Thursday, June 3, 2010

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KWAKO ERIK!!

Imetimia miaka 10 leo tangu kijana wetu Erik azaliwe. Ni kijana ambaye anapenda sana kusoma, kuandika, kucheza mpira wa miguu (football), kuendesha baiskel na marafiki mountain bike pia anapenda kupiga aina ya mziki wa fidla au (Violin. ) Twakuomba Mwenywezi Mungu uwe /uzidi kumbariki kijana wetu Erik azidi kuwa kama na hekima . Na pia twakoomba uzidi kutupa sisi wazazi/walezi nguvu ya kumlea ili azidi kuwa kijana mwema na mwenye busara. ERIK HONGERA SANA KWA SIKU YA KUZALIWA.

21 comments:

  1. Hongera sana Erik kwa kutimiza miaka 10. Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akujaalie afya njema na mafanikio tele. Ukue katika hekima na iwe faraja kwako na kwa wazazi wako.
    Heri kwa sikukuu ya kuzaliwa!

    ReplyDelete
  2. Erik Mama yako anaWIVU na wewe kuna SIFA MOJA hatataja...... nina hasira naanza kulia aaaaaaaaahhhh ooooooohhhh uuuuwiiiiiiiii ayyyyyyaaaaa khaaaaaaaaa mmmmmmmhhhh... Lol ametaja sifa zile safi kabisa lakini amesahau kuwa mwanae ERIK K.T anapenda sana KUKIMBIA/MAZOEZI YA KUKIMBIA. Hii ni sifa adhimu sana hajataja nina hasira nayo nalia tena uuuuuwwwiiiiiiii aaaaaahhhhhhh mmmmmmmhhhh.

    Erik mtoto mwema,
    umepata wazazi wema,
    wenye mengi mema,
    na malezi mema,

    makuzi wapata mema,
    upendo mwema,
    mungu akupe mema,
    kila siku njema,
    wahesimu baba na mama,
    amana ya mema,
    siyo benki au hisa,
    bali heshima njema,

    Mzee wa Lundu nyasa
    mengi nakuombea,
    ukue vyema,
    kwa wazazi wema,
    mengi utapewa,
    mwana tulia sema,

    Mungu akupe kila lililojema na mwana wa Nazarethi kwa Joseph na Maria wakulinde zaidi. Miaka kumi siyo mchezo Erik a.k.a Rastaman au Brothe Erik.

    BABA MIKONI MWAKO TUNAKUOMBA UMLINDE KIJANA HUYU daima. amen

    ReplyDelete
  3. Mtoto mzuri Erik,
    Twamwoma Mungu akubariki,
    Akulinde katika mikiki,
    Ndani ya hii dunia.

    Mungu akupe afya njema,
    Akwepushie mbali homa,
    Akubariki katika kusoma,
    Akili zaidi kukujalia.

    Akufanye mtoto mzuri,
    Kwa wazazi uwe johari,
    Nao wakwonee fahari,
    Kama maua ukachanua.

    Daima akujalie busara,
    Ili usiwe nazo papara,
    Wala mtu mwenye hasira,
    Bali mwenye kutulia.

    Uwe mtu mpatanishi,
    Daima pawapo ubishi,
    Jiepushe ulalamishi,
    Dunia utaifurahia.

    Ujaaliwe upendo tele,
    Nyumbani nako shule,
    Usiwatenge watu wale,
    Wala kuwachukia.

    Uwe mtu wa sala,
    Hata kabla ya kulala,
    Na wakati wako wa kula,
    Uwaombee wenye njaa.

    U kama jemedari,
    Kwa wako umahiri,
    Simama kwenye mstari,
    Mungu atakusimamia.

    Heri ya siku ya kuzaliwa,
    Maisha marefu utapewa,
    Daima unaombewa,
    Na mema tunakutakia.

    Wasalaam,
    Anko Fadhy.

    Shairi hili pia linapatikana hapa.

    ReplyDelete
  4. picha inaonyesha hata karate anacheza ila mama yake amebinya ili tusimuogope. LOL

    be blessed little man

    ReplyDelete
  5. hongera sana Erik,Ukuwe uwe na busara na upendo kama mama yako.Mungu akulinde na akuzidishie miaka mingi duniani.

    ReplyDelete
  6. Mamaaaa! juzi tu tulikuimbia happy birthday,ukiwa na baskeli yako,he! mara mwaka umekatika?

    Hongera sana Erik kwa siku yako ya kuzaliwa,mungu azidi kukunyooshea njia ili utimize ndoto yako,pia mungu azidi kuwapa afya njema wazazi wako na kuwaongezea busara,uwe na siku nzuri pamoja na familia yako.
    xoxo!

    ReplyDelete
  7. Haya Yasinta ongeza sasa, kina Erik na dadake watakusaidia kulea mdogo wao......!!

    Erik hongera sana kwa kutimiza miaka kumi, Mungu azidi kuwa nawe na familia yote kwa ujumla.

    Kila la heri.

    ReplyDelete
  8. Nimekuja kuunga mkono ushauri wa da Mija.

    ReplyDelete
  9. Nafikiri Da Mija ana pointi hapo. Sweden HAIJAJAA hata kidogo na bado twahitaji wengine wengi. Hasa kama "chata" zenyewe ni nzuri namna hii.
    Hivi kutozaa vya kutosha si dhambi kweli? Hasa kama uzao wako una vipaji na masuluhisho mengi namna hii?
    Nimepenyuka kuandika. Hata sitakiwi.
    HONGERA "Uncle" Erik. Hongera FALIMIA nzima ikuhusuyo Da Yasinta (ikitujumisha ma-bloggers)

    ReplyDelete
  10. Erik hongera sana kwa kutimiza miaka 10 Mungu akujalie maisha marefu yenye furaha na afya tele akuzidishie busara na kila yaliyo mema akujalie.

    Happy Birthday Erik

    ReplyDelete
  11. erik!

    i have been your sister since you were born and iam very glad for that. you means a lot to me.

    ReplyDelete
  12. Hongera sana tena sanaa kijana Erik....!!!! Pia hongera nyingi kwa wazazi wako, kwa kukulea na kukutunza vizuri. Nakutakia kila laheri kwa yote yawe mema na mazuri daima katika haya maisha.

    ReplyDelete
  13. siku hizi blog zenu zimekuwa za ma-birthday,anyway heri ya siku ya kuzaliwa mjomba

    ReplyDelete
  14. Hongera sana kujana..umefanana sana na mama yako. vibinti wa mtaani watakuletea kokoro sana!!

    ReplyDelete
  15. Mungu azidi kumwangazia nuru njema kila kukicha

    ReplyDelete
  16. Happy belated birthday Eric, endelea kuwa mtoto mzuri, msikivu na hodari. Mwenyezi Mungu akupe umri mrefu ufikishe miaka 101.

    Bi Mkora

    ReplyDelete
  17. kwa niaba ya Erik n apenda kuchukua nafasi hii na kuwashukuruni wote kwa kupongeaza siku yake ya kurimiza miaka kumi. Aanawashukuru akina mama wakubwa na wadogopia akina dada wote kwa mioyo yenu minyoofu pia wajomba wote. Ahsanteni sana nawapendeni wote.Upendo Daima..

    ReplyDelete