Thursday, August 26, 2010

India inateswa na malaria tena!!

Anopheles gambiae
mosquito,






P Falsiparum
India inateswa na malaria, hasa Mumbai watu 9000 wamepatwa na malaria.
Hata ile sehemu ambayo watalii wanaipenda Kerala, ambayo inasemekana ilikuwa hakuna malaria kwa miaka kadhaa uiliyopita nako sasa watu wanapata mmateso tena.

Mwaka jana waliambukizwa watu 154 na mwaka huu mpaka sasa wameambukizwa watu 82.
Kuna aina nne (4) za malaria na mojawapo ni P Falciparum ambayo ni hatari sana kuliko nyingine zote. Aina hii inasemekana imeingia India.

Chanzo Aftonbladet la 4/8/2010

8 comments:

  1. Nipe anuani zao niwatumie HATI PUNGUZO.... lol

    ReplyDelete
  2. Sio hati punguzo tu, hapa tuna kiboko ya malaria, hamjaigundua hiyo, upo muarubaini, upo mkwinini, yapo nasikia hata majani ya mpapai, sasa tuitafute hii tenda.
    Wajamani, lakini malaria inatesa, sisi huku Tanzania imekuwa njia ya kutafutia ulaji kwa watu. Badala ya kutafuta njia ya kumuangamiza huyu mdudu mbu watu wanashauriwa kujikinga naye , kama vile ni mtukufu fulani hatakiwi kuangamizwa. au ndio haki za viumbe kuwa kuwaangamiza tutakiuka hakli zao?

    ReplyDelete
  3. emu-three nipe tano. bora osama afe mbu asife. hivi kweli dunia hii na teknolojia yoote imeshindwa kabisa kuangamiza mbu? hapana. nadhani ni biashara za watu flan-flan. hivi mnajua dawa mseto ya malaria inatengenezwa brooklyn , new york? mbako hakuna malaria

    dawa za kutibu malaria nazo balaa. inafaa kabla ya mgonjwa kupewa dawa fulani apimwe mzio (alergy) kwa dawa hiyo. dawa zaweza kuwa tatizo kubwa. ona binti wa waziri magufuli alivyopoteza maisha kwa kunywa dawa ya kutibu malaria.

    ReplyDelete
  4. uuuwii, hii ni habari njema, maana wahindi walivyokuwa wabunifu watagundua chanjo ya hii kitu tu, natamani malaria iingie china, chanjo haraka na mbo watakoma!

    ReplyDelete
  5. Hili gonjwa sijui kama litaisha na sijui kama kutapataikana dawa. Halafu sijui kama kuna umuhimu wa kula kinga maana mwka jana nilikula kinga kila wiki na mwisho wake nini? Nikapata malaria na ikawa chupuchupu.

    Nimekuwa nikifuatilia hili suala la mtoto wa waziri kupewa dawa na zikamdhuru, Nimejiuliza kwa nini hawakumuuliza kama ni dawa gani zinamdhuru na zipi ni safi?

    Hivi ina maana kuna vidimbwi vingi sana Tanzania, India pia sasa Afghistan?
    Nami naamini Kamala ameandika vibaya hapo alitaka kuandika mbu.

    ReplyDelete
  6. Aisee nawapa pole, sjui huu mradi umekuja Tanzania wa vyandarua Sh.500/= unafadhiliwa na watu gani? wangeelekeza huko, manake wanadai chandarua kina dawa inayodumu miaka 5, ila sijaelewa vizu hicho chandarua kama kinafuliwa na hiyo sawa imo tu automatic haichuji au ni vp kweli chandarua kidumu 5yrs kikiwa na dawa.

    ReplyDelete
  7. nawapa pole sana ndugu zangu wa india kwasababu maria hata tanzania inattesa lakini ilikuwa zamani ssana watu saizi wameelika sana tanzania hakuna tena maria watu wanaumwa magonjwa mengine maria siyo kama miaka ya nyuma.

    ReplyDelete