Monday, October 11, 2010

SWALI :- NANI ALIZIPA HIZI NCHI MAJINA NA LUGHA ZAKE??

Nani alitoa majina ya hizi nchi?

Siku, miezi na hadi miaka imepita huku nikijiuliza hivi KWA NINI au NI NANI alisema/amua haya majina ya hizi nchi zetu? Pia lugha za nchi? Kwa mfano nchi Tanzania lugha kiswahili. KWA NINI?

Na ndio nikaona niliweka hili swali hapa kibarazani ili tujadili kwa pamoja. Kwani Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

14 comments:

  1. rejea mkutano wa Berlin kule ujermani japo mnadai nyerere ni baba wa taifa wakati hakuwepo berlin conference

    ReplyDelete
  2. ha ha haaaa!

    Kamala, kumbe baba wa taifa ni mjerumani? Na lugha yako ulipewa na wajerumani?

    Ni lazima kuna aliyewaita...kwa mfano: nyote mnajua kuwa Singida kuna wanyaturu. Lakini kiuhalisia hakuna kabila liitwavyo hivo.

    Waliitwa hivyo kwa kuwa walipokuwa wanawasaidia wakoloni kufuatilia nyayo za ng'ombe walioibwa walikuwa wakisema 'turu' wakimaanisha 'hapa ama hizi hapa' yaani nyayo za ng'ombe.

    Hivyo wakoloni walipokuwa wanafanya survey ya rasilimali walielekezwa na wenzao kuwa mkifika eneo hili mtakuta waTURU lakini kabila lao halisi ni WaRIMI yaani wakulima!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Swali zuri Yasinta, Chacha asante kwa jibu lako nina hakika utakuwa unajua na asili ya jina Sukuma au Wasukuma.....nasubiri

    ReplyDelete
  4. ha ha ha ha haa! Da Mija una mambo..labda hilo tumuachie Mwl. Matondo atudadavulie!!!!

    ReplyDelete
  5. Mada kali na tamu sana hii. Hapa ndipo penye hekima na akili. Ni moja mijadala ambayo wanazuoni wanapaswa kufanya utafiti juu ya hali halisi. Kwa mfano kuna jamaa anafanya utafiti wa lugha za mwambao wa Mbamba Bay hadi mpakani Msumbiji na TZ ili kufahamu mahusiano yao na Malawi(Wamwera). Hili ndilo jambo bora.

    Na vilevile nimelazimika kuanza kuweka makala zinazoelezea historia ya MTU MWEUSI ili tujadili kwa kina(fuatilia hapa; www.fananinyasa.blogspot.com). huo utakuwa mfululizo ambao kaka Kamala utamfumbua macho, maana dhana ya Berlin haiakisi suala la majina bali inachoakisi ni mipaka ya nchi na namna ilivyotengenisha jamii zetu. Ndiyo maana Obama akiwa pale Accra alithubutu kusema nguvu ya mahusiano ya binadamu hayana mipaka, hakuna mpka utakaoweza kuzuia hilo. labda kweliiiii.

    sasa suala la kusema ilikuwa basi tumfaute kaka Matondo nina hakika katika utafiti wake wa Isimu atakuwa na la kusema haya mambo. na mzee wetu Mbele atasema juu ya MATENGO FOLKTALES, maana nina historia ya makabila mawili ya WAMATENGO na WANDENDEULE ambayo niliipata kwa wazee fulani pale Songea kwahiyo suala la majina ni rahisi sana Dada Yasinta a.k.a Kapulya, mimi ugumu upo katika uwepo wa mwanadamu kwanini 'TULIUMBWA KWA MFANO WAO'? ha ha ha ha nisihame topiki..... nashukuru kaka Chacha a.k.a mzee wa kitambi ametujibu kiufasaha sana ingawaje ni fupi. heshima kwako kaka Chacha, ni bonge la habari nzima na kitabu juu yake.

    ReplyDelete
  6. nyongeza bado napakua juu ya HISTORIA ni KWANINI ILIANDIKWA SANA KIPINDI CHA HUYU MTU AITWAYE CHRISTOPHER COLUMBUS? ni kweli aliivumbua Marekani huyu bwana punde mwaka 1492 ndipo historia ya dunia ilianza hapo?

    ni aina ya maswali ambayo yanafanana na mada hii ya dada yasinta. hongereni mnaojadili...

    ReplyDelete
  7. Wanahistoria wanasema Christopher Columbus ndiye alikuwa wa kwanza kuvumbua Amerika, nadhani si kweli kwani tayari Amerika kabla ya kufika Columbus waliishi Waamerika wazaliwa (Native Americans au Red Indians),nadhani hawa waweza kuwa wa kwanza na si Columbus.Inahitaji utafiti mkubwa.

    ReplyDelete
  8. Wachangiaji maoni naona mmekwepa kujibu swali. Swali ni nini asili ya majina ya nchi zetu kama sikose.
    Nitaongelea Kenya Tanzania na Uganda.
    Kenya inatokana na lugha ya kikamba ingawa wakikuyu walikuja na madai kuwa Kenya inatokana Kirinyaga. Kirinyaa, Kiinyaa au Kerinyaga yaani mlima wenye weupe (barafu juu pia kuna wanaosema kuwa Kenya maana yake ni nchi yenye mbuni.

    Tanzania imepata jina hili kutokana na kufanyika mashindano ya kutafuta jina la nchi. Majina mengi yalipendekezwa likachukuliwa la Tanzania.
    Uganda inatokana na Buganda, kabila kubwa nchini mle. Muda hautoshi. Unaweza kufanya utafiti wako na kujibu hoja ya Yacintha kama alivyolitundika.

    ReplyDelete
  9. Kwa uelewa wangu mdogo nadhani Tanzania imetokana na kuunganisha nchi mbili Tanganyika na Zanzibar, hivyo kuchukua herufi za mwanzo tatu kwa kila nchi.

    ReplyDelete
  10. Usiye na jina wa October 12, 2010 4:44 AM! Na je? Tanganyika ilitokana na nini na pia Zanzibar? Majina haya nani aliyapa nchi hizi?

    ReplyDelete
  11. Ukipata jibu niambie manake nami huwa najiuliza swali kama lako, au yawezekana zilikuwa zinapewa majina na watu wenyeji, eg. sehemu za Dar kama Buguruni kuna mzee alikuwa anashona malapa, na hilo eneo likapewa jina la Malapa (Buguruni malapa).

    ReplyDelete
  12. Dada yangu Yasinta.
    Tanganyika ni kiunganisho cha maneno mawili, Tanga na Nyika.Maana ya Tanga kama ujuavyo ni usafili wa majini kwa kiswahili chepesi mtumbwi, na maana ya nyika ni msitu. kwa hiyo, wageni waliovamia eneo hili na baada ya kugawana huko Berlin wakaamua kuita Tanganyika kwa maana ya eneo ambalo limezungukwa pembeni na maji wakati katikati ni misitu.
    Zanzibar ni neno la kiarabu, maana yake "Zayn Z'al Barr" likiwa na maana ya eneo(ardhi) yenye haki(usawa).
    Natumaini kwa hilo umepata mwanga kidogo.

    ReplyDelete
  13. Bahati Zabroni LuvanzaOctober 12, 2010 at 1:55 PM

    kila kitu unachokiona kimetokea na hujui ilikuwaje ujue kuwa yupo aliye juu yako anayefikisha hapo ikiwa ni mema Mungu muumba wa mbingu na nchi anahusuka kama ni baya ibilisi ndio kazi yake.

    ReplyDelete
  14. hapa kuna utata kipenzi for me natamani na sisi tungekuwa tunatumia kingereza tokea zamani..kama nchi nyingine za Africa

    ReplyDelete