Wednesday, June 2, 2010

SWALI LA LEO:- HIVI NI KWELI HAPA DUNIANI MUNGU AMETUUMBA WAWILI WAWILI??

Mama Mubelwa /Mzee wa Changamoto au hapa
changamotoyetu.blogspot.comDada Agness Andersson kiduchu.blogspot.com
Mwenzenu nimechoka kufananisha peke yangu na leo nimeona niwashirikishe wenzangu au sijui ndo uzee unaniingia? Je? Hawa watu kweli hawajafanana?

7 comments:

  1. Unajua Dada Yasinta mimi pia nina hako kaugonjwa mwenzako,na ndio maana ktk MNM Blog nina hako ka-segment kila ijumaa,hao wadada kwakweli wanafanana,tena sana tu,Agness namfahamu vzr sana coz nafanya nae kazi,na nilipoiona hiyo picha ya huyo mdada mwingine wallah nikajua Aggy,kweli vile,hauzeeki,ni kweli wamefanana,tena sana tu.

    ReplyDelete
  2. kamala - loool!...Fadhy - mtafute au? lol

    anyway wamefanana kwa kweli...they should meet..

    ReplyDelete
  3. Mimi nilishasema siku nyingi, lakini labda tungepata picha zaidi za Mamaa wa Changamoto ili tuone akiwa katika mapozi mengine kama bado wanafanana.

    Hivi Kamala wewe vituko utaacha lini? Umenifanya niangue kicheko.

    ReplyDelete
  4. Da Mija taratibu bibi. Utajakuta ukiangalia hizo picha zaidi unazozitaka utaona wanafanana na mimi sijui itakuwaje?

    Si unaona shida unayotaka kuniletea? ....lol

    Nakumbuka nikiwa sekondari moshi tulikuwa wawili twafanana majina na sura.

    tatizo la yule tulofanana naye jina ilikuwa ikija TMO yeye ndo alikuwa akiifuata kwa kuwa alikuwa ananizidi kidato hivo HM akaamuru mie niongeze jina la 3.

    Yule alokuwa anafanana nami sura alikuwa mtorokaji sana akienda kwao shirimatunda kula maparachichi na mbege hivo miye ndo huwa nilikuwa napata kibano pale atakapofumwa huko town na kumtoroka mwalimu... :-(

    Unaona ubaya na utamu wa kufanana?

    ReplyDelete
  5. Kamala! nafurahia kuzeeka:-)

    Kaka Renatus! nimepita kwenye blog yakona nimeona lakini nimeshindwa kutoa maoni. Sijui kuna shida gani? 100% hawa watu wamefanana yaani mpaka mtindo wa nywele.

    Mtani Fadhy! subiri nimtafute aliyefanana nawe yupo tu.

    Au vipi Cindy1?

    Da Mija! najua ulisem. Kwa taarifa yako Kamala hataacha vituko mpaka siku ya mwisho....

    Ha ha ha ha! kaka Chacha kaniumiza mbavu kweli pole sana kwa kufanana na huyo mtu na kila kosa likawa lako..ha ha ha ahahuo si utamu ni UBAYA .. kaazi kwelikweli!!!

    ReplyDelete