Tuesday, August 17, 2010
Kwanini kuwatumia ma- house girl kama watumwa??
Kuna jambo nimekuwa nikiliwaza na pia nimekuwa nikitumiwa barua pepe na wasomaji wa blog hii ya Maisha na Mafanikio. Wakitaka niandike kuhusu kwa nini tunawatumia sana ma-housegirl/boy(wasaidizi wa nyumbani)kama sio binadamu.
Kwanza kabisa niseme binafsi sijawahi kuishi na/kuwa na msaidizi wa nyumba. Nakumbuka kuna rafiki yangu mmoja aliniuliza:- "kama nina msaidizi wa nyumba, nikamwambia HAPANA, akaniuliza inakuwaje? unawezaje kumudu kazi zote za nyumbani na wakati wote wawili mnafanya kazi?" Nikamjibu tunazifanya wenyewe. Tunasaidiana
Kuhusu wasaidizi wa nyumbni sitakikusema kuwa watu wasiwe na wasaidizi la hasha! Ila tu kuna wakati utakuta wengine wanawatumia wasaidizi hao kama mashine na sio binadamu. Yaani atafanya vijikazi hata ambavyo mke /mume au mtoto angeweza kufanya mwenyewe kwa mfano kufua nguo za ndani(chupi) kuchota/kuchukua maji ya kunywa. Nimewahi. Na halafu la kusikitisha zaidi utakuta msaidizi huyohuyo anatamaniwa na mwisho kupachikwa mimba. nimewahi kusikiliza wimbo mmoja wa Dr Remmy Ongala Hamisa ukisema hivi "Akina mama nao jamani eti mfanyakazi wake anaanguka naye" au pia ni kinyume "akina baba nnao jamani eti mfanyakazi wake anaanguka naye". Na hii inatokea mara nyingi na bado tatizo hili linatokea kila siku katika jamii/ndoa zetu.
Naweza nikasema maisha ya ndoa au maisha kwa ujumla kikubwa zaidi ni KUSAIDIANA:- Nikiwa na maana ni vizuri sana kusaidiana kwani ukimwacha mwanamke afanye kila kitu ndani ya nyumba atakuwa anachoka na mwisho wake atashindwa kuitumikia ndoa yake. Na matokeo yake mume ataanza kutafuta nyumba ndogo. Lakini kama kungekuwa na umoja haingetokea hivi.
Tuwe waaminifu na ndoa zetu zitadumu na tuwatumie wasaidizi wetu kama binadamu, tuaache utumwa.
Tabia za watu zinatofautiana sana, huyu anayewatumia wasaidizi wa nyumbani vibaya ni sawa na wale mabosi ofisni wasiowajali wafanyakazi wao wa chini. Ni tabia fulani mtu anayo ya kujioana, na kudharau wengine.
ReplyDeleteMfanyakazi wa nyumbani ni sawa na mfanyakazi ofisini, alihitajiwa apewe haki zote kama mfanyakazi, lakini tatizo ni hali za kiuchumi na sheria kutowajali sana wao. Kwahiyo kama wewe unaye unatakiwa umpe haki zake ikiwa ni pamoja na kumheshimu na kuheshimu utendaji wake.
Kwa vile tunawachukulia kama ni wasaidizi wa kazi zetu ya kuwa hatuwezi kuwatimizia haki zao kama mfanyakazi wa maofisini(kusaidiana) basi tuwahurumie kwanii tunakula jasho lako! Kuwahurumia huku ni pamoja na kutowabana sana, au kuwafanya watumwa.
Kwa wale waliobahatika kuwa nao wamegundua mengi , kuwa wapo wengine wana tabia ambazo sio nzuri, basi kama ulimchukua kama msaidizi au ndugu , mfanye kama mwanao au jamaa yako, kwa kumkanya pale anapokosea kama vile unvyomkanya ndugu yako. Mpe huduma za kawaida kama vile unavyompa ndugu yako, au mtoto wako, na hapo yeye mwenyewe atajiona ana haki na kuituma kutaongezeka.
Yapo maswala ya utomvu wa adabu pale baba mwenye nyumba anapomfanya nyumba ndogo huyu binti, hiyo ni tabia na hulka za wanaume wasiotosheka au wenye tamaa, lakini na sie akina mama tuwe makini kwa kuhakikisha zile kazi ambazo zinastahili yeye kuzifanya azifanye yeye na sio kumtuma mfanyakzi huyo kutandika kitanda chenu mnacholala wewe na mumeo, au kumtuma maji ya kuoga bafuni, na vitu kama hivyo, pia timiza wajibu wako wa ndoa ili kusiwe na `njaa ya ndoa'na mwisho wa siku jamaa akatamani visivyotamaniwa
Kama unahitaji mfanyakazi wa ndani, basi hakikisha unamfanyia yale ambayo wewe ungependa ufanyiwe, sidhani kama ni sahihi kumnyanyasa kwa sababu ya dhiki zake wakati anakusaidia wewe kazi zako, kwanza unaleta picha gani kwa watoto wako, inamaana unawajengea tabia ya ukatili au chuki sijui nisemeje inakera
ReplyDeleteHmmmmmm, Yasinta acha wivu! labda unawasiwasi wa kupinduliwa! Anyway just kidding.
ReplyDeleteNi ukweli usiopingika kuwa wafanyakazi ndani aidha wawe ni wakike au wakiume hukumbana na manyanyaso toka kwa waajiri wao.
Binafsi nimewahi kushuhudia unyanyasaji na udhalishaji wa mfanyakazi wa ndani toka kwa mwajiri mwenye asili ya kiasia. Pengine hata mbwa asingestahi niliyoyaona yakitokea hapo.
Kweli kuna watu hawawezi kuishi vzr na binadamu wenzao hasa anapokuwa msaidi wa kazi (mtumishi).
ReplyDeleteLakini yote kwa yote kuishi vizuri ama vibaya na mfanyakazi ni tabia binafsi za kibinadamu maana kuna watu wanawafanya watumwa watoto wao wa kambo ama watoto wa ndugu zake wa damu hata wadogo zao.
Bora umerudi tulimiss mambo kama haya.
ReplyDeleteas you think so you become!!!!
ReplyDeleteMmmmmH!
ReplyDeletenikweli dada wengine hawatendi haki hata kidogolakini wafahamu kuwa nao wao ni binadamu pia
ReplyDeleteKuna filamu moja (documentary) inayojadili haya matatizo...
ReplyDeletehttp://vijana.fm/2010/06/04/ziwa-viktoria-mgongowazi/