоnations tгuly pleasant funny stuff too.


    my ωeb page - instant loans

    ReplyDelete