Monday, February 7, 2011

MAONI YA PROFESA MBELE KATIKA MADA YA KAZI YA UALIMU: TAALUMA MUHIMU ILIYODHARAULIWA

Maoni haya yalitolewa na profesa Mbele tareha 3/2-2011 kwanye mada hii hapa.
Hapa ni mwenyewe profesa J.Mbele
Na hivi ndivyo alivyosema;-
Mimi ni mwalimu, na nilikuwa na wito wa kuwa mwalimu tangu nilipokuwa mdogo, sijaanza hata shule. Kila siku najitambua kuwa niliitwa na Muumba kuwa mwalimu, na sijawahi kutetereka hata siku moja, pamoja na magumu yake.

Nitatoa mifano miwili ya magumu hayo. Nilianza ualimu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1976, baada ya kuhitimu shahada ya kwanza. Baina ya mwaka 1980-86 nilikuja Marekani kusomea shahada ya uzamifu.

Nilifanya juhudi masomoni, hadi kupata tuzo ya mwanafunzi bora, nikanunua vitabu vingi sana, kwa kuelewa kuwa ndio nyenzo nitakayohitaji wakati wa kurejea tena Chuo Kikuu Dar kuendelea kufundisha.

Nilirejea nchini ule mwaka 1986 na shehena kubwa ya vitabu. Wa-Tanzania waliniuliza kama nimeleta gari ("pick-up"). Kwa vile sikuwa nimeleta gari, bali hivyo vitabu, waliniona nimechemsha.

Hii ndio hali halisi, ambayo kwangu ni ngumu. Kwa mtazamo wangu, mwalimu si mtu anayefundisha darasani tu, bali anatakiwa kuwa mfano kimaisha. Nami nilijaribu kuonyesha mfano wa kuthamini elimu.

Kinachonitatiza akilini ni kujiona ninajaribu kuwafundisha watu ambao akili zao ziko kwenye magari, na hapo darasani wanatafuta vyeti tu waende zao kusaka mali. Si kwamba wanathamini elimu kama elimu. Hawanioni mimi mwalimu kama mtu ninayewapa mfano wa kutambua nini kitu muhimu maishani, yaani elimu.

Suala la kuwasukuma wa-Tanzania watambue umuhimu wa elimu lina usumbufu na kero nyingi, kama alivyoelezea Profesa Matondo hapa.

12 comments:

  1. Da Yasinta,kabinti ka kingoni.Huyu mkuu Profesa anchoongea katika mtazamo wake kuhusu matokeo ya wale anao wafundisha,ya wezekana profesa anawasemea yaliyo mawzoni mwao/akilini mwao.sina hakika kama kila mtu anapokwenda shule kusoma ,na kupata elimu, basi lazima elimu ile ikubaliane na mawazo na mitazamo ya mtoa elimu ile, nakuwa kithibitisho kuwa kweli umefuzu na utaitumia elimu hiyo kama mwalimu wako profesa anavyotaka kama mkufunzi.kuna usemi wa kiswahili,kwamba "tenda wema usingoje shukurani" je nini shukurani ya mwanafunzi kwa mwalimu? kama mwalimu ushatimiza wajibu wako,kilicho baki nikuangalia elimu aliyo ipata mwanafunzi huyo inamsaidia katika maisha yake(magari,nyumaba,wanawake,maduka,nk.) ilibasi umfikishe mwanafunzi huko unako fikiria kusikokuwa na mawazo ya magari,nibudi kubuni zaidi katika ufundishaji ambao utamjenga mtu atika ufahamu kielimu ambao wewe kama profesa/mwalimu una ufikiria.na huo kwangu mimi ndicho hasa nakiona kina takiwa kutoka kwa mwalimu,uwezo,utashi wa kumuwezesha binadamu kupa elimu yenye thamani hiyo uisemayo profesa.zaidi ya hayo, nikuwajali waalimu kimasilahi ili watende kazi zao kwa ufasasha zaidi,na hii ni mwajili wao ambaye ni serilali.vinginevyo kweli utaona vigimu kurudi na vitabu badalaya gari. nihayo tu .kaka s.

    ReplyDelete
  2. tasnia hii ya ualimu ina mengi yanayozunguka-zunguka. awali jina tu 'mwalimu' lina ukakasi miongoni mwa jamii, hasa za mijini. linahusishwa na umasikini. Ni ukweli usiopingika ukiamua kuwa mwalimu sahau utajiri maana utajiri bado haujaona makazi katika miili ya ualimu. labda mwalimu atumie nafasi yake ya ualiku 'kuchakachua' mali na kuzielekeza kwake, mathalani kwa kupotosha matokeo ya utafiti ili kumfurahisha mwanasiasa huyu ama yule, ambaye hatimaye atakugawia bingo.

    Pili niwaonapo wanafuzi darasani siku ya kwanza sura zao na viwiliwili vyao huonyesha hamu ya kupata vyeti. kama ingewezekana basi wapatiwe vyeti tu mithili ya kibaba cha sembe dukani kwa mangi ili wakavitumie kutafuata maali.

    aah ualimu!!!

    ReplyDelete
  3. Hivi kweli kwanini `hatuna shukurani; hebu tujiulize kama asingekuwa mwalimu ungeliwa raisi, waziri, au dakitari au nani vile...je hawa watu tunawashukuruje?

    ReplyDelete
  4. PROFESSOR MBELE IS SHOOTING HIMSELF IN THE FOOT.

    (WaMerikani wale waliyomwelimisha Prof nao wangekubaliana nami labda kwa lugha yao yaKiingereza kwa kusema ‘maoni kama hayo yake Profesa ['ni sawasawa namwanajeshi aliyekaa chini kwa uvivu hata aliposikia amri mapigano yameanza kisha akajaribu kumpiga adui risasi na kwasababu hakuinuka kabla ya kurusha risasi, basi kajipiga mwenyewe guuni!']).


    Natoa maoni kwa heshima kubwa kwa Professor Mbele.

    ["...Ninajaribu kuwafundisha ..ambao akili zao ziko kwenye magari...waende zao kusaka mali"].

    Anavyotoa hayo maoni yake, hasa pale mwishoe kama nilivyonukuu hapo juu, anakuwa kama simwalimu tena.


    Amekuwa kama mtume au nabii wakuishutumu nakuilaani Sodoma kabla ya Mungu kuiteketeza.


    Kwa upande mwingine sisi sote tunaokuwa na mawazo pamoja na jitihada za kuhamasisha au kuboresha jamii zetu kimawazo nasi WALIMU SAWASAWA, kwamaoni yangu.


    Kazi yetu ni ngumu sana kama walimu. Hali ya kusikitisha kwa mwalimu halisi (CLASSICAL) kama Profesa Mbele nayo pia tunaijua waziwazi.


    Pamoja na hayo hatutakiwi hata kamwe tutoe maoni yakuwafanya wale tunayejaribu kuwaelimisha kwamba wanao mtazamo usiyofaa au “wanashughulikia ubinafsi tu”.

    Tukionyesha dharau au hata cheche moja tu ya kufikiria upungufu wa akili za hao wakufunzi wetu, dharau itaturudia sisi hapa.

    Kwao tutaonekana kama watu wakujidai mno badala ya kujigamba juu ya elimu yetu. Na wakishapata ["mali na magari waliyokimbizana nazo”] tutakiona cha mtemakuni!!!


    Si sisi tulikuwa tunakimbizana mara na vitabu vya Profesa Mbele?

    Si tulikuwa tunakimbizana namapesa yakununulia kampyuta ili “tujidai” kwamba eti tunablogi zetu kama Yasinta Ngonyani, Simon Kitururu, Fadhy Mtanga au Manyanya Phiri?

    Haya basi!!! Leo tutaona!!!

    Wao wamekwishapata magari yao sasa yakwendea sokoni 4X4, wakati Mwalimu Phiri mwenye blogi maarufu yenye umri 30 anatumia bado ile 5X5 yake ya kuingilia kaburini.

    Wacha tuone sasa nani atakuwa anakula vumbi mbioni zakwenda sokoni!

    Kwakuwa “tulijidai mno tulipokuwa tumesimama mbele yao darasani na kuwakashfu” wala hawatasaidia lolote KUBADILI JAMII MPAKA HAPO ITAKAPOMPA HESHIMA anayostahili mwalimu halisi (CLASSICAL) kama Profesa Mbele!





    Hapana kabisa, Profesa Mbele!

    Pointi umepoteza kabisa hapo.

    Ulikuwa umetingwa na kazi zingine nini, Prof?


    Labda utakuwa na muda tena wakwandika kwa mapana na marefu juu ya TOPIC hiyohiyo mpaka utufikishe pale uliyekuwa umepalenga bila kujengea walimu adui zaidi katika wanafunzi wao.

    Inaelekea wengi wameridhika na maoni yako; lakini hadi leo hii, mie mtoto waKitumbuka hujanifikisha popote bali umenichang'anya akili zaidi. Ninauhakika hata hao akinaPhiri Matanje WaMphuno Ngandunyungu mababu zangu nao wanakubaliana nami!Labda hatujaelewa Kiswahili vizuri.


    Kwa Heshima Yako Prof!

    ReplyDelete
  5. Ahsante Professa kwa kuithamini na kuipenda kazi yako

    ReplyDelete
  6. Chaguzi nyiingi na mitizamo ya wanafunzi pia hutokana na aina ya maisha aliyoishi mhusika, japo pia muelekeo wa mazingira na jinsi jamii inavyoyatizama mambo na kuyapa kipaumbele ndio chachu kuu.

    Japokuwa haya nayaeleza ila zaidi ni kutokana na kumbukumbu ya wazazi wangu waliopitia hiyo sekta ya ualimu. Tangu baba yangu alieacha hiyo kazi mwaka 1975 na kwenda kusomea uchungaji mama yangu naye akawa katika njia ile ile ya ualimu ila ni baada ya kuacha unesi.

    Mustakabali wa Profesa na jitihada zake za kuonesha mitizamo ya wanafunzi na watanzania kiuelewa ni sehemu ya hali halisi ya jinsi mambo yalivyo, haipingiki japo kila mmoja na namna yake ya kupambanua kama sio kuchanganua.

    Nakumbuka rafiki mmoja wa Baba ambaye naye alipenda sana siku moja awe mchungaji kama Baba ili wote watumike katika kanisa la wasabato Tanzania, jitihada za kumfanyia mipango ili akasomee ziliangukia pazuri maana matokeo yalionesha anastahili kwenda marekani kusoma.

    Baada ya miaka 3 naye pia alirudi na shehena kubwa sana ya vitabu...weeengi pamoja na mimi kama walivyoanza kutujenga tuliamini atakaporudi atakuwa nna gari zuri, fedha za kutosha, nguo za uhakika mabegi na mabegi-cha ajabu ikawa tofauti.

    Ukweli ni kwamba uchungaji ni wito ndio lakini kwenda ulaya sio kigezo cha kurudi na vitabu pekee...hayo yalikuwa ni maoni na mitazamo ya weeeeeengi eneoni sirari mapakani mwa kenya na tanzania wilayani tarime.

    Gumzo hilo lilidhihirisha jinsi tulivyo na upeo wa aina yake!! ina chekesha nikikumbuka hilo na ninapounganisha na hoja za Profesa. Mwisho wa yote kuna kazi kubwa sana ya kutoa ukungu fikrani katika mawazo ndani ya vichwa.

    Hilo nalo ni neno na kwa kuwa kila mmoja ana namna anavyoyatazama mambo si ajabu ukisikia mtu akipinga na kulazimisha mtizamo wake ndio utiliwe maanani, ni safari ngumu milimani.

    Nina kiu sasa maji nayo ni ya mgao...!! Tanzania bana.

    ReplyDelete
  7. Kila mtu ni mwalimu lakini sio ule wa kitaaluma!

    ReplyDelete
  8. Napenda kuchukua nafasi hii na kuwashukuruni wote kwa mchango wenu. Ni furaha kila wakati kusoma maoni yatolewayo. Karibuni tena na tena. Na ni ruksa kuendelea na mjadala wala haujafungwa.!!

    ReplyDelete
  9. Jamani, jamani tuandike Kiswahili (au hata Kiingereza) kama tuliosoma. "nabii wakuishutumu nakuilaani Sodoma." Mtu aliyesoma Kiswahili vizuri ataandika: "nabii wa kuishutumu na kuilaani Sodoma..." Pili, panga hoja zieleweke zikiwa na mtiririko. Tatu andika sentensi zilizokamilika. Kila mara jifikirie ungekuwa ndiyo msomaji, ungependa kusoma kitu kilichoandikwa vipi.

    ReplyDelete
  10. anaonymous wa mwisho hapo nakupa angalizo tu. huyo mchangiaji unayekikosoa kiswahili chake sio mswaswahili kama wewe au mimi. ni mzulu. kwa maana jinsi hii basi anajitahidi sana mosi kukitumia kiswahili pili kukienzi kiswahili, lugha isiyo yake.

    ReplyDelete