Sunday, April 25, 2010

NGOJA LEO TUSALI KWA PAMOJA :- SALA YA ASUBUHI

Siku mpya inaanza, Nimuabudu Mungu kwanza,Mungu wangu baba yangu, upokee shukrani yangu. Wewe kwa usiku mzima, ulikuwa kwangu daima,kunilinda kwa amani na mitego ya shetani. Kwako baba wa milele, Ninaomba neema tele, Niepuke dhambi zote. Nikutumikie pote. Ubariki kazi yangu, Shida na furaha Zangu. Mama safi ee Maria, Nipe msaada wako pia. Ee malaika kiongozi, Nipeleke kwa Mwokozi. Yesu nijalie neema, Niwe daima mkristo mwema. Amina.

NA KUMBUKENI NI JUMAPILI YA 17 YA MWAKA. JUMAPILI NJEMAZ WOOOOTE!!!

10 comments:

  1. NOJA LEO TUSALI......

    ReplyDelete
  2. Jumapili njema na wewe dada pamoja na familia!

    ReplyDelete
  3. ni jambo jema kumkumbuka Mwenyezi Mungu.

    ReplyDelete
  4. Nawashukuruni wote kwa kutochoka kutembela hapa kwangu na nafikiri wote mmekuwa na jumapili njema binafsi jumapili yangu imeishia kazini. Mbarikiwe wote!! UPENDO DAIMA

    ReplyDelete
  5. Da Yasinta: hatuchoki kukutembelea kwa kuwa kuna chakula (elimu na habari) twaja kudoea...lol

    Aksante kwa sala!

    ReplyDelete
  6. Jumapili njema na wewe.

    ReplyDelete