Unajua na labda hutaki kuzingatia
1. wewe unajua mimi sijui
2. Mimi najua wewe hujui
3. Wewe unajua mimi sijui
4. wewe hujui na mimi sijui.
Leo katika pitapita zangu nimepata kumsikiliza Mshairi mahiri wa Tanzania Mrisho Mpoto. Katika kumsikiliza maongezi yake ambayo yalifanyika na Bongo Tanzania TV 3/12/ 2009. Aliyatamka maneno haya ambayo katika maisha kuna milango yenye madirisha mnne. Nimeupenda sana usemi huu na nimeona nigawane na wenzangu na madirisha hayo ni:-
1. wewe unajua mimi sijui
2. Mimi najua wewe hujui
3. Wewe unajua mimi sijui
4. wewe hujui na mimi sijui.
Kwa hiyo ukijua ni diriasha gani zuri la kukufanya uishi vizuri na watu basi utaishi kwa raha mustarehe, shangwe na nderemo na mashasha katika nafsi yako.
Mrisho kwa visa si mchezo.
ReplyDeleteDada Yasinta naona ya tatu inarudia ya kwanza;sijui Mrisho alikusudia au la?Mimi naona pengine ingebidi moja iseme "wewe unajua mimi najua" ili madirisha yawe yamekamilika.
ReplyDeleteAsante na ubarikiwe sana!