Saturday, January 8, 2011

TUNAWAEZI VIPI WATANZANIA WALIOTUWEZESHA KUFIKA HAPA TULIPO

Tanzania yetu


Habari ya Jmosi,
Nimeguswa sana na ujumbe wako wa kutakiwa kujivunia makabila yetu,kutokana na ujumbe huu likanijia wazo la kuenzi mambo mema yaliyofanywa na watu mbalimbali katika Nchi yetu ya Tanzania mpaka tukawa wamoja.

Kutokana na hilo nikazikumbuka nyimbo mbili ambazo tulikuwa tunaziimba sana shuleni katika miaka 1970-1980,na nikaona tuna kila sababu ya sisi watanzania popote tulipo kuona kuwa tunachangia kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha nchi yetu inaenedelea kuheshimika na kustawi kiuchumi. Nadhani ni jukumu la kila mtanzania popote alipo kujiuliza yeye ana mchango gani katika kuona kwanza familia yake inastawi kiuchumi na kijamii(maendeleo kwa ujumla) na kwa kufanya hivyo mwishowe tutaifanya Tanzania kustawi. Nimetanguliza kusema kuona jinsi gani familia yako inastawi maana siku hizi kuna msemo unasema Kitu kinachoitwa UZALENDO kimeondoka miongoni mwa Watanzania badala yake kuna kitu kinachoitwa UBINAFSI ambacho kinachukua nafasi ya UZALENDO. Lakini pamoja na ubinfsi kuchukua nafasi naamini kwa kuiwezesha jamii inayokuzunguka,ukoo na familia utakuwa unachangia katika ustawi wa jamii nzima na hatimaye Nchio.
Nabandika na nyimbo mbili tulizokuwa tunaziimba na kutuhamasisha ili ujikumbushe enzi hizo na kuona ni kwa jinsi gani tunawaenzi watunzi wa nyimbio hizi kwa kuifanyia Tanzania kile wao walichokuwa wanakifikiria kupitia katika nyimbo hizo

WIMBO WA HALAIKI WA TANZANIA

1.Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote;
Nchi yangu Tanzania,Jina lako ni tamu sana;
Nilalapo nakuota wewe,niamkapo ni heri mama we;
Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote;

2. Tanzania,Tanzania,ninapokuwa safarini;
Kutazama maajabu,biashara nayo makazi;
Sitaweza kusahau mimi,mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote.

3. Tanzania,Tanzania,watu wengi wanakusifu;
Siasa yako na destruri,ilituletea uhuru;
Hatuwezi kusahau sisi,mambo mema ya kwetu hakika
Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote.

Wimbo wa pili unahusu Tanzania nchi nzuri.

1.Tazama ramani,utaona nchi nzuri,
Nchi hiyo mashuhuri inaitwa Tanzania,

2.Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri;
Nchi hiyo mashuhuri inaitwa Tanzania,

3. Nchi hiyo imejaa mabonde,mito na milima;
Majira yetu haya yangekuwaje sasa,
Utumwa wa nchi Nyerere ameukomesha
Nchi hiyo mashuhuri inaitwa Tanzania.

Nakutakia Jmosi Njema. Na kaka Salehe Msanda Njombe.

5 comments:

  1. umegusia neno UZALENDO wazalendo niwachache sana kwa Tanzania yetu.Bado tuna safari ndefu katika kuijenga nchi yetu Tanzania.Labda tu niseme jambo moja ambalo limeota mizizi UBINAFSI,ambao ukiufuatilia kwa jicho la kusema NYOKO ,malalamiko,mengi ya watanzania chanzo ni ubinafsi.tunasahau kuwa kuna kesho.
    ni hayo tu,mtani wangu ,Yasinta(nyamayao was me) kaka s

    ReplyDelete
  2. Uzalendo ni muhimu lakini shurti kuwepo uwajibikaji. Siyo watu wanahangaika kujenga nchi halafu mafisadi wanajihomolea kama wanavyofanya kwa sasa akina Rostam, Kikwete, Lowassa, Chenge na wezi wengine wakubwa wakubwa.
    Tunaipenda nchi yetu kiasi cha kuijenga na wenye meno kuitafuna watakavyo.
    Zingeshughulikiwa kashfa za watajwa hapo juu angalau tungetiwa moyo. Lakini nani afanye kazi hii takatifu iwapo wao ndiyo wameshika kani?

    ReplyDelete
  3. Nashukuru kunikumbusha wimbo wa taifa letu

    ReplyDelete
  4. Kweli ujumbe mzito huu, wimbo unaogusa nyoyo za Watanzania, lakini je wimbo peke yake unatosha...mmmh vitendo ni muhimu sana, ...

    ReplyDelete
  5. Nionavyo mimi, itakuja fika wakati, hata wale waliopigania hii nchi kuwa huru, hawatakumbukwa kabisa, sababu sasa hivi watu wanachojali ni jinsi gani ya kushiba na kujilimbikizia

    ReplyDelete