Saturday, July 24, 2010

UJUMBE WA LEO NI KUTOKA IRINGA!!! UREMBO AU KUSOMA???

Je? utamaduni wetu upo wapi?

Kwako dada Yasinta, mimi ni msomaji wa blog ya maisha na mafanikio .Ninakuomba uufikishe ujumbe huu. Ni kwamba ningependa kupata maoni ya watu mbalimbali hapa ambapa hawa dada zetu wa
vyuo vikuu vya Tanzania wanafanya mashindano ya urembo. Kwa mtazamo wangu
watanzania tulipa gharama za hawa kusoma sasa ni kupoteza muda kufanya mambo ya
urembo.

Pengine cha kusitisha zaidi pamoja na kuwa ni mambo ya urembo pia hayana ubunifu
wowote ule. Inachoonekana hawa dada zetu wa vyuo wananukuru mambo ya
ulaya/Marekani kama yalivyo wanashindwa hata kufanya ubunifu ili waweke hata
utanzania kidogo. Kwanini wamevaa vikaputa badala angalau ya kufunga kanga au
kitenge au vinginevyo. Hata Japan au China mashindano haya yapo lakini
wameyafanyia marekebisho kidogo kuwa ya kichina/kijapani aidha kubadili mavazi
au vinginevyo. Sisi watanzania tena kama kawaida yetu tunanukuru tuu. Siyo
kwamba sipendi hawa watu waonyeshe urembo wao hapana ila tuwe tunaweka
u-tanzania kwenye hivi vitu la sivyo tutabaki kuwa watumwa wa tamaduni za watu
wengine.
Picha hii ni hisani ya Mjengwa blog. http://www.mjengwa.blogspot.com/

2 comments:

  1. Binafsi kuhusu mashindano ya urembo kwenye ngazi ya vyo sioni kama inatatizo.Maana hata kama upo chuo kuna kipindi unabidi unapumzisha BONGO zaidi ya hapo unaweza kuchizi.

    Hivyo kikubwa ni kufanya hayo mambo kwa nidhamu.Kuhusu mavazi ilo nikubwa zaidi.

    Mimi sioni tatizo la kaptula mbona tuna makabila watu wanajifunika tu tungozi mbele na nyuma ya maungo ya uzazi? sasa hapo vipi?

    Tuna makabila ambayo hadi baba wa taifa ilibidi atumie nguvu kuwashawishi wakina dada kusitiri nyonyo maana kwa sio issue..

    Ila kama ulivyosema ni vizuri kwenye mashindano hayo ya urembo kuweka ubunifu na utaifa mbele.

    ReplyDelete
  2. Mimi naona mashindano ya urembo hayasaidii kabisa ndiyo mtu unahitaji break lakini msomi serious hahitaji kwenda kwenye mashindano haya. Jamani kweli sisi tunahitaji hivi vitu au tuu tunaangalia na nukuru kwa sababu tuu vinafanya ulaya?

    ReplyDelete