Monday, September 20, 2010

NILIDHANI KUWA NI KAPULYA MDADISI TU KUMBE KUNA:- KIMWAGA MDADISI PIA!!!

Raha ya kujua kusoma


Nimekisoma mimi na sasa watoto wangu wanasoma ama kweli raha
Nilikuwa nimeishau hii hadithi, nilidhani kuna Kapulya mdadisi tu kumbe! Nadhani kuna wengi tunakumbuka darasa la tatu tulipokuwa tukisoma hadithi hizi :-haya hebu fuatana nami pia mtoto Erik katika hadithi hii ya KIMWAGA MDADISI.


Hapo zamani palikuwa na motto moja aliitwa Kimwaga. Mtoto Hugo alimpenda sana babu yrke Lukindo. Kimwaga na babu yrke waliishi katika kijiji cha Kwemasafi, Wilayani Korogwe. Jioni, baada ya jua kuzama, Kimwaga alikuwa akikoka moto kwenye Kilanda chao cha mazungumzo. Babu yrke alikuwa akipenda sana kuota moto na kuzungumza na mjukuu Wake.

Siku moja jioni, Mzee Lukindo na Kimwaga walikuwa wakiota moto. Kimwaga alikuwa motto mdadis sana. Alimsimulia babu yrke habari moja iliyomshangaza. Alisema, “Babu, leo tulikuwa tukilima katika samba letu la shule. Mimi niliinua jembe kwa Nguru ili nichimbue magugu. Jembe likagonga jiwe, nikaona cheche za moto zinamulika. Hivi babu moto ulitoka wap?”

Babau yrke akamuuliza, “Hivi mjukuu wangu hujui hadithi ya moto?” Kimwaga akamjibu, “Sijui,” Babu yrke akamwambia, “Basi nikueleze kidogo, Hapo zamani za kale binadamu hawakuwa na moto. Waliishi katika mapango yenye giza. Walikula matunda na Nyala mbichi. Maisha yao yalikuwa ya tabu sana.

“Kwa Bahai, siku moja mzee moja akachukua mawe, akayagongagonga ili yavunjike apate jiwe la kuchimbia viazi mwitu. Alipoyagonga aliona yakitoka cheche za moto. Akafikiri sana. Halafu akaweka manyasi makavu karibu na ylle mawe, na akaendelea kuyagongagonga. Mara ylle manyasi yakawaka moto. Kumbe alikuwa amegundua moto kama ulivyoona wewe leo wakati ulipolima huko shuleni.”

Kimwaga akamwambia babu yrke, “Kumbe hata mimik nimegundua moto.” Kisha akaendelea, “Babu, juzi tulipokuwa tunatoka shule tulinyeshewa na mua tukalowa. Tulipofika kwenye samba moja tulijificha chini ya Kilanda kimoja kidogo. Mwenzetu Kimweri akapekechapekecha vijiti viwili vikavu. Mara tukapata moto, tukautumia kwa kukaushia nguo zetu. Je, babu moto ule ulitoka wapi?”

Mzee Lukindo akasema , “Aaa, wewe Kimwaga unadadisi sana. Basi nitakueleza hadithi nyingine. Hapo zamani sana, kabla mimi sijazaliwa, palikuwa na motto moja mtundu sana. Siku moja alitaka kutoboa kigogo kikavu ili atengeneze kidude cha kuchezea. Akachukua kijiti akaanza kupekecha. Kile kigogo kikatoa unga mweusi. Akaendelea kupekecha kwa nguvu sana. Akaona Moshe. Mwisho ule unga mweusi ukashika moto. Akachukua nyasi kavu na kuziweka karibu na ule unga. Nyasi zikawaka moto. Kumbe naye alikuwa amegundua moto.”

Siku nyingine tena, Kimwaga akamweleza babu yrke namna alivyomtazama buibui. Akamuuliza babu yrke, “Je, babu, ule uti ambao buibui hujengea nyumba unatoka wap?” Mzee Lukindo akajibu, “Buibui ni mdudu wa ajabu. Anapotaka kujenga nyumba yrke, hutoa maji kutoka tumboni make. Maji haya yanapotoka nje tu huganda, na anapokwenda huonekana kama uti.”

Babu yrke Kimwaga alipomaliza kusimulia habari za buibui, Kimwaga alikuwa anasinzia kwa sababu siku ile alichelewa sana kwenda kulala. Mzee Lukindo akamwambia, “Sasa mjukuu wangu, Nena ukalale. Nitakueleza hadithi nyingine kesho.” Kimwaga akaenda zake kulala.

10 comments:

  1. hivi huyo 'litle man' Kiswahili kinapanda kweli

    ReplyDelete
  2. kaka John yaani ungejua hata usingesema. Kiswahili hapa ndo nyumbani...

    ReplyDelete
  3. Naongeza, Nimezungumza mara kadhaa na chijana huyu chijana Erick. anabonga kweli chiswahili bin kiswahili...... Ila tatizo lake anapenda sana kuogelea utadhani samaki duh!!! ama kweli wanyasa+wangoni+waswidi= wamechakachua... mweeeeeeeeeeeeee

    Ila nimekukosa kweli kweli Erick, haya bwana wewe jificheeeeee tu

    ReplyDelete
  4. typos kwenye hii hadithi duh!

    ReplyDelete
  5. Safi sana kama ananyaka kiswahili. Nilikuwa najiuliza kama Mwaipopo

    ReplyDelete
  6. Hivi vitabu ni hazina, mimi sina hata kimoja labda vya sekondari

    ReplyDelete
  7. Hongera sana kama kiswahili kinapanda maana watoto ni wepesi sana kushika lugh ya sehemu wanayokaa na kupoteza lugha nyingine.
    Vitabu kama hivyo, kwa watoto ni vizuri sana, nakumbuka vitabu nilivyosoma mimi nikiwa mdogo, kama vya sungura mjanja, bulicheka, safari za sinbad nk, sijui kama vinapatikana!

    ReplyDelete
  8. Markus! "Ila tatizo lake anapenda sana kuogelea utadhani samaki duh!!! ama kweli wanyasa+wangoni+waswidi= wamechakachua" Nimecheka kweli hapa mweeh!!

    Usiye na jina :-)

    Kaka Chib! Utashindwa wewe:-)

    padiri Chacha! we acha tu!!
    Kaka Bennet! Ni hazina kubwa sana basi itabidi ufunfe safari kuja kututembea maana hapa ni maktaba ndogo.

    emu.3! "Vitabu kama hivyo, kwa watoto ni vizuri sana, nakumbuka vitabu nilivyosoma mimi nikiwa mdogo, kama vya sungura mjanja, bulicheka, safari za sinbad nk, sijui kama vinapatikana! Kwa ninavyokumbuka hivi vitabu vyote ninavyo ni ni kumbukumbu nzuri sana nadhani unamkumbuka BWANA MATATA hicho pia ninacho . Namshukuru baba yangu kwa utunzaji wake mzuri. Na leo wengi wanafaidiaka.

    ReplyDelete