Wengine walikuwa wamesinzia
Niko kwenye daladala, watu wametulia kila mtu akitafakari mambo yake. Mara kaibuka abiria mmoja akavunja ukimya akauliza." WaTanzania wenzangu naomba kuuliza swali". Abiria wote tukageuka kumwangalia. akajitolea dada mmoja akamjibu, "uliza tu baba" unajua aliuliza swali gani? ha ha haaaaa!!
Akauliza:- Jamani mie binti yangu anaolewa tarehe 31 siku ya uchaguzi, sasa aolewe au asiolewe?Maana polisi wasije wakatukamata kwa kufanya sherehe siku ya uchaguzi.
Pakazuka malumbano miongoni wa abiria, wengine wakisema aolewe na wengine wakisema asiolewe kwani watakamatwa kwa kufanya sherehe siku ya uchaguzi. Mpaka nateremka kwenye daladala bado malumbano yalikuwa yanaendelea. Kaazi kwelikweli!!!
Habari hii nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio aishiye jijini Dar es Salaam.
NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA NA PIA MWISHO WA JUMA MWEMA BINAFSI NITAKUWA NAFANYA KAZI. KILA LA KHERI!!!!!!!!!!
Asiolewe kwani uchaguzi msiba? Hehehe...ni hayo tu
ReplyDeleteKama kuna sheria inayopiga marufuku kufanya sherehe ya aina yo yote au mikusanyiko ya watu basi ni wazi vijana wa FFU wataleta usumbufu.
ReplyDeleteJe, watu watakaoshiriki katika harusi hii kweli wataweza kupata muda wa kwenda kupiga kura? - Jambo ambalo kwa maoni yangu ni la muhimu zaidi kuliko hiyo sherehe yenyewe.
Ni vizuri kama atatafuta tarehe nyingine!
Kama kuna sheria inayopiga marufuku kufanya sherehe ya aina yo yote au mikusanyiko ya watu SIKU YA UCHAGUZI basi ni wazi vijana wa FFU wataleta usumbufu.
ReplyDeleteJe, watu watakaoshiriki katika harusi hii kweli wataweza kupata muda wa kwenda kupiga kura? - Jambo ambalo kwa maoni yangu ni la muhimu zaidi kuliko hiyo sherehe yenyewe.
Ni vizuri kama atatafuta tarehe nyingine!
Kaka Matondo kwani kupiga kura lazima?
ReplyDeleteSasa iweje watu wanyimwe kula pilau la kumuozeshwa mwali binti kigoli?
Mie naseme aolewe tena sherehe zianze alfajiri mpaka majogoo.....hakuna kulala.
Kwanza hata kama tukipiga kura, mshindi ashajulikana kuwa ni CCM!
Wenzenu washaiba kura kitamboooo...
Sidhani kuwa siku ya uchaguzi wanakataza mambo mengine ya kijamii kama harusi, sina uhakika wa hilo, lakini kama watakataza basi watakuwa wameingilia imani za watu na hapo watakuwa wamechanganya dini na siasa.
ReplyDeleteMmmmh!
ReplyDeleteIjumaa Njema!
kwana narekebisha swali. je aolewe siku hiyo au siku nyingine? nimerekebisha swali kwani suala la kuolewa liko palepale.
ReplyDeletenajibu swali langu. ndoa ifanyike siku hiyo hiyo ila isiwe umbali fulani tokea kituo cha karibu cha kupiga kura (nadhani mita mia). hata hivyo deployment ya askari ni kwa ajili ya kuzuia vurugu. sio kuzuia sherehe. na askari ni watu ambao hutumia busara kama watu wengine (ingawaje wakati fulani askari huwa hamnazo kukichwa)
kuhusu kujumuika katika harusi na kujumuika katika uchaguzi vyote vinawezekana. nijuavyoo mimi hekaheka za harusi huanza mishale ya mchana (bibi harusi ndio huanza mapema kidogo kwa sababu ya nywele na makarokoro yao). kwa mfano harusi itakuwa na watu 100. woote wanaweza kupiga kura na kushiriki ndoa na sherehe. vituo vya kupiga kura hufunguliwa asubuhi saa 12 ama saa moja. hii inamaanisha hata bibi harusi anaweza kushiriki uchaguzi na ndoa yake.
na katika kfuatilia zaidi ya Mwaipopo, anaolewa wakati gani? Usiku ama mchana....????
ReplyDeleteIjumaa na wikiendi njema!
Mmmmmh!!
ReplyDeleteHarusi haikatazwi lakini wapiga kura ni watu,na wale watu wanawezekana wakawa wanahusika na zoezi la kupiga kula hivyo ikaadhili shughuli za harusi,ni vizuri kutumia zaidi hekima,kupanga siku nyingine.
ReplyDelete