Thursday, October 7, 2010

Wanamitindo na warembo wa wiki hii ni hawa:- kumbe tupo wengi tunaopenda kutinga mgololi!!!


Yasinta Ngonyani na Salma Kikwete

Mama wa Maisha na Mafanikio na vazi lake la asili la mgololi na halafu hapo si mwingine tena ni mama Salma Kikwete akiwa naye ametinga vazi la asili aina ya mgololi. Ebu angalia ni kitu gani unaona ni tofauti au sawa katika picha hii:-) TUTAONANA WAKATI UJAO!!!

12 comments:

  1. Hivi mgololi si ndio huohuo wanaume huuvaa pia?

    ReplyDelete
  2. Ahsante Edna!

    Simon! Ni kweli je wewe umewahi kuva hivyo na kama ndio badi naiomba hiyo picha uwe mwanmtindo wiki ijayo:-)

    ReplyDelete
  3. @Demu Yasinta: Sina mgololi ila nafikiria kuanza kuvaa nikipata mpenzi hivi karibuni ili tuwe tunashea nguo ili kubana matumizi.

    Si unajua miye ni Mpare na Wapare kwa kubana matumizi ndio maprofesa, kwahiyo hebu fikiria ikiwa kila nguo ni za Bibi na Bwana na ugomvi ni kugombea tu lini Mimi au Kipenzi ndani ya siku ni zamu yanani kuvaa mgololi wenye rangi ya kijani kama wewe- itakavyo sevu bajeti ya nguo.:-)

    ReplyDelete
  4. Mt. Hiyo itakuwa bombi kweli kuvaa mgololi mmoja na mpenzio (wifi) Ni kweli nimesikia hiyo kuwa wapare ni wabahili kweli. Haya nakutakia kila la kheri katika kufikiria kutafuta huyo mpenzi:-)

    ReplyDelete
  5. Kweli nawapa tano bora...niliwaza mbali kwani hapo upo na nani vile??? mmmh, au nawe unataraji kuwa `first lady nini?' ni mawazo tu

    ReplyDelete
  6. Candy1! haswaaaaa:-)

    emu-three! huwezi kujua ya mbele:-)

    ReplyDelete
  7. Tena ingependeza kama ungekuja kuwa First Lady wa hapo Sweden Yasinta...lol..!!

    ReplyDelete
  8. Hivi mgololi asili yake wapi mara ya kwanza nilisikia neon hili mkoani iringa 1987 walipomvika hayati mwl nyerere alipokuwa ziarani huko

    ReplyDelete
  9. so cute

    Huo unavaa wenyewe na brezia tu bila nguo ingine ndani?

    ReplyDelete