Wednesday, December 22, 2010

PICHA YA WIKI HII:- JE UMEWAHI KUONA HII?

Nimeipenda picha hii, kwa nini kupoteza muda, mimi nakusuka wewe na wewe msuke binti yako . Safi sana..... ukitaka kupendeza....Lakini huyu mama anaonaje anapomsuka huyo binti?

14 comments:

  1. Dada Yssy, blog yako haikosi visa na mikasa..... Hii picha innikumbusha picha za mama yangu za utotoni, natamani niziweke pale VUKANI, lakini Mweh!! patachimbika maana mama Mkundi najua inakuwa kaaazi kweli kweli.

    Haya dada nimeipenda sana picha hii nimemuonesha mama na yeye ameipenda pia.

    Unasalimiwa na Familia ya Mzee Mkundi na wote tunakutakia Sikukuu njema ya kumaliza mwaka.

    ReplyDelete
  2. duh bila shaka kuna na michezo mingine yaweza kuchezwa kwa pamoja

    ReplyDelete
  3. Mhh, kweli nakumbuka hata wakati tukitwanga, mnaweza kutwanga watu zaidi ya waili kwenye kinu kimoja...mhhh unakumbusha watu mbali

    ReplyDelete
  4. @Yasinta: Kwa wazoefu hawahitaji kuangalia wafanyacho .Hujawahi kuona MATAIPISTI wakiendeleza soga nyingine huku wanaamngalia pengine lakini hawakosei kutaipu barua ya bosi?

    ReplyDelete
  5. Hii kali, nadhani msusi alikuwa na ratiba nyingine ya haraka.

    Aisee, ni vile tu mganga hajigangi!

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli ya kale ni dhahabu, siku hizi tunachunwa kweli kwa kulipa hela za Salon, lakini zamani. akha... watu wanakaa chini ya mwembe na kusukana bure bileshi....
    wazee wtu walifaidi kweli

    ReplyDelete
  7. Hii nitaiita wakati,muda ni mali!
    nimeipenda hii!

    ReplyDelete
  8. Ndugu zanguni hii staili kama haupo makini ndio inaweza ikakupotezea muda kabisaaaa!!Maana vichwa vinavyosukwa vitakuwa havitulii na ususi ni kutulia.

    Yasinta umeipata wapi picha hii?

    ReplyDelete
  9. Hii saloon? inapatikana nyakati hizi? Msusi wa mtoto anatupa funzo kuwa mjuzi anamacho matatu.

    ReplyDelete
  10. KWA MARA YA KWANZA NIKUPONGEZE, ILA HIYO PICHA INANIAMBIA KUWA KUMBE WAAFRIKA TUNAJALI MUDA. "TIME CONSCIOUS". LA SIVYO HAPO WANGESUBIRIANA.

    ReplyDelete
  11. nimeipenda hii imetulia,nionavyo mimi hiyo picha wasukwaji wote watapendeza na mistari itanyooka na nywele kuvutia pia.anaanza aliyesimama kumsuka aliyekaa huku aliyekaa anamchana mtoto kisha aliyesimama akifika karibu na kisogoni ,aliyekaa anainama na anaanza kumsuka mtoto usoni vizuri sana.mpaka wanamaliza,

    ReplyDelete
  12. Huyo mama anatumia uzoefu kumsuka huyo binti!

    ReplyDelete
  13. yeah hii tumeifanya sana mashuleni kuokoa muda

    ReplyDelete