Monday, December 20, 2010

KATIKA MAISHA KUNA KUPENDWA NA KUCHUKIWA NA WATU


Mada hii ni marejeo niliandika mwaka 2008 bila ya kuwa na sababu isipokuwa kutaka kujua maana ya haya maneno inga kapulya.
Kupenda/upendo ni kitu cha ajabu sana mara nyingi nimekuwa nimejiuliza kwa nini sisi binadamu tuna upendo tofaoti kwa kila mtu. Nikisema hivi nina maana kuna wakati mtu inaweza kutokea unampenda mtu kiasi kwamba huwezi kujizuia. Na cha ajabu mara nyingine uanaweza kumpenda mtu ambaye hujawahi kumwona ana kwa ana(uso kwa uso) na upendo ukawa wa nguvu kali sana.

Halafu sasa inaweza kuwa kinyume kabisa. Yaani watu tunaweza kuwa na chuki. Unaonana na mtu siku moja tu na utasikia simpendi kabisa jamaa huyu. Au hata kuangalia tu picha yake unapatwa na chuki. Nashangaa sana kwa uwezo kama huu ambao MUNGU amatupa na pia SHETANI anaingilia na kuharibu.Swali:- Hivi hii inatokana na nini?
Leo nimeona niimbe mwenyewe ila samahani hamtaisikia sauti yangu:
Upendo, upendo, upendo ni amri ya bwana, Yesu alisema pendaneni, pendaneni kama nilivyowapenda. Nanyi pia, nanyi pia mpendane palipo na upendo Mungu yupo nasi tupendane tupendanex2.
Lakini pia si mbaya kama tukimsikiliza Mr Nice na ujumbe wake wa kikulacho ki nguoni mwako haya karibu....!!!

18 comments:

  1. Na pia tujiulize kwa nini mtu huyohuyo tunayempenda baadae anaweza kuwa adui yako mkubwa...na huyo unayemchukia pia anaweza kuwa ndio rafiki yako mkubwa.....wanadamu tunavituko.

    ReplyDelete
  2. Dada Edna umeuliza swali la msingi sana na nafikiria wale wanaomchukia Yasinta Ngonyani hata kufikia kumwita MNAFIKI wanastahili kujiuliza na wala hawaalazimiki kutoa jawabu kwasababu wametanguliza jawabu kuwa Yasinta Ngonyani ni MNAFIKI. Ndiyo kuna uwezekano wewe UKAMPENDA MUNGU USIYEMUONA KISHA UKAMCHUKIA YASINTA NGONYANI UNAYEMWONA NA KUMWITA MNAFIKI. halafu hata huo UNAFIKI HUSEMI. Naam nazungumzia kupendwa na kuchukiwa kama kunakotangazwa katika BLOG kwamba Yasinta Ngonyani ni mnafiki. kama somo la kupendwa na kuchukiwa ni laiki yetu wanaduamu basi kuna umuhimu wa kuatafsiri mantiki ya KUMPENDA YESU USIYEMUONA HALAFU UKAMCHUKIA YASINTA NGONYANI UNAYEMWONA. haya ni maajabu ya kasumba za wanadamu, hawa wale wanaojiita wamesoma na kuitwa wanazuoni bado wana tabia za UDAKU kwa kusema fulani namhcukia ama an=meniudhi bila kueleza sababu. H ha ha ha KAMA UNADHANI KUSEMA KWA HASIRA KWAMBA YASINTA NGONYANI NI MNAFIKI na kadhani kwa hasira zako TUTAKUELEWA endalea kutanga matusi wakati unasahau kuwa kuna watu WANAMPENDA YASINTA NGONYANI. naan siwezi kusimama katika kambi kaka Matiya ambaye amemwita Yasinta mnafiki. akiandika katika blogu yake akisema Yasinta ni mnafiki bila kueleza mintarafu ya yatokanayo. unadhani kuwaambia watu eti yamekwisha halafu ukimwita mmwenzako MNAFIKI inafuta kuwa hujamwita mnafiki? nashukuru Yasinta una akili sana hukuchangai UDAKU ule utokanao. ndiyo nazungumzia unafiki vile vile kutoeleza sababu za kumwita mtu mnafiki, tena unapoeleza hadharani tunarajai utaweka na kisa cha unafiki. lakini kama huelezi nawe ni MNAFIKI MWENYE PHD YA UNAFIKI.
    somo ka kupendwa na kuchukiwa ni refu na kwangu sijali unanipenda hunipendi naweka ............. jaza upendalo. na ufakki unatufikisha kuishi Ki-machiavelli na kujiumbia picha kwamba fulani ni shujaa wakati mwoga afadhali ya kungulu. na unafiki ni mkubwa na anastahili PONGEZI kwa unafiki. MCHARUKO HUO hapa leo, nimevumilia unafiki lakini siwezi. ndiyo maana somo la kupendwa na chukiwa linatuletea maana kwamba wpo wanafiki wenye udaku. na mantiki iliyopinda inahitaji kuwa mnafiki uliyepevuka kutosema sababu za kumwita Yasinta mnafiki.

    ndiyo maana nimekumbuka soma la Mtakatifu Kitururu kwamba kuna tafsiri zingine huleta vituko. na naamini hata hii inaleta vituko kwani unapoona BLOGU inaandika YASINTA NGONYANI MNAFIKI halafu hatuambiwi unafiki wake ni nini, unadhani inaleta picha yeoyte kama siyo UNAFIKI KWA MWANDIKAJI kijeba wa kufikiri? labda ni ndiyo maana ikaandikwa ati Yasinta mnafiki.
    UTISHIKE MHESHIMIWA KIJEBA MWENYE PHD YA UNAFIKI. au labd amaoni yangu yafutwe na mhusika mwenye blogu hii ambaye ni rafiki yangu ninayesimama upande wake. sipendi unafikiiiiiiii, au suiyo KIJEBA??

    ReplyDelete
  3. Kupenda na kuchukia yote yapo kwa mwanadamu, na ukitaka kutafsiri utajikuta unatafsiri vile uonavyo wewe ili isaidia hisia zako.
    Watu wahekima wanasema, mwenzako akikuchukia wewe mpende, kwasababu kila jambo huja kwa minajili fulani, huenda katika chuki hiyo ni sababu ya kukujenga wewe au kukuepushia wewe na jambo usilolijua, au ukafanye juhudi fulani na kugundua kitu, na matokeo yake mkawa karibu kuliko ilivyokuwa mwanzoni. Huyo huyo anayekuchukia akaja kukupa pongezi na kukupenda na kama ana hekima akaja kukuomba msamaha.
    Lakini pia wengine wanaweza wakatumia misamiati ya maneno wakiwa hawajakusudia hilo ambalo tafsiri yake inaleta hisia fulani moyoni! Huenda aliitumia kama anavyopenda kutumia mkuu MT, lakini akiwa na maana iliyojificha. Yote ni heri!
    Kama wanajamii wa blog sisi ni wanandugu, na katika kuishi kunaweza kukatokea sintofahamu ama ya tafsiri au ya hisia na mwisho wa siku sintofahamu hiyo ikikua ujirani unaweza ukaona nyasi. Hilo sio jambo jema, lazima tutafute njia ya ujirani mwema!
    Mimi naona kama imetokea sintofahamu ni vyema majirani kwanza tukasameheana na kusameheana ni ucha mungu, yule asiyemsamehe mwenzake hana upendo. Pili ni kujua nini kilichosibu hali hiyo itokee, na tatu ni kukutana na mhasimu na kumjua hali na kumuuliza nini kulikoni. Unafanya hivyo ukiwa wewe umekosewa, na kwanini bado uendelee kufanya hivyo wakati wewe ndio umekosewa, ni kwasababu hulka ya binadamu ni ubinafsi, mwingine anaona alichofanya ni sawa, kwasababu ya tafsiri, sababu ya hisia au sababu ya kusikia. Sasa wewe umeona mbali na hilo, basi jitose na umuulize jirani, nini kulikoni!
    Kupenda na kuchukia ndio hulka zetu wanadamu,na haya yamekuja kwasababu ya ubinadamu wetu. Na wakupenda au kuchukia ni sisi wenyewe, unaweza ukatengeneza upendo ukaikimbiza chuki. Basi tupendane na chuki itakimbia.
    Ni hayo tu kwa leo!

    ReplyDelete
  4. Markus: "Like dissolves like" Unyasa+Ungoni= Uruvuma+ukabila hadi kwenye blogu.Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza+ debe tupu halikosi kupiga kelele.

    ReplyDelete
  5. Annon hapo juu. Kama HUKUJUA KUHUSU MIYE na hayo makabila unayotaja, nenda katika blog ujue mie nimetokana na makabila mangapi.

    Pole miye sitokani na wangoni. Na nakuomba urudi katika kanuni za CARLO CIPOLLA.

    ha ha ha ati unanijumlisha na nomino za dhahania. ungelikuwa shupavu usingalitumia ANNON. kwamba wewe ni mnafiki mmoja wapo unayewachukia watu kwa kuwachuja na mabila. UKWELI haina nasaba zozote na KABILA LA MTU, asilani usinidanganye.

    KAMA wajua debe tu halipigi kelele, yanini kujificha na kupiga kelele? jawabu ni chuki ambayo huzaa UNAFIKI.

    kama unakijua kisa kwanini usieleze visa na visasili vyake? jibu ni chuki, na unakuwa MNAFIKI kwa kujificha. ha ha ha ha ha ha aliyenipa jina la MCHARUKO hakukosea, ingawaje sijui vigezo vyake.

    MKWELI HUSEMA UKWELI, SIYO KUSEMA LIMARKUS LIMENIUDHI SANA NA LIROHO LAKO LIMEKWAZIKA.

    halafu unaweka njia panda kikukwazacho husemi. Matokeo yake ni KUATAMASISHA KWAMBA>>>>........


    Markus: "Like dissolves like" Unyasa+Ungoni= Uruvuma+ukabila hadi kwenye blogu.Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza+ debe tupu halikosi kupiga kelele.""""""


    ANONN ongeza na mengineyo bado haijtosha, napenda kuelezewa kwa staili yako inanikurohua nafsi. ha ha ha ha ha ha ha watu wa waa wa wea we akwaaaa akwaaa nakuongezea utoto ili uendelee kujificha ha ha ha LOL......

    ReplyDelete
  6. Kinachotusibu ni kuwa tuliowengi tuna njaa ya kupendwa wakati suala la kupenda ni la kwako binafsi na wala huna uwezo wa kumlazimisha mtu kukupenda.

    Kwa maana nyepesi kupenda ni kumkubali mtu kama alivyo bila ya kujaribu kumbadilisha na kutakua kuwa kama wewe unavyotaka.
    Kingine kinachotokea mara nyingi tunaita kupenda kumbe si kupenda bali tunaweza kusema kuvutiwa au kutamani. Kwa upande wa pili hilo la kumchukia tu mtu ni suala la kimaumbile ambalo linahitaji utafiti wa kina wansayansi jamii na saikolojia watusaidie.

    Kila la kheri na hongera kwA KUTUIMBIA WIMBO WA UPENDO

    maandalizi mema ya noel

    ReplyDelete
  7. Kaka Salehe, ni muhimu umeelza vema juu ya suala hilo. Lakini kama mtu humpendi kuna haja ya kumtusi mwenzako na kumwambia ni CHUI NDANI YA NGOZI YA KODNOO? kama amekuudhi kwa sababu ambayo kwako ya msingi mwambie na unapoeleza mbele za watu sema Limarkus limeniudhi hap na pale. mbona wenzetu wa ustawi wa jamii wanayo Pyschological contact?

    iweje leo mtu anamwita mwenzke mnafiki halafu hakuelezwi yatokayo? Binafsi mtu anipende asinipende nitamwambia arejee KANUNI ZA CARLO CIPOLLA.
    ndiyo maana naungana na dada EDNA katika maoni yake

    ReplyDelete
  8. Markus: Think rationally, argue wisely and finally, try as much as you can to control your emotional outburst! Mind your own business.

    ReplyDelete
  9. akurudia ANNON na kwakuwa najua wewe uandikaye ni nani, na kwakuwa mie ni gwiji la maandiko, nakuambia mie ni mwendawazimu ambaye najisikia kuandika kwakuwa nina uhuru wa kuandika.

    LAITI UNGELIKUWA NA HEKIMA USINGELIJIFICHA. LAKITI UNGELIJUA HEKIMA NA AKILI NI MUHIMU SUINGELIANDIKA. NA KAMA UNADHANI KUANDIKA TU KITUMWA NA KWA LUGHA YA WATUMWA NDIYO SOMO huria na mintarafu inayoeleweka, basi sitosita kukueleza FIKRA ZAKO ZIMEKATA ROHO. MWENYE KUJIGAMBA AMEKULA NONDO ANAANDIKA KIUDAKU? ANAYEKULA NONDO ANAANDIKA UMBEYA ATI NIMEUDHIWA? KAMA WEWE NI MWANAMMME KWELI JITOKEZE MBONA WAJIFICHA RAFIKI?
    ha ha ha unajisumbua ati nihusudu yangu, ndiyo haya ni sehemu ya yanga, wala haigombi kukueleza UMEKUWA MMOJA WATU WENYE KUJIVALIA SUTI KWA KUUFICHA UJINGA WAKO.... ha ha ha ha ha ha pasua angaaaaa. ha ha ha NIKO SIMPO MNO ndiyo maana najikuta vidole vinawasha kuandika tuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

    RUDI KASOME MAANDIKO YA KANUNI ZA carlo cipolla

    NILIZALIWA ILI NISEME UKWELI SIYO KUFICHA UKWELI.

    KWANINI UFUGE VIROBOTO UOGOPE KUTOA FUNZA?

    ReplyDelete
  10. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  11. Markus: Keen writers always read carefully. Your arrogance and pompous behaviour made you a careless and superficial reader.Shame on you! Read twice before you write gabbage.

    ReplyDelete
  12. ENDELEA KUBWATA ENDELEA KUBWEKA.

    NATAKA USEME KINYWANI MWAKO. hii nafanya MAKUSUDI ILI UAPTE GHADHABU NA KUONGEZA JUHUDI, ninachoandika sikisomi kwasbabu sina sababu ya kukuheshimu ili usome vema.

    unaandika maoni unafuta, kisha jina lako linabaki. Nani katoa MBWEO hapa kama siyo wewe na laiki ya wa wanafiki? ha ha ha ha NA BADO NIPO NAWE KWENYE MSTARI IWE USIKU AMA MCHANA NITAKWENDA SAMBAMBA HAKA UKIJAMBA.......
    ha ha ha ha JITU LENYE UHAKIKA HALIMCHUNGULII MKEWE

    kwanini ujifiche yahkeeeeeee.

    UNAVAA SUTI KUFICHA UJINGA WAKO?

    jamaa zangu wa Jamii Forum wanasema FICHA UPUMBAVU WAKO, USIFICHE HEKIMA ZAKO. yanini kuficha kile ambachp naamini sivyo inavyoapswa kuwa. na tatizo la kwanza wadhani MARKUS ni pungwani lenye hasira kama zako za kuandika MTU AMEVAA NGOZI YA KONDOOO ha ha ha ha ha ha ha ha ha ULIAZIMA AKILI YAKHEEEEEEE

    ReplyDelete
  13. Markus: I am not the man of your own calibre. You deserve to be arguing with Wapiga debe wa pale ubongo bus stand, your share a lot in common in terms of personality. Low self-esteem is all you are suffering!

    ReplyDelete
  14. ANNON;
    ONGEZA JINGINE HILO HALITOSHI. TENA LINASTAHILI KUAMBIWA MTOTO WA CHEKECHEA.
    KUTOKUWA KALIBA YAKO HAKUMAANISHI NIKUBALIANE NAWE KILA USEMALO. HUJIULIZ KWANINI wanazuoni wanasoma mawazo ya Sacrotes? Bado ongeza jingine wapiga debe halitoshi, na taswira ninayokuumbiwa NAOMBA UONGEZE NATOKA HOSPITALI YA VICHAA PALE MIREMBE, DODOMA.
    ha ha ha ha ha ha ha ha ha hewala mkuu! ubarikiwe kwa kulka NONDOZI ambazo unataka sote tukubaliane.

    NAOMBA UONGEZE JINGINE, ikifaa nifananishe na yule Profesa aliyeanzisha genge na Laska el Toiba.

    NINA KIU YA KUENDELEA KUKUSIKILIZA. HALAFU NGOMA NIKUTAKIE KRIMASI NJEMA RAFIKI AU VIPI MKUU NONDOZI. Lol

    ReplyDelete
  15. Markus: Merry Christmas and happy new year 2011.

    ReplyDelete
  16. Markus: Kama mdogo wangu na rafiki yangu, najua unanijali la sivyo usingejibu mapigo yangu. Fundisho kwako na Yasinta, pamoja na Chib. najua chib ni gentleman, I always honour him, pengine he was just too busy to read all. Wakati mimi nampongeza rafiki yangu toka Mozambique kwa kula nondo yake ya PhD, nyie mumenihukumu kuwa mimi ndiye niliyekula nondo hiyo,kumbe mimi ni kapuku tu. Umenihukumu kuwa najigamba kula nondo kumbe sivyo. Mwisho wa yote niseme nawapenda na ninawaomba mkasome ile posti ya nondo kwa mara nyingine. Ni kwa msingi huu mimi nikakuhukumu kuwa you are not a keen reader as you proclaim! God bless you! Kiipis!

    ReplyDelete
  17. Kama kaka yangn nastahiki kukupa heshima yako. kama mkubwa wangu nastahii kufuata taratibu zote za kiafrika. na kama binadamu nastahiki kukueleza kwamba nakuheshimu sana. Hilo ndilo kusudio.

    Pamoja na hayo katika heshima na kukupa kila lililostahiki ukubwa ni muhimu kuelewa kuwa NONDOZI haikumaanisha juu ya posti husika ndugu yangu, BALI nilifanya hivyo kwasababu mie utashi wangu mdogo ninaandika kiswahili lugha maridadi ya kwetu ninayoamini itaniletea maendeleo anuai ikiwemo maarifa mapya. Kwahiyo nikadhani kiingereza ndiyo NONDOZI ya kueleweka sana.

    Na katika yote ninayoandika wala hayana chembe za HASIRA WALA DHARAU. bali tunajaribu kuelezana tu hapa na huwa siafiki kuelezana pasipo kutazama kwa kina na kuweka usawa wa stahiki ya mtu.

    ndiyo maana unaona makosa ya kimaandishi sana nilimaanisha sikujali sana ninachoandika labda kwa lugha ya kigeni ningesema MARKUS IS CARELESS ONE. hapo ndipo unaweza kuona ni kwanini nilishupalia tu, na wala sikuona haja ya kuacha kwasbabu nilijua ninayeandikiana ni mtu mzima. ingelikuwa nimekwisha kuacha kitambo kama ingelikuwa ni wale wapendao SHARi.

    NIMEMALIZA. Na sitoacha kukupa heshima yako mkuu lakini bila shaka ukweli hauna umri wala nasaba. nikikosea nami nikosolewe mwanzo hadi mwisho... dosari zisemwe kwa lugha yoyote iwe chungu ama iliyopozwa. nawakaribishwa waungwana

    DAIMA NAPENDA UKWELI MCHUNGU, SIYO UKWELI MTAMU.

    kwaheri hapa

    ReplyDelete