Saturday, August 28, 2010

Kumbukumbu:- Swali la leo nadhani wengi wetu tumecheza michezo hii tulipokuwa watoto au?

Wengi tumecheza michezo hii!!
Ndiyo, Ndiyo!! ndugu zanguni ngoja leo tukumbuke ya kale .. kuna michezo mbalimbali ya utoto ambayo ilikuwa ni burudani, vituko na wakati fulani ilizaa urafiki wa kudumu sana. Michezo ambayo watoto wetu leo hii wanaweza kuona kuwa haina maana tena na wamebakia kucheza na computer, TV nakadhalika.

Kombolela au rede
Kioo kioo
Ukuti ukuti
Kuruka kamba
Hiki na Hoko
Namtafuta rafiki
Tiari bado (mchezo huu ungepigwa marufuku!!!)
Kitambaa changu cheupe
Tukuone maringo yako!
Watoto wangu eh

Upi uliupenda na kwanini?
Kama kuna mchezo nimeusahau unaweza kuutaja.
Jumamosi njema wote!!

11 comments:

  1. Nanukuu "Tiari bado (mchezo huu ungepigwa marufuku!!!)"

    Kwa nini upigwe marufuku??? Ni mchezo hatari ama?


    Kiongozi: Nyama nyama nyama
    Wote: Nyama
    Kiongozi:Nyama ya kuku
    Wote: Nyama
    Kiongozi: Nyama ya mbuzi
    Wote: nyama
    Kiongozi: Nyama ya fisi
    Wote: ......

    Hata sijui huu mchezo ulikuwa unaitwaje...

    ReplyDelete
  2. Da Yasinta kwanini tiari bado upigwe marufuku?

    ReplyDelete
  3. Da Yasinta: kuuliza kama tumecheza michezo hiyo ama la ni sawa na kumuuliza osama kama ana ndevu....lol!

    Uwe na wakati mwema!!!

    ReplyDelete
  4. Sikumbuki kama mchezo wa Tiara ulipigwa marufuku.

    Nakumbuka kaka zangu walikuwa wakisusha hiyo sijui ndio tiara, l;akini walikuwa wakiita Kishada wakati huo..... sina uhakika kama hilo jina la Kishada ni rasmi au ni wao walikuw awakiita hivyo.

    Kuna mchezo mwingine ulikuwa ukichezwa na watoto wa kihuni pale mtaani kwetu, wenyewe walikuwa wakiita "KIDEGE LUKA" Je kuna mdau anaufahamu mchezo huo?

    ReplyDelete
  5. umesahau baishoo i luv u baby

    Keoro, Dada YAsinta kaongelea mchezo wa tairi mtoto anaingia katikati ya tairi halafu mnaanza kuliendesha yeye akiwa ndani, na hasa kama kuna mteremko mahali basi mnaliachia, ni mchezo wa hatari hasa sasa ambapo magari ni mengi

    ReplyDelete
  6. Naona nimechelewa kidogo kujibu swali lenu kaka matondo na mtani Fadhy. Kwani kaka Bennet amejibu kuwa "Tiari ni mchezo wa tairi mtoto anaingia katikati ya tairi halafu mnaanza kuliendesha yeye akiwa ndani, na hasa kama kuna mteremko mahali basi mnaliachia, ni mchezo wa hatari hasa sasa ambapo magari ni mengi" hii ndiyo sababu ya kupigwa marufuku. Halafu nilisahau mchezo mmoja tena mnakuwa wawili au watano hivi na mnainama huku mnashikana mabega aliyetangulia anaangalia na wengine mnafumba macho unaaenda hivi:-


    wote: tumefika
    Kiongozi: bado
    ni hivyo hivyo mpaka mkifika muendako kiongozi atajibu tumefika.

    ReplyDelete
  7. kombolela ulitumika kujifundisha 'mambo' fulani huko walikokuwa wakijificha.

    ReplyDelete
  8. Kuna mchezo tumeusahau unaitwa kula umbakishie baba, mnaweka lundo la mchanga na kijiti kati kati, halafu mnakuwa mnatoa mchanga kidogo kidogo kama vile ndio mnakula chakula, sasa ukila sana na kijiti kikadondokea kwako basi unakula mkong'oto mpaka ouakshike ukuta au kitu mlichi kichagua

    ReplyDelete
  9. michezo jamani inankumbusha mbali sana hasa mimi nilikuwa napenda sana kucheza mchezo wa kuruka kamba .Nilikuwa napenda kwasababu nilikuwa nikiruka kamba nilikuwa naona furaha sana alafu nilikuwa napenda sana michezo nilikuwa nikirudi tu shule natafuta rafiki zangu ili tuweze kurahi nao pamoja nashukuru kwa kutukumbusha enzi yetu ya zamani .asasnte

    ReplyDelete
  10. Katika hii michezo uliyoitaja, mimi nilipendelea kucheza rede.
    kwasababu iliniburudisha sana na vili vili iniweka fiti kimazoezi.

    ReplyDelete