Saturday, October 9, 2010

Usijemuahidi mwenye upere kucha. DC atolewa mkuku Maghala ya Hifadhi ya chakula Ruhuwiko

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Savery Maketa, (Mwenye Suti) akizomewa na wakulima wanaosotea kuuza mahindi yao kwa wiki tatu sasa katika Maghala ya Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula Kanda ya Songea Ruhuwiko Manispaa ya Songea jana (Picha na Muhidin Amri-Ndolanga) Tatizo la soko la mahindi mkoani hapa limechukua sura mpya ambapo watu wanakesha usiku na mchana kusotea kuuza mahindi yao, Dc huyo alionekana kama bughudha na hana uwezo wa kuwasaidia hivyo kutimuliwa kama muionavyo hiyo picha. Dada Yasinta na mnaofuatilia Blog yenu hii mmeona mambo hayo?

habari hii nimeipata kutoka hapa na nimeona si vibaya kama nami nikiiweka hapa Maisha na mafanikia na ukizingatia ni nia moja.

3 comments:

  1. wakati mwingine ahadi ni deni... maana hata kama mvumilivu hula MBOVU na siyo mbivu. kwakuwa anajua kuwa ukimletea upere utakuna na kushuhudia mengineyo yatokanayo na upere......

    ReplyDelete
  2. hahahahah mwaka huu mbona watazomewa hadi wachanganyikiwe,,watu wamewashtukia na uongo wao,,,

    ReplyDelete
  3. wangekuwa kwetu kule mpakani na Kenya wasingesota kubembezea wanunuzi waje, yananunuliwa kama pipi tena haraka na pesa ya uhakika, ndio maana hata wakipiga kelele sisi tunayauza hata kwa kupitia njia za panya

    ReplyDelete