Sunday, September 19, 2010

HESHIMA YA MWANAMKE NA WITO WAKE!!!!

"Mwnamke kama Mama na mlezi wa kwanza wa mwanadamu ana haki ya pekee kabla ya mwanaume. Umama kwa upande wa utu na maadili unaonyesha uwezo wa mwanamke wa kuumba ulivyo muhimu sana ambao unadhihirisha wito wa pekee na ni changamoto ya pekee inayomchochea mwanmume na ubaba wake"


"Heshima ya mwanamke hutegemea utaratibu wa upendo, nao ni hasa utaratibu wa haki na wa kupendana.."



"Hongera kwa mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha!" Yesu akajibu, "Barabara; lakini heri yake zaidi yule anayelisikia neno la Mungu na kulishika" (Lk 11:27-28). NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA KWA WOTE !!!!!!

6 comments:

  1. "Mwnamke kama Mama na mlezi wa kwanza wa mwanadamu ana haki ya pekee kabla ya mwanaume"

    Lakini mwanaume ndiye aliumbwa kabla ya mwanamke au?

    Naamini katika usawa wa kijinsia (usiopindukia kimo) na kwangu mama ndiye alpha na Omega. Tazama maoni yangu kuhusu nafasi ya mwanamke katika maisha yangu hapa:

    http://matondo.blogspot.com/2010/05/dunia-ingekuwaje-bila-mwanamke-happy.html

    Akina mama - nawapenda na kuwaheshimu sana!!!!!

    ReplyDelete
  2. kwa kweli kuhusu mada hiyo heshima ya mwananke hutegemea
    kwanza hishima pili tabia tatu upendo nne utaratibu mwanamke akiwa na
    sifa hizo
    mungu atampa maisha marefu hata kwa mungu na wanadamu

    ReplyDelete
  3. Ama kweli mke mwema hutokana na malezi bora, na ili umpate inabidi na wewe pia uwe na tabia njema na kumuomba sana bwana mungu wako!

    ReplyDelete
  4. Ahsanteni sana kaka zangu na pia wengine mliopita hapa na kusoma . Na pia kumbukeni mnapendwa wote. Jumapili yangu mie ilikuwa njema tu kwani nilipata muda wa kuwa na familia yangu kwani hicho ni muhimi sana kwangu.

    ReplyDelete