Tuesday, May 11, 2010

Wanafunzi Songea waomba elimu zaidi ya Ukimwi madarasani

Wanafunzi mkoani Ruvuma wakiimba wimbo wa pamoja kwa vitendo

TATIZO la wazazi pamoja na walezi kutokuwa wawazi kwa watoto wao hasa wakati wanapotakiwa kuwaeleza kuhusu maswala ya afya ya uzazi na ujinsia ni moja ya tatizo kubwa chanzo linalonachangia kuongezeka kwa wanafunzi wanao ambukizwa virusi vya ukimwi katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Tuliani iliyopo kijiji cha Lilondo kata ya Wino wameona ni bora wawaombe walimu wao kuwasaidia kutoa elimu ya ugonjwa huo kwa undani zaidi madarasani ikiwa ni pamoja na kuongeza vipindi hivyo ambavyo vitasaidia kuzungumza kwa kina ili wanafunzi hao waweze kutambua na kujilinda wasiambukizwe na maradhi hayo ingawa wapo ambao tayari wameshapata maambukizi hayo.

Wanafunzi hao walisema , ingawa wanafundishwa somo la ukimwi lakini bado kuna vitu vingi hawajui kama njia mbali mbali zinazochangia kuambukizwa virusi vya ukimwi na namna ya kuishi na ugonjwa huo kwa watu ambao wameshambukizwa.

Mwanafunzi Joseph Mwenda (12) wa Darasa la nne shule hiyoamesema, bado wanafunzi wanahitaji elimu zaidi ya ukimwi kwani wamekuwa wakifundishwa juu juu bila kuelezwa namna ugonjwa huo unavyoambukizwa hivyo kuwaacha njia panda.

“Najua ukimwi ni ugonjwa hatari mwalimu mgina ametufundisha ila hajatueleza unavyoambukizwa unavyoenezwa hatujafundishwa darasani ila nimeona mtu anaumwa mama akaniambia anaumwa ukimwi alikuwa anakohoa sana na hawezi kutembea kabisa,”alisema Mwenda.

Kwa upande wake Notigeo Mlowe Mwanafunzi wa darasa la tano anasema si vibaya iwapo walimu watawasaidia kuwaelewesha wanafunzi kwa undani zaidi lakini wafanye hivyo kwa wanafunzi wenye umri mkubwa kidogo kwani wakiwaelekeza wote wengine ni wadogo hawajui chochote.

Anasema,kuna mwanafunzi mwenzao anaishi na virusi vya ukimwi lakini wamekuwa wakimsaidia kumfundisha maswali na kumfundisha michezo mbali mbali ili asijisikie vibaya ingawa kuna wanafunzi wengine wanamwogopa kutokana na kutopata elimu ya kuishi na wagonjwa wa ukimwi.

"Tuna mwenzetu anaumwa ugonjwa wa ukimwi mtoto huyo anateseka kwani mama yake hamtunzi bali anaishi na kaka zake tu uwa anaumwa hadi tunamwonea huruma hata afya yake siyo nzuri na ana furaha kabisa,"anasema

Mwanafunzi huyo kuwa , iwapo wazazi wataendeleea kuwa waoga basi kuna uwezekano watoto wao wakaambukizwa ugonjwa wa ukimwi bila wao kujua kwani watoto wengi wanapenda kuishi maisha mazuri na wanadanganywa kwa kununuliwa vitu vidogo vidogo.

Anasema,Kuna wanafunzi wengi wanadanganywa na kufanya ngono na watu wakubwa ila wazazi wao hawajui sasa wakielezwa watajua na kuogopa kufanya hivyo ,kwani watajua ni hatari katika maisha yao.

Aidha Notigeo anawaomba watu wenye mapenzi mema kuendelea kuwatunza watoto na kuacha kuwaambukiza magonjwa ya zinaa, kuwapatia mimba na kuwaaambukiza virusi vya ukimwi kwanihata wanaofanya hivyo nao wanawatoto ipo siku Mungu hatawaadhibu kwa matendo yao.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Rajab Mtiula amewataka wanafunzi hao kufanya bidii zaidi katika masomo yao na kuacha kujiingiza katika matendo ya ngono kwani yatawaharibia maisha yao.

Aidha ameshauri kuwa walimu waendelee kutoa elimu hiyo madarasani ili wanafunzi wapate elimu hiyo kwa undani zaidi na kuweza kujilinda wasipate maambukizi ya ukimwi.kwani hali ya maambukizi katika wilaya hiyo ni ya kutisha na imekuwa ikiongezeka siku hadi siku.

ni vema wananchi wakawa wawazi na kutoa taarifa sahihi iwapo ndugu au jamaa zao watabainika kuwa wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi watoe taarifa za kifo chake ili kupunguza kuendelea kuenea kwa maambukizi.

“Nawaomba ndugu zangu tujenge tabia ya kuwa wawazi , ni vizuri sasa tuwe tunaambiana ukweli iwapo kuna watu watapoteza ndugu zao kwa ugonjwa wa ukimwi basi wawa wawazi ili kusaidia watu wengine wasiambukizwe zaidi pia kusaidia kupatikana takwimu sahihi za watu waliokufa kwa ugonjwa huo hapa kwetu,”alisema Mtiula

Mtiula ,anasema hadi sasa idadi ya wagonjwa 5281 wanaoishi katika halmashauri hiyo wamesajiliwa na kuanza kutunia dawa za kupunguza makali ya ya virusi vya ukimwi.

Amesema,takwimu zilizopatikana katika vituo vya afya zinaonyesha kuwa wagonjwa hao wamesajiliwa katika kipindi cha januari hadi octoba 2009 ambapo kati yao wanawake ni na wanaume ni 2357 ambapo 158 walifariki katika kipindi cha mwaka 2008-2009 ambapo wengi wa wagonjwa hao ufia nyumbani hivyo takwimu zao kutopatikana .

Joyce Joliga,Songea wa Gazeti la Mwananchi

4 comments:

  1. "TATIZO la wazazi pamoja na walezi kutokuwa wawazi kwa watoto wao hasa wakati wanapotakiwa kuwaeleza kuhusu maswala ya afya ya uzazi na ujinsia .........". Hao wazazi na walezi elimu hiyo waliipata wapi? wanawezaje kuitoa kama watakuwa hawana? Labda kuwajenga watoto katika maadili yanayofaa. Pia kuna suala la mipaka. Elimu ipi ya afya ya uzazi inayofaa? tukifaulu hapo watu wetu watakuwa na ufahamu tisha juu ya ukimwi. Suala jingine liwe kujikita katika elimu ya afya ya uzazi na mitindo mbalimbali ya maisha na chaguzi. Elimu hii apewe nani? Jibu liwe jamii nzima ya Tanzania. Tunao watu wakufundisha? Sijui. Njia za kufundishia? zipo kibao? Hapo utagundua kisomo cha watu wazima na kisomo chenye manufaa hakikwepeki!!
    Alamsik

    ReplyDelete
  2. je ni kweli wanahitaji elimu ya malango (sex education)?

    Mmmmmh! Itajakuwa watoto wa shule za msingi wanataka kondomu ya saizi yao :-(

    ReplyDelete
  3. Ndugu shikamoo!kidole kwenye paji la uso.

    Naungana na kaka Chacha. Binafsi inakera sana basi tu kwakuwa sina namna.

    Ni vema kuwafundishi jambo hilo wakiwa kidato cha pili, nimeona wengi wana umri mdogo na kwa kidato cha pili ndipo hasa mabadiliko makubwa yanatokea. Lakini tukidanganyana kwamba tuanzishe madarasa ya kufundisha hilo, NITALIA BUREEE.

    Pili niseme UKIMYA WA WALEZI NA WAZAZI nao unakera sana basi tu, sina namna. Matokeo yake eti VIJANA WA SIKU WAMEHARIBIKA.Ebo nani kawazaa hawa? Mcharukoooooo huo

    ReplyDelete
  4. I am happy to find you Yasinta,even if just to say hello Marlow will be possible.

    A hug

    & & S.I. & &

    ReplyDelete