Tuesday, June 15, 2010

LAU KAMA WANAUME WANGEKUWA WANANYONYESHA!!

Tujikumbushe hili. Hivi ingekuwa wanaume ndio wananyonyesha watoto na mihasira yao sijui ingekuwaje?. Lakini Mungu kwa kuona mbali akaona hapana. Kama mwanaume ataona mtoto ni wake kwa ubini wa jina lake na kwa ubabe lakini watoto watanyonyweshwa na mama zao. Ukiwa kama baba umejaribu kumpa mkeo upendo wa ziada kuwa anayofanya kwako, kwa watoto na familia kwa ujumla?
Kumbuka mwanamke hata akipita vitani wanajeshi hushauriana kama wamuue au la. Mwambie mkeo Ahsante kwa yote!

5 comments:

  1. Duuh...hii kali kweli. Lakini ni kweli kabisa, lazima tuwaheshimu sana akina mama kwa kazi kubwa wafanyayo kwa malezi ya watoto. Maaana si mchezo kulea mtoto.

    Hongereni sana akina mama wotee Duniani.

    ReplyDelete
  2. Swali na mada ya kipumbavu hii.Kila binadamu ana nafasi yake katika jamii na katika familia.Ndivyo ilivyo,ilivyokuwa na itakavyoendelea kuwa.Zipo kazi ambazo mwanamke anamtegemea mwanaume na vice versa.Tunaokosea ni sisi wanadamu(wenye fikra kama zako)tunaojaribu kuubadilisha usiku kuwa mchana.Ole

    ReplyDelete
  3. Nahisi Anony ni mkurya kama mimi ...lol!

    Nadhani anamhitaji mama mchungaji ampe mawaidha kwa kuwa sidhani kama amesoma kichwa cha mada na kama kasoma hajakielewa!

    Na kama hajakielewa si kosa lake...lol! Dunia ni mzunguko na hasa kwa wasojitambua!

    ReplyDelete
  4. Ha ha ha ha ha SWALI LA KIPUMBAVU? sasa nani MPUMBAVU BIN MWENDAWAZIMU kati ya muuliza SWALI NA WEWE UNAYEDAI NI UPUMBAVU(namuuliza Anon hapo juu Juni 16).

    KUNA UPUMBAVU SUIOKUWA NA UKWELI? kama tungelijua thamani ya kumheshimu binadamu anaytupatia changamoto na yule anayetukana kwa changamoto za KIPUMBAVU? Moja ya sifa za WAPUMBAVU NI KUTUKANA na kujivunia UPUMBAVU WAO. na sifa kuu ya MPUMBAVU ni kufanya mambo ambayo yana maanisha UPUMBAVU.

    Nikisoma mada ya Yasinta, imenipeleka palepale ninaposema HII NI AJALI KWA WANADAMU, na nakubaliana na Prof Mochiwa, kwamba watu wanazaliwa hawakuchagua jinsia. Na hapo swali linaelekea kumwuliza huyo MUNGU? sasa kama nathubutu kumwuliza Mungu swali. Wewe ni nani hata UPINGE MASWALI NA KUDAI NI UPUMBAVU.
    SIFA YA UPUMBAVU ni wewe kuwa na OMBWE la akili na msaragambo wa KALIBA YAKO. SWALI kuna mambo mangapi yanakukera lakini hujayaita ya KIPUMBAVU. Je waulizaji maswali wote ni WAPUMBAVU?? Na wale WAPUMBAVU wanasifa ipi kama siyo wewe ukiwemo kati ya WAPUMBAVU?

    unafikiria kuruhusiwa kuchanga maoni huru ni lazima kutoa matusi NA kujionyesha wewe ni bingwa wa HOJA?
    MALCOLM X alisema ukitaka kupambana na adui jifunze lugha yake. SASA kama wewe anon unadhani kUTUKANA NI SILIKA YAKO, basi UPUMBAVU NI SHEMU YA MAISHA YA WANADAMU UKIWEMO WEWE KIONGOZI WA WAPUMBAVU.

    Vinginevyo utakubaliana na mimi kuwa MPUMBAVU WA KWANZA NI MUNGU........ unayeamini yuko huko kusikojulikana

    ReplyDelete