Mwisho wake hutuletea maumivu
Bado nina ndoto za Alinacha, leo nikiwa nimejipumzisha hapa kwangu, nikawa najiuliza. Hivi ni nani aliyevipa vito na madini thamani? Je mtu kumiliki vito na madini yenye thamani ni ili iweje?
Kuna siku nilipita duka moja linalouza vito na kukuta kuna ulinzi mkali ajabu, na si hayo tu bali pia visa vya wanawake kukatwa masikio na kujeruhiwa shingo na vidole vya mikono wakiporwa Pete, Hereni, Cheni za Dhahabu na vito vya thamani haviishi kila kukicha.
Kuna wakati nilipokuwa nyumbani Tanzania niliwahi kukoswa koswa kukatwa sikio na vibaka wakitaka kunipora hereni zangu za dhahabu, na kama sio wifi yangu kuwahi kupiga kelele, leo hii Yasinta ningekuwa na sikio nusu.
Labda niwaulize wanawake wenzangu, hivi hizi Lebasi za Ulimbwende zatufaa kitu gani il-hali zatuhatarishia maisha?

mtakapo jua kuwa uzuri umo ndani mwenu na sio nje yenu ndipo mtakapoachakuvaa vitu vya kijinga kijinga na kujichooooora utadhani nini sijui
ReplyDeletezawasaidia kujionesha kuwa hamjithamini kwa ndani bali kwa nje tu!
ReplyDeletekaazi kwelikweli
watu na akili zao wanavaa MAWIGI yaani nywele ya bandia. watu na akili zao wanavaa kucha za bandia. watu na akili zao wanavaa nguo za kubana makalio. watu na akili zao wanapaka masizi, na uchafu usoni kwao. NANI ANATAKA HUO UREMBO WA SANAA??? MCHARUKO HUOO
ReplyDeleteHeleni za dhahabu, cheni za dhahabu, mipete ya dhahabu na vitu vya vito vito kuvaa, ukiwauliza wanawake wa Kigambia, Senegal au Waarabu watakupa jibu sahihi.
ReplyDeleteSwali kama hilo ukiwauliza dada zangu wa Kitanzania utakuwa huwatendei haki, maana hawajui sana maana yake japo wanavaa, labda umvae dada wa Kizenji.
Ni sawa kumbandika swali la aina hiyo mwanaume wa Kikongo, minyororo ya silva wanayoivaa shingoni kama "mbwa" ina maana gani. Hawezi kukupa jibu la kukuridhisha.
Mkongo yeyote hata kama utamwuuliza kwanini wanapenda kusimama mbele ya magari ya bei mbaya, wakati wakipiga video zao za miziki. Hajui sababu yake. Kwao hakuna neno "Ushamba".
It's Great To Be Black=Blackmannen
Hii ya leo ni kali sasa wangekukata kwani siungepona? huoni kama ukivaa hayo madude unakuwa mzuri daima? au unafikiri ukiacha kuvaa machinga wataishije? hujui kama hata serikali inaingiza fedha nyingi sana za kodi kwa ajili ya urembo? ila na nyie wanawake mmezidi mbona hata mitindo imewaishia mpaka mnadiliki kuvaa nguo ambazo mabega wazi,nguo gani hizo? anyway sijui
ReplyDelete