Saturday, April 24, 2010

HONGERA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA MARIA FIDELIA NKUGI BINTI WA Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!


Nimeona nami nikuweka hapa mna kukutakia siku yako ya kuzaliwa. Napenda kukutakia siku hii maalum HONGERA sana kwa siku yako ya kuzaliwa na nakutakia maisha marefu na mema. Pia ukue, uwe na afya njema na uwatii baba na mama na watu wote katika dunia hii.

4 comments:

  1. Mwe, haka kabinti malaika kazuri haka kumbe ni uzao wa Chacha? mwe, eee Mtoa uzima Umbariki huyu mtoto pamoja na wazazi na walezi wake waweze kukuza na kumlea vyema! Uwabariki na wale wote watakaokuwa na moyo wenye nia njema kumwongoza mtoto huyu katika njia ya haki.
    Namwombea na kumtakia mafanikio mema katika siku zake za kuwepo hapa duniani!
    Hongera Chacha!

    ReplyDelete
  2. Sitaki kubaki nyuma,
    Nami nataka kusema,
    Kaka ana katoto kema,
    Mola akajalia salama,
    Maisha yawe mema.

    Heri ya siku ya kuzaliwa.

    ReplyDelete
  3. nami nakutakia kila la kheri. HONGERA SANA KWA SIKU YAKO!!

    ReplyDelete
  4. Aksanteni kwa wote wajameni kwa kumtakia kheri binti Nkugi.

    ReplyDelete