Tuesday, November 16, 2010

TUKUMBUKE KUTAMKA HAYA,

Sijui kuna wangapi huwa wanasema haya maneno mara kwa mara kwa mara. Kama kawaida yangu Kapulya mdadisi leo nimedadidi kitu kwa msomaji wa Maisha na mafanikio na mnimepata jibu na nimeona ni vema niwape elimu hii na wenzangu. Haya endelea hapa chini.

Ukiona jambo zuri watakiwa kusema “mashaallah”, yaani mapenzi ya mungu yatimizwe.
Ukiahidiwa jambo unatakiwa kusema “Inshaallah”, yaani litawezekana kwa utashi wa mungu.
Ukihisi maumivu unatakiwa kusema “laailaha illa allah” hakuna mwingine ila ni wewe mungu wangu.
Ukiahidi jambo unasema “bi idhinillah” kwa idhini ya mungu
Ukipata neema unasema “alhamdu lillah” yaani nakushukuru ewe mungu wangu
Ukikasirika unasema “ Audhubillah” yaani mungu niepushe
Ukistaajabu unasema “subhanallah’’ ewe mungu ndiye mpangaji wa yote.
Ukitendewa wema unasema “jazakallah” yaani mungu akuongezee.

5 comments:

  1. Idd mubaraka! Kweli wewe umeiva, kwani unacheza namba zote, natumai hata wewe unayasema haya maneno, kwani yana maana kubwa sana, kwamba kila kitu unamweka mungu mbele!

    ReplyDelete
  2. Natamani ningeyasoma hayo maneno kwa lugha yake halisi!

    ReplyDelete
  3. Da Yasinta - ushasilimu nini? Angalia usije ukawalize Wakatoliki!

    Maneno haya yanatamkwaje katika Kingoni? Au ni lazima yawe na ladha ya Kiarabuarabu?

    ReplyDelete
  4. Usiige tu mama, angalia!

    ReplyDelete