Tuesday, December 21, 2010

HIVI NI IBILISI AU NI TAMAA?

Ilikuwa 2009 nilipokuwa nyumbani Songea Ruvuma. Nilikuwa nimeenda kusuka kwa waMasai, sehemu ya kusukia ilikuwa nje tu. Tena barabarani kabisa au nisema kando ya barabara.

Watu wakawa wanapita wa kila aina, bahati mbaya au nzuri akapita mwanadada mmoja ambaye ilionekana wamasai hao walikuwa wakimfahamu. Wakaanza kusema, he! Angalia mwanadada yule! Mmoja wao akawa anasema, miezi michache iliyopita alikuwa nusu kufa dada huyu, AMEATHIRIKA(VVU) na alikuwa amedhoofika sio mchezo. Lakini nasikia amepata dawa za kuongeza siku na sasa mwangalie alivyonawiri, mmmhh!

Maongezi yakawa yanaendelea, lakini maongezi yenyewe yalikuwa yakiashiria tamaa ya kimwili walivyo wamasai wale kwa kummezea mate kimwana Yule. Muda wote nilikuwa kimya nikisikiliza maongezi yao. Mara wakawa wanaulizana wapi anaishi binti Yule, na lengo ilikuwa ni kutaka kumwendea na kujivinjari naye. Mwenzenu nikabaki mdomo wazi, mweh!!!
Leo katika kuwaza kwangu ndipo mkasa huu au tukio hili likanipitia na ndio maana leo nimeona tutafakari pamoja. Je? Hii ni tamaa? Au Je? Ni kukosa kufikiri kwa makini? Maana wote walishajua kuwa ameathirika, sasa iweje wammezee mate ya kufanya naye tendo !!!?……

15 comments:

  1. nadhani pamoja na porojo zote walikuwa hawana uhakika kama ameathirika. Sidhani kama walikuwa na hakika bado wangeendelea kumfuata. lakini kama walikuwa na hakika basi itakuwa si tamaa, si ibilisi bali ni ujinga wa kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu VVU. OLE WAO WALE WAFUATAYO NYAYO ZA SIMBA...

    ReplyDelete
  2. Unajua labda kama maelezo yao yana ukweli kuwa `kweli' aliathirika' vinginevyo ni njia ya ile hadithi ya sungura ya sizitaki mbichi hizi.

    ReplyDelete
  3. Kuwasema (kuwajadili) watu kwangu mimi ni umbea. Na Pia tumezoea kusikia umbea wa namna hii kwa wadada wa saluni. Kumbe hata wanaume wakisuka nywele ni yale yale

    ReplyDelete
  4. kama walikuwa wakimaanisha basi ni ujinga. Waafrika bado tunahitaji elimu ya kila kitu, tuko nyuma sana kifikra.

    ReplyDelete
  5. da Mija keshasema kile nilichotaka kukisema...sitaki kuaharibu utamu lakini habari ndo hiyo

    ReplyDelete
  6. kwa mtaji huo itabaki miti tuu!sukari imeingia sumu.

    ReplyDelete
  7. Japo kwa sasa ninamtazamo tofauti juu ya VVU & AIDS lakini niseme mjadala wa akina Ole hao ulitawaliwa na ujinga na pengine "umbeya". Mtu hawamfamu lakini wanajua undani wa afya yake?? Inatia shaka. Kwambali naona huenda hii ni aina ya "mtego" wao kujipatia windo rahisi!

    ReplyDelete
  8. Neno moja:
    Jacob ZUMA.

    Si inakumbukwa kuwa mpaka Jacob Zuma rais wa Afika kusini alikiri hadharani kumshughulikia binti ya rafiki yake aliyejua ana mdudu na kudai alipomalizia mkito alienda kuoga ili kuzuia kupata MDUDU?


    Nijaribilo kusema:

    Kuna watu MDUDU ni ajali kazini tu kama tu kwa bahati mbaya uwezavyo kukanyaga mavi ya kuku wakati wa kwenda kazini.:-(

    ReplyDelete
  9. Tukiachana mjadala wa akina Ole, je sisi tunasemaje juu dhana hizo "ukimwi" na VVU? Kuna mchangiaji ametupatia mfano wa Prez Zuma japo hakutoa health status yake. Kwann VVU imekuwa ni tatizo kwa nchi masikini? Je tatizo la kutengenezwa (mantiki)?
    Dada samahani nataka kuacha njia.

    ReplyDelete
  10. Swali la leo lauliza "Hivi ni ibilisi ama tamaa?"
    Na kwangu jibu ni TAMAA ZA IBILISI.
    Yaani kwa tamaa hizi twamkaribisha ibilisi.
    Lakini si unajua kuwa wengine wakikosa kitu wanajifariji kuwa "kaathirika". Na wanapoona "chansi" ya kumpata wanasahau walilowaza kabla.

    Kaka na Dada zangu wamesema vema
    Nikianza na Kaka Matondo aliyesema BINADAMU..... Huyu (binadamu) kuna wakati HUWAZA KWA DHARURA. Yaani anapokuwa na shida huaz mema yote.
    Mfano...umeshawahi kuwa kwenye "situesheni" ya kuhisi umebeba ama kubebeshwa mimba? Hapo unaapa yote..Utasikia "Eee Mungu nisaidie isiwe kweli na sitafanya tena mapenzi yasiyo salama". Siku ikigundulika huna ama hana, unajipongeza kwa ngono isiyo salama.
    Kwa hiyo kuna wakati ambao huwa nawaza kuwa "tunastahili kuishi maisha ya uoga" maana kwa watu wengine, uoga wa kuvurunda huwafanya wawaze upande wa wema.
    Nasikia hata wezi wanapohisi wamezingirwa husema "nikiokoka sitaiba tena". Anayehisi atabambwa na kufukuzwa kazi naye anaomba sala ya "kuokoka" lililopo mbele yake kisha "anaapa kutorudia kosa" lakini ni wangapi hurudia?

    Waliojadili kabla yangu wamenena vema na mfano wa Kaka Kitururu ni mfano tosha
    BINADAMU

    ReplyDelete
  11. Mzee wa changamoto, naona umesherehesha mjadala, maana umejibu kiutambuzi haswaaa...
    Heshima kwako mzee.

    ReplyDelete
  12. Habari,
    Asante kwa habari hiyo hsa kama ilikuwa songea ni pale mfaranyaki au bombambili au pale penye kuku wawili weupe.

    Unachokisema ni zaidsi ya tamaa na kufikiri vizuri.

    Sisi binaadamu hasa wa kizazi hiki tumetoka katika kuyaona maisha katika uhalisi,uhitaji tumejikita katik akuyaona maisha kwa upande wa utashi- kutawaliwa na tamaa zisizokuwa na maana na kuita ni uhitaji. Zaidi ya hayo sasa hivi tuliowengi tunaendeshwa na miito ya kimwili na tumekuwa kama maroboti tunafanya mambo bila ya kufanya tafakari ya kina wa yakinifu.

    Maana katika hali halisi tendo nla ndoa ni mahususi kwa kuaajili ya kuujaza ulimwengu lakini sasa hizi linatumika kama seheme ya kupata burudani na starehe ili kupunguza maumivu y a electronic life.

    Bado tuna nafasi ya kurudi katika maandiko matatakatifu na maadili sahihi ya kuyaangalia mambo yote kwa uhalisia na ukweli wake

    Kila la kheri
    Maandalizi mema ya noel

    ReplyDelete
  13. nommmma itabidi tuendelee kuelimishana kuhusu tatizo hili mtu akiwa mnene wanataka kukimbilia

    ReplyDelete
  14. Yasinta kwani hujajua wamasai wana tabia zisizo ridhisha?, kwz wanafanya ngono ovyo ovyo,e.g akipenda mke wa rafikie hana haja ya kumtongoza, yeye huwahi na kuweka mkuki wkt rafiki yake katoka, na kwa sheria zao mwanaume ukikuta mkuki nje ya nyumba yake huruhusiwi kugonga inabidi ageuze akatafute pa kulala, na hata keshoe akirudi hana ruhusa kumwuuliza mkewe usiku alilala na nani. yeye huendelea kutwanga.


    kwz una bahati hao waliokusuka walivaa labda chupi, wengi huwa uchi na jinsia zao husimama ovyo ovyo, kutaka kucheza mchezo kila wkt.

    ReplyDelete